Naona umetoa shutuma kali kweli. Mimi pia mteja wa Broadband ya TTCL. Binafsi nadhani hao TTCL ni much better kuliko wengine.
Speed ya internet imeongezeka, hasa nime-notice video streaming (hapa inategemea RAM pia).
Juu ya servers zao kuwa down, ni kweli. Nimeona mara mbili tatu hivi. Lakini si kiasi cha kukatisha tamaa. Suala kwamba hawapokeai simu sina hakika nalo kwani ukipiga 100, unaunganishwa baada ya muda(kama line iko wazi).
Kuhusu bei, ni kweli bado ziko juu. Mimi napata 1G kwa kulipia elfu 60 kwa mwezi. Ni ghali mno. Lakini niliongea nao, pale ofisi ndogo iliyoko Ubungo Plaza, wakaniambia mwezi wa 10 watashusha bei.
NB: Habari za uhakika ni kwamba serikali isipotoa sh bilioni 18 mapema iwezekanavyo, kampuni hii inakufa na kuzikwa.
Swali kubwa ambolo najiuliza hii TCRA kama regulator anafanya nini kulinda maslahi ya wateja waoibwa na makampuni haya kwa kulipia gharama kubwa ya bandwidth na mteja anachopata si sawa na amount ya bandwidth aliyonunua
Hamia Zantel 3G,au unaonaje?