Elections 2010 Tuangalie luninga gani?

Rwechu

Member
Mar 17, 2009
85
20
Nimekuwa nafuatilia kwa makini taarifa za habari za Tv mbalimbali tangu kampeni zimeanza na nimeona yafuatayo.

MLIMANI TV, Hii ndio Tv pekee ambayo imeonekana kuwa fair kwa vyama vyote na inatoa taarifa za kampeni zote zinavyoendelea bila upendeleo, habari yao inaanza saa moja na nusu jioni.

TBC1, hii ndio Tv ya taifa lakini imeonyesha upendeleo wa wazi kwa chama tawala, hata wanapoamua kuongelea habari za upinzani hawaoneshi picha au wanaonesha picha zilizopitwa na wakati au sehemu ambapo wapinzani wana watu wachache kwenye mkutano wao. Kumbuka pale jangwani slaa alipokuwa anatafuta wadhamini walimuonyesha yeye tu tena kuanzia kiunoni kwenda juu kana kwamba alikuwa anahutubia hewa.

ITV, Pamoja na mengi kuonekena mpiganaji lakini naona ccm wmeisha muweka sawa maana Jk na kampeni zake anapewa airtime kubwa mno na upande wa wapinzani hawana muda wakujua kinachoendelea.

Chanel 10, Hii ndo kabisa hawana muda wakujua kampeni za wapinzani zinaendeleaje, wanaripoti za ccm tu, any way nadhani wengi wetu mnajua wamiliki wa sasa wa kituo hiki so haishangazi.

Star Tv, Hii sijafuatilia kujua vizuri muelekeo wake maana habari zinagongana za vituo vingi saa mbili kamili so no comment.


Wanajamvi manaonaje vituo vyetu vinavyotoa nafasi kwa vyama vya siasa?
 
Kaka uko sawa, Mimi pia na mitazamo kama yako ila star TV huwa naangalia pia bado wana kawoga kadogo japo ni wazuri kwenye kusoma habari zilizoandikwa na watu wengine (Yaani kutoka magazetini). Mlimani TV mimi nadhani ni kweli wanaripoti wanachokiona kwa wote japo coverage yao ni ndogo na nadhani pia hawana staff wa kutosha kuweza kukusanya habari nyingi na sehemu mbali mbali.
Ndo hivyo hao wengine wanaiogopa serikali ya CCM, kwa kifupi sio watu wa kuwategemea. Kwani wewe hukumbuki wakati TIDO Mhando na Kikwete wameanzisha kipindi cha rais kuongea na wananchi live ? Tido alikuwa kama katoto ka DSJ kalikomaliza juzi certificate ya uandishi habari.
Wananchi sikilizeni BBC hawamwogopi mtu walee nimewapenda sana.
 
Dawa yake na sisi tuwe na TV, Redioa na magazeti yetu, tena ikiwezekana magazeti ya Kikanda. Kazi ya ukombozi ni kubwa eti, Je tupo tayari kubeba hizo gharama. CCM wanawajau watanzania wao linapofika suala la kutoa fedha wagumu kweli kwel,i ila kwenye harusi tuu.
 
Dawa yake na sisi tuwe na TV, Redioa na magazeti yetu, tena ikiwezekana magazeti ya Kikanda. Kazi ya ukombozi ni kubwa eti, Je tupo tayari kubeba hizo gharama. CCM wanawajau watanzania wao linapofika suala la kutoa fedha wagumu kweli kwel,i ila kwenye harusi tuu.

kaka nakuunga mkono, TBC ni wanafiki na kwa sababu wanasema , wanasupport vyama vyote wakati wanakipa ccm muda mwingi wa hewani
 
TBC huwa wananichosha na zile messages wanazozisoma!
Zile msg ni cooked kabisa, genuine ni chache sana, na zote wanazosoma siku hizi ni kuwambia CHADEMA waache kampeni za matusi...

Tido keshapoteza credibility yake...

Politics zimefika mahala pake, tutaona mengi zaidi ya haya...
 
Mnakumbuka yale mauaji ya kimbali ya Rwanda!
Vyombo vya habari vilikuwa mstari wa mbele kueneza chuki.
Ndio ninachokiona kwa vyombo vyetu vya habari.
wapo radhi wampambe mtu hata kama ni mchafu na ananuka. Ni nidhamu ya uoga na kujipendekeza.
 
Wikiendi hii wakati wa kampeini za Chadema TBC wenyewe walikata matangaza juu ya kwamba Marando alikua anaanza kutaja majina ya Mafisadi wa EPA kama Majira ilivyoripoti. Yani Tido hapa kachemsha kwa kweli. Maskini Marine akapewa kichapo.:playball:
 
Tatizo la Mlimani TV nadhani coverage yake ni ndogo but hawa wengine bora kuangalia DSTV 301 catoons tu!
 
Inashangaza kuona pesa zetu za kodi zinatumika katika kukipamba chama kimoja hasa CCM,ila mapinduzi ya kweli hayaji katika kutoka katika TV,s bali kwa kampeni za nyumba hadi nyumba mpaka kieleweke.
 
Back
Top Bottom