Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,466
- 113,543
Wanabodi,
Tuliwahi kusema humu, Tanzania inachohitaji sio a one man show, bali tunahitaji mifumo imara na thabiti, yaani an effective system. Ukiishakuwa na mfumo imara, na thabiti, kila kitu kinachofanyika kwenye taasisi, kinafanyika ndani ya mfumo thabiti, kinakuwa automated, na very transparent, chochote kitakachofanyika out of system kinakuwa detected automatically na kuwa ejected out of system, hivyo hakutakuwa hata na haja ya kutumbua tumbua, once the system is there, anyone who goes against it, anakuwa ejected out of system automatically hivyo anajitumbua mwenyewe kwa ku fall out of system.
Mimi sio mchumi ila humu jf tuna wachumi lukuki, hivyo naomba ndugu zetu wachumi wa humu, jitokezeni mtusaidieni kutuelimisha kuhusu haya mambo ya fedha, na kutuelimisha kuna dhambi gani kufungua FDA ili fedha kiduchu taasisi inazopewa zihifadhiwe huku zinazaliana angalau kukidhi mahitaji ukilinganisha na kuzihifadhi tuu fedha hizo kule BOT ambako hazizalishi hata sentí moja?!.
Mwezi Julai nilifanya mahojiano na CAG Prof.Musa Assad kuhusu kupigwa panga kwa budget ya CAG. Kumbe sio ofisi ya CAG pekee iliyopigwa panga, bali wizara zote na idara zote pia zimepigwa panga na kupewa only 40% ya mahitaji yake ya kibajeti.
Sasa kama TRA imepewa hicho kidogo kisichotosheleza mahitaji, menejmenti ikajenga hoja za msing kwenye bodi wafungue FDA ili hicho kidogo walichopewa ambacho hakikidhi mahitaji, angalau kiongezeke kupunguza nakisi, kwa maoni yangu, hili ni jambo jema na kama linafanyika kwa nía njema na kwa uwazi, kuna ubaya gani?.
Hivi ni kweli hizi FDA za taasisi za umma ikiwemo TRA, zimefunguliwa ili bodi na menejmenti wazipige hizo interest?!. Yaani bodi zenye watu wenye weledi walioteuliwa na rais na waziri husika, tena kukiwemo mwakilishi kutoka kule kwa wale 'jamaa zetu', halafu wote wacollude na menejimenti ya taasisi zao, kufungua FDA, ili waziibe hizo interest?!, japo kuna watu wanaamini everthing is possible in Tanzania!, mimi siamini hili linawezekana!, kwa sababu hata ikitokea kuwa ni kweli, wengine wote wanaweza kuwa ni majizi!, lakini hata wale 'jamaa zetu' wale?!, kama hili ni kwel na limekuwa likitendeka, then, Tanzania tuna tatizo kubwa zaidi kuliko tunavyojidhania, yaani tutakuwa tuna a rotten system!, yaani mfumo uliooza kabisa na unanuka!. Ndio maana nasisitiza Tanzania we need an effective systems zenye maximum transparency na sio hizi one man show zinazoendelea sasa.
Kwa vile Mkuu sio mchumi, ila amezungukwa na wasaidizi ambao ni wachumi waliobobea wanaojua uchumi kinyumenyume, ambao wanajua kama ni kweli rais ametoa amri fedha zote kabisa za umma na taasisi zote za umma zitumie BOT pekee kwa shughuli zake zote za fedha, then wanajua wazi kwamba he is not doing the right thing na wameamua kulinyamazia hili na kukaa kimya bila kumweleza mkuu kuwa hili haliwekan, ba badala yake wakimwacha tuu afanye anavyotaka kwa kumuogopa tuu, wajue ni wao ndio watakaohukumiwa kwa sababu wao ndio wanaojua na huyo mtendaji yeye hatahukumiwa, kwa sababu hajui atendalo!.
Nasisitiza Mkuu hatahukumiwa kwa sababu kila analoliwaza, analolisema na analolitenda, anayafanya yote hayo kwa nía njema na dhamira safi, lakini kumbe masikini wa watu, hata hajui atendalo kwenye uchumi wa nchi hii kwa sababu hajaambiwa, hivyo yeye hana kosa.
Sekta binafsi yenye nguvu ndio injini ya uchumi wowote imara wa taifa lolote, sekta binafsi nchini iko kwenye hati hati ya ku collapse kutoka na kupungua kwa mzunguko wa fedha, huku sote tukiitwa ni wapiga dili!. Hivi kweli kila mwenye kilio cha hali ngumu ya uchumi ni mpiga dili?!.
Kama issue ni mabenki binafsi kutengeneza faida kwa amana ya fedha za umma, then BOT wafungue kitengo cha BOT Commercial Bank, na wawe na matawi nchini nzima ili hizo pesa za taasisi za umma zinazokula kiyoyozi tuu kwenye strong rooms za BOT, ili zisiote uvundo, zifunguliwe FDA huko huko BOT, ili zizalishe interest, na sisi sekta binafsi pia turuhusiwe twende tukakope BOT turudishe fedha kwenye mzunguko.
Vinginevyo hata hii Tanzania ya viwanda inayohubiriwa sasa ni hadithi tuu, hata serikali ikitegemea capital injection ya uchumi wa viwanda itoke kwenye FDI (Foreign Direct Investment), bila a strong private sector, bila DDI (Domestic Direct Investment), kwenye hiyo Tanzania ya viwanda Watanzania watakuwa ni watazamaji tuu hiyo Tanzania ya viwanda badala ya kuwa ni washirika, ila hata hiyo raw materials ya kushibisha uchumi wa viwanda itatoka wapi?.
Wachumi jitokezeni mtuelimishe maana sisi wengine sio Wachumi maana naona kwa Tanzania kila kitu ni siasa, siasa ni siasa, jamii ni siasa hata uchumi sasa ni siasa! . Tuachage siasa kwenye mambo mengine jameni sisi huku mitaani tunaumia, tunapigika kweli kweli!.
Paskali.
Update.
Kwanza asanteni wachumi wa jf mliojitokeza kwenye uzi huu, ila Msajili wa Hazima, ameifunga rasmi mjadala huu kwa kauli hii.
Aliyoyasema msajili
1. Sii kweli rais amezuia taasisi za umma kutumia benki za biashara, bali makusanyo yote ya umma, government revenue, ndio sasa yatatunzwa BOT.
2. Tasisi zote zitaendelea kutumia mabenki kwenye operesheni zake.
3. Hakuna ubaa wowote kufungua FDA.
4. Kama ni kweli kulikuwa na wizi kwenye FDA, CAG ameagizwa kufanya ukaguzi maalum, hili likibainika, sheria itaachiwa kuchukua mkondo wake.
Asanteni.
Paskali