Tuache Desturi na Mila mbaya za wazee wetu!

Topical

JF-Expert Member
Dec 3, 2010
5,174
935
Kuna makabila mengi Tanzania bado wana mila na desturi mbaya; na kuna watu bado hawataki kuacha destruri na mila hizo. Napenda kuwafahamisha kuwa si lazima kuwafuata wazee wako walikuwa wanaamini nini? au wanafanya nini fanya utafiti mwenyewe tafuta ukweli kabla ya kifo; maana kila mtu atabeba mzigo wake ahera..

1. Chunguza kama dini za wazee wako ni sahihi i.e. usikubali kuabudu mizimu, sanamu wala usimshirikishe Mwenyezi na kitu chochote. Si lazima kufuata dini za wazee kama wanaabudu mizimu, sanamu maana utaulizwa mwenyewe tu wala kufuata baba yako haitakuwa sababu ya kutosha siku hiyo..

2. Usikubali kuonea wanawake na watoto; kuna makabila watoto wa kike hadi leo wanaonewa, na wanawake hawapewi stahili zao; hakuna mgawanyo wa mali; nimekutana na kesi moja huku Dodoma wanaume tu ndio wanaridhi maliya baba kama ng'ombe na ardhi lakini wasichana hawapati chochote.

3. Mnaweza kuongeza mila na desturi mbovu......mnazojua???
 
Kuna makabila mengi Tanzania bado wana mila na desturi mbaya; na kuna watu bado hawataki kuacha destruri na mila hizo. Napenda kuwafahamisha kuwa si lazima kuwafuata wazee wako walikuwa wanaamini nini? au wanafanya nini fanya utafiti mwenyewe tafuta ukweli kabla ya kifo; maana kila mtu atabeba mzigo wake ahera..

1. Chunguza kama dini za wazee wako ni sahihi i.e. usikubali kuabudu mizimu, sanamu wala usimshirikishe Mwenyezi na kitu chochote. Si lazima kufuata dini za wazee kama wanaabudu mizimu, sanamu maana utaulizwa mwenyewe tu wala kufuata baba yako haitakuwa sababu ya kutosha siku hiyo..

Siku ipi?
Yaani unatuambiwa tujiulize kuhusu mila za mababu zetu lakini hapo hapo ushatupa jibu kuwa tufate unachotaka wewe!

*ni mirathi sio miradhi
(kwa Waswahili miradhi hutumika kumaanisha maradhi ya kila aina wakati)
 
2. Kuhakikisha hiyo haitokei inabidi na dini fulani nayo iangaliwe maana inakandamiza sana wanawake na sehemu ya watoto.
 
2. Kuhakikisha hiyo haitokei inabidi na baadhi ya dini nayo iangaliwe maana inakandamiza sana wanawake na sehemu ya watoto.

Unaweza kutusaidia kutujuza hizo baadhi ya dini na namna zinavyokandamiza sana wanawake na watoto?
 
2. Usikubali kuonea wanawake; kuna makabila watoto wa kike hadi leo wanaonewa, na wanawake hawapewi stahili zao; hakuna mgawanyo wa mali; nimekutana na kesi moja huku Dodoma wanaume tu ndio wanaridhi maliya baba kama ng'ombe na ardhi lakini wasichana hawapati chochote.
Nafasi ya mwanamke iko palepale tu,kamwe hawezi kuwa sawa na mwanaume hata ufanyaje,wazee walikuwa sahihi ila kwa kuwa siku hizi mnaleta uma-gharibi ndo maana mambo yanaonekana tofauti,wazee walikuwa makini sana na busara nyingi kuliko watu wa sasa.Unyanyapaa wa wanawake ulianza tangu zamaniiiiiiiii na hata utake kuuondoa huwezi coz ndo imeumbwa iwe hivyo.
Halafu mwanamke ukimpa nafasi ana manyanyaso sana,hivi si ushasikia kuwa hata wao wanashauri USIOE MWANAMKE ALIYEKUZIDI KIPATO AU ELIMU??? Hujiulizi kwanini??? then pata picha wanawake wote wawe na elimu na pesa dunia itakuwaje?
Wacha ile kwao hivihivi.
 
Imeumbwa iwe hivyo na nani?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom