Tuache ung’ang’anizi................. ..!

Mtambuzi wengi huwa tunatamani haya uliyoyazungumza, lakini ukweli ni kuwa moyo uliopenda ni mgumu sana kubadili nia kirahisi. Nimeshuhudia watu wakinyanyasika na kuteseka kwenye mahusiano yao lakini bado wanang'ang'ana. Kwa kweli upendo ni kitu cha ajabu sana.

Ila kwa ushauri naungana na wewe kwa wale wenye ujasiri wa kuvunja mahusiano mara wanapotamkiwa kuwa hawapendwi tena ni bora kufanya hivyo ili kuepuka baaadaye kuja kufanyia vitendo vya kikatili ikiwemo kuchomana visu au kuunguzana moto au pengine hata kukatana mapanga kama tulivyoshuhudia kwenye baadhi ya mahusiano fulani fulani.
 
Last edited by a moderator:
wakati mwingine kukataliwa ni neema tu kwa sababu ungelijua Muumba anakuepusha na nini pengine ungelipiga vigelegele..................
 
Mtambuzi hapa hujanikamata.Mimi ni kinganganizi hasaa nilipata somo zuri kutoka kwa dada gfsonwin.
 
Ah mtambuzi...some times hiyo kitu ni so hard kukubaliana nayo...si unajua moyo wa kupenda hauambiliki jambo
 
Kuna wengine kila mara wanakula vichapo na kufungashiwa vifurushi lakini wanang'ang'ania tu......duh!! Yaani huwa nawaangalia mara mbili mbili nakosa jibu, ila nadhani na familia zetu zinachangia wajameni. Wanawake wengine wakiachika huwa wanarudishwa tena kwa waume zao!
 
Binafsi nakichukiaaaaaaa sana mtu king'aninizi au tendo la kung'ang'ania loooh! Na kama ndoa ili idumu ndo inabidi uwe king'aninizi basi mie hapo nimefeli,senkyuuu.

Kuna wakati mpenzi anaambiwa kabisa na mwenzake kwamba hatakiwi, lakini yeye anasema, "tutabanana humu humu hatoki mtu hapa." Bila shaka hiki ni kichaa cha aina fulani. Mtu akishasema sikutaki, maana yake hakuna tena kinachoweza kuwaunganisha, yaani hisia za upendo. Kulazimisha kuishi na mtu asiyekutaka ni kujifanya mtumwa bila sababu. Inabidi tuamke na kuwa sisi kamili kabisa.

I love youuuuuuuuuuuuuuuuu
 
Kuna wengine kila mara wanakula vichapo na kufungashiwa vifurushi lakini wanang'ang'ania tu......duh!! Yaani huwa nawaangalia mara mbili mbili nakosa jibu, ila nadhani na familia zetu zinachangia wajameni. Wanawake wengine wakiachika huwa wanarudishwa tena kwa waume zao!
Kipipi hao wanaorudishwa ni kweli wapo ila mimi nasema wanakua hawana msimamo........huwezi kunirudisha kwenye nyumba ambayo nimeshachungulia kaburi wallaih nakwambia,kama na undugu ufeee!!!!
 
Last edited by a moderator:
mkuu nimeshuhudia rafiki yangu niliyekuwa naishi naye wakati nasoma chuo kikuu mjini hapa amekuwa chizi kisa mwanaume kaishi naye 12yrs in a relationship yule mwanaume akadai kamchoka eti kazeeka akachukua kichuda akamwambia njoo geto kwake mabibo ile kafungua mlango kamkuta na mwanamke ,maskini yule dada mpaka leo chizi Mtambuzi wangu
 
Last edited by a moderator:
Ah mtambuzi...some times hiyo kitu ni so hard kukubaliana nayo...si unajua moyo wa kupenda hauambiliki jambo

Kama unampenda mwenzako utaheshimu hisia zake.Na namha ya kuonesha heshima na upendo huo ni kuondoka kama anavyotaka!
 
Back
Top Bottom