dolevaby
JF-Expert Member
- Aug 25, 2013
- 12,956
- 9,482
Asante ndugu kwa hili bandiko tatizo watanganyika tunakariri mamboLabour and professionalism ni commodity, bei yake hutegemea ubora wake na mahitaji ya soko. Watanzania wengi wanadhani mshahara huamuliwa na akili na kiwango cha elimu. Kitu ambacho ni kosa kubwa.
Mshahara huamuliwa na performance. Nini output yako. Unaweza kuwa na akili kama shetani, unaweza kuwa na PhD lakini mshahara wako ukazidiwa na mwenye diploma. Unapokuwa performer, unatafutwa, hutafuti kazi. Kwa sababu umetafutwa una-dictate terms. Kama hutaki terms zake unaachana nae, ataendelea na wengine.
Na nina hakika Msechu kutoka kwa mwajiri wake wa awali, na kwa kuijua serikali ilivyo kigeugeu atakuwa alijiwekea ulinzi wa kutosha wa kiajira. Na mkitaka kumtoa hapo, unaweza kulazimika kumlipa mshahara wake wa sasa kwa mwaka mzima au miaka miwili. Halafu unamlipa leo, kesho utamsikia ameajiriwa Ethiopia, Nigeria au SA. Kwa kuifanya NHC kuwa katika nafasi ya ubora katika Afrika, huyo mkurugenzi ni wa kutafutwa tu, hatalazimika kutafuta kazi. Ndivyo biashara za kisasa zinavyotaka.
Kuna wakati nilikuwa nalipwa mshahara wa $8,000, nilipofanikiwa kuongoza timu yangu na kupata mradi uliokuwa na thamani zaidi ya $4 billion, ndani ya wiki moja nilitafutwa na makampuni manne tofauti, kila mmoja na offer yake. Mimi niliweka terms za ajira, pamoja na mambo mengine, mshahara niliweka $16,000, mwajiri akaamua kunilipa $19,700. Tukazanie performane ili tuwe na nguvu katika kupanga mishahara.
Kwenye biashara za kisasa kinachoangaliwa unazalisha kiasi gani nawe unachukua kiasi gani. Mkurugenzi wa kwanza alikuwa anazalisha negative TZS 3 billion halafu analipwa TZS 5 million. Huyu alikuwa aghali zaidi kibiashara kuliko Msechu.