Tuache/Tupunguze kuchangia harusi............

BIG X

JF-Expert Member
Nov 4, 2011
777
212
Tuchangie Elimu sasa.

Kuna sababu gani ya kuchangia mamilioni ya hela kwa harusi inayofanyika kwa masaa manne tu!!. Na ndoa zingine hazimalizi hata mwaka zimeshavunjika!!. Tubadilike jamani tunapokwenda kila mtu anajua umuhimu wa Elimu, Kila mtu atahitaji mtoto wake asome mpaka level ya university, kwahiyo kwa namna yoyote ile serikali haitaweza kusomesha watoto wote kwa asilimia 100. Lazima tutahitaji kuwasaidia vijana wetu wapete Elimu na kuweza kujitegemea vizuri.

Tukiwa bado tuna uwezo leo wa kutafuta pesa, tuwafikirie vijana wetu baada ya miaka 6 mpaka 10 watakuwa wapi. Badala ya kuchangia maharusi hela nyingi, watu wengine watachangia malaki/mamilioni. bora hizo hela tuchangie kwenye Elimu ya vijana wetu. Sisemi basi tuache kabisa kuchangia harusi basi hata tupunguze, mi nina uhakika elfu 25-30 kwa kwa mtu mmoja kuchangia inatosha sana, sasa itategemeana utachangia harusi ngapi kwa muda gani. Lakini mtu uwe na kikomo, Angalau mtu ujue unachangia kiasi gani kila mwezi kwa watoto wako kama huwezo kwa jamii huna.

Wazazi tukumbuke Leo tupo, Lakini kesho tunaweza tusiwepo. Tunaowachangia mahela kibao leo kwenye harusi hawatakumbuka/kuja kuwasaidia watoto ambao utakuwa umewaacha. Watoto watapata shida na kulaani jinsi wazazi mlivyowatelekeza.

Naongea haya kwa sababu kuna familia ambayo leo inapata shida, watoto hawezi kwenda shule sababu hakuna pesa. kwa bahati mbaya baba yao alifariki kwa ajali ya gari akiwa bado kijana, Huyo baba alikuwa mtu mkubwa kwenye taasisi fulani maarufu na alikuwa na uwezo sana, lakini sifa yake kubwa ilikuwa kuchangia hela nyingi maharusi na masherehe makubwamakubwa. Leo watoto wake wanapata shida baada ya yeye kufariki.
 
Back
Top Bottom