PayGod
JF-Expert Member
- Mar 4, 2008
- 1,259
- 57
TTCL yaomba bil.70/- kujiimarisha
CHAMA cha Wafanyakazi wa Sekta ya Huduma za Mawasiliano nchini (TEWUTA) kupitia Shirika la Simu (TTCL), kimeitaka serikali kulikopesha sh bilioni 70 kwa ajili ya kufufua utendaji wa shirika hilo la kizalendo.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Katibu Mkuu wa Tewuta Junus Ndaro alisema kupatikana kwa kiasi hicho cha fedha kutakuwa suluhu ya TTCL kuanzisha miradi mbalimbali na kutoa huduma bora ya mawasiliano katika soko la ushindani wa makampuni mengi ya simu kutoka nje.
Alisema kukwama kwa shirika hilo kumetokana na hujuma iliyofanywa na makampuni ya kigeni dhidi ya TTCL ambayo yaliingia ubia kupitia wafanyakazi wasio wazalendo.
Ndaro alisema fedha hizo zitaendesha miradi ya kampuni hiyo nchi nzima kwa na kufanikisha uwepo wa mawsiliano nafuu na wananchi kuendelea kunufaika na huduma kutoka kwa wazalendo.
Alisema TTCL mwaka 2001 ilikuwa na sh bilioni 250 benki lakini baada ya utitiri wa makampuni ya simu ambayo hayana uwezo kuingia ubia na shirika hilo kulisababisha kutafunwa kwa fedha hizo na kuliacha shirika kuwa ombaomba.
"Tunaiomba dhamana serikali kuweza kukopa sh bilioni 70 kwa kuanzia ili kuweza kulisimamisha shirika letu kiutendaji zaidi kwa kutoa huduma bora kwa bei nafuu" alisema wakili huyo.
Alisema shirika hilo linashindwa kuendelea kutokana na wadeni wao kushindwa kulipa ikiwemo serikali ambayo inadaiwa sh bilioni tisa hivyo.
Ndaro alisema serikali inayo haja ya kuipa dhamana TTCL kuliko kuendelea kuilipa Dowans mabilioni ya fedha ambazo haziwezi kimsingi ni kumkandamiza mwananchi wa kipato cha chini.
"Ifike mahala Watanzania kuwa na uchungu wa kuendeleza shirika lao kuliko kuendelea kuwa na makampuni ya kigeni na kinyonyaji kwa walipakodi wa nchi hii" alisema Ndaro
Imefika wakati sasa TTCL , kufanya biashara kwa umakini, kwa mfano kama wakiamua kuwekeza kwenye internet service kiumakini zaidi watapata faida kubwa coz, wanamtandao mkubwa kuliko hata kampuni nyingine za simu.