TTCL na huduma ya internet

Mkuu Fungwe,

Asante kwa ushauri ingawaje umesema hiyo sera ya TTCL (OF COURSE SIO) lakini pamoja na hiyo isolated case yangu kama mnavyosema, inakuwaje hawana moden mpaka wateja tununue wenyewe? Suala hapa kwa mtindo huu hawa jamaa wamejiandaa kushindana kweli kwenye ili soko huria? Nakumbuka wakati naomba nifungiwe line ya simu some 10 years ago, it did not take that much long pamoja na kwamba they were only service provider available. Iweje leo wakati watoa huduma za internet wako kibao?

Tiba

Achana nao, sio lazima uwe na Internent ya TTCL kama mwanzo ndio huo kuna uwezekano wa kupata usumbufu zaidi hapo baadae! Tumia Zantel au Sasatel.
 
Asante mkuu kwa ushauri. Tatizo tayari nimelipia connection fee, nimenunua modem na tayari nimelipia hiyo huduma kwa mwezi mzima Tshs. 60,000 sasa nikiachananao si itakuwa imekula kwangu? Najua itakuwa taabu kuwaambia warudishe pesa zangu ili niende kwa service provder mwingine. Nafikiri wananifanyia hivyo kwa kuwa tayari wana pesa yangu, lakini je kwenye biashara ya ushindani approach hii inafaa? Wataweza kudumu kwenye ushindani?

Tiba
 
mie ya kwangu net iko poa ila simu haifanyi kazi mwaka na nusu sasa nisharipoti weeee mpaka nimechoka juzi nimeenda mwenyewe pale plaza na wakampigia simu fundi mbele yangu na wakampa na namba zangu kama atapotea, hivi ninavyo sema nina wiki naendelea kumvumilia labda ana kazi nyingi sana
 
BOL haifanyi kazi vizuri hapa nilipo/nilipohamia kama ilivyokuwa kule nilipokuwa naishi zamani na wanasema hakuna coverage hivyo hakuna jinsi. Sasa nataka kuhama mtandao, nihamie wapi? Sitaki kurudi TTCL maana waliniboa sana na yale masimu ya HUAWEI, yalikuwa slow sana! Huwa siamini vipya vinyemi hivyo naogopa kwenda SASATEL! Sasa, je, nichague ipi kati ya hizi:

SIMBANET

AFRICAONLINE

IWAY

ZANTEL

VODACOM

?
 
mie ya kwangu net iko poa ila simu haifanyi kazi mwaka na nusu sasa nisharipoti weeee mpaka nimechoka juzi nimeenda mwenyewe pale plaza na wakampigia simu fundi mbele yangu na wakampa na namba zangu kama atapotea, hivi ninavyo sema nina wiki naendelea kumvumilia labda ana kazi nyingi sana

Mkuu Waukae,

Sasa kama tatizo ni fundi si waongeze mwingine au watafute kwenye customer service centre nyingine kwa muda ili kukabiliana na matakwa ya wateja? Ningesikiliza ushauri wa rafiki yangu, nisingekuwa hapa nalalamika. Hivi landline kama haifanyi kazi bado internet inakuwa inafanya kazi?

Tiba
 
Pole, That is one isolated case, TTCL broadband is the fastest, cheapest na most reliable!. 40,000/= per month, you enjoy unlimited wireless 24/7.

Pasco, we mwenzetu unalipia wapi hizo 40,000/= per month unlimited TTCL wireless? Mimi natumia hiyo hiyo lakini nalipa 45,ooo/ per month na siku nyingine nalazimika kulipa 50,000/= kwa sababu hawana voucher za 5,000/=!!
 
Mkuu pole, hujafa hujaumbika. kwani wewe ni mgeni na utaratibu wetu ukitaka huduma ? hasa kwenye mashirika yetu haya? hebu tafakari kuna mahali UNAKOSEA.

kweli mkono mtupu aulambwi ndipo anapokosea tu
 
Naleta mbele yenu kisa hiki ambacho kimenipata mimi mwenyewe. Ukipita mitaa mingi ya Dar Es Salaam kuna mabango kila mahali yanayoonyesha kwamba TTCL wanatoa huduma ya internet. Pamoja na kwamba kuna makampuni mengi sasa hivi yanatoa huduma hii, mimi nilishawishika kuwajaribu TTCL kwa maana nzima ya kulipiga tafu shirika letu la umma pamoja na kuonywa na rafiki yangu mmoja kwamba TTCL ni wasumbufu na kwamba itanichukua muda mrefu kupata huduma hiyo. Lakini kinachoendelea kwa sasa huwezi kuamini kwamba ndio watu wale wale walitumia mamilioni ya shillingi kuweka matangazo kwamba wanatoa huduma hii. Tarehe 21 December 2009 nilikwenda pale TTCL Ubungo plaza na kuulizia uwezekano wa kuunganishiwa internet nyumbani kwangu. Nilipewa fomu nikajaza na kuonyesha nitachukua package ipi kati ya zilizokuwepo baada ya kupewa maelezo na kushauriwa nitumie landline ili niweze kupata huduma nzuri zaidi. Niliwafahamisha kuwa ninayo landline nyumbani kwangu na hivyo nikaambiwa atatumwa fundi kuja kuangalia eneo. Ni kweli fundi alikuja na baadae walinitaka nikalipie. Nililipia connection fee ya Tshs. 25,000 na baada ya hapo ikawa kimya. Baada ya kuwafuatilia nikataarifiwa kuwa siwezi kupewa huduma hiyo kwa sasa kwa kuwa wameishiwa modem. Nikaulizia uwezekano wa kununua modem yangu mwenyewe wakasema sawa ninunue halafu niwataarifu waje kufunga. Pamoja na kulipia hiyo gharama ya internet ya mwezi mmoja tarehe 21 January 2010, mpaka leo fundi hajaja kuniunganishia hiyo huduma. Ukienda pale ofisini kwao wanakwambia fundi alikuja hakukuta mtu nyumbani, ukimpigia fundi simu kuuliza anadai alikuwa busy sana bado hajaja!!! (Contradiction)

Swali langu ni je hali hii imeishamkuta mtu mwingine au imetokea kwa bahati mbaya kwangu tu? Je hawa jama zetu kwa mtindo huu ni kweli wamejiandaa kufanya biashara kwa ushindani? Je wakubwa huko makao makuu wanajua madudu yanayofanywa na watendaji wao hawa?

Natabiri kufa na kuzikwa kwa TTCL muda si mrefu endapo hali hii haikutokea kwa bahati mbaya tu.

Tiba

PIGA # 100 katika cmu yako landline omba watu wa broadband, utahudumiwa, wanajitahidi kwa kweli!!!!!!!!!!1111
 
Nilikua mteja wa Sasatel nikaachananao bada ya kuhesabu MB nikaona zinakwend aupesi hata kama nimefungua webpage isiyo na picha wala video. nimeamua kuachana nao.

Swali langu, mimi natumia sana Net kucheki shows kweney Youtube, sija jua ni mtandao gani utakau kidogo afadhali maana hizo 1GB ni najidanganya , je Africa online wao wako vipi?,Thanx

kwa ushauri wangu nakushauri uchukue zantel evdo modem 226 zipo fasta zaidi ya ttcl nimejaribu hilo na wanapakeji nzuri
 
Naleta mbele yenu kisa hiki ambacho kimenipata mimi mwenyewe. Ukipita mitaa mingi ya Dar Es Salaam kuna mabango kila mahali yanayoonyesha kwamba TTCL wanatoa huduma ya internet. Pamoja na kwamba kuna makampuni mengi sasa hivi yanatoa huduma hii, mimi nilishawishika kuwajaribu TTCL kwa maana nzima ya kulipiga tafu shirika letu la umma pamoja na kuonywa na rafiki yangu mmoja kwamba TTCL ni wasumbufu na kwamba itanichukua muda mrefu kupata huduma hiyo. Lakini kinachoendelea kwa sasa huwezi kuamini kwamba ndio watu wale wale walitumia mamilioni ya shillingi kuweka matangazo kwamba wanatoa huduma hii. Tarehe 21 December 2009 nilikwenda pale TTCL Ubungo plaza na kuulizia uwezekano wa kuunganishiwa internet nyumbani kwangu. Nilipewa fomu nikajaza na kuonyesha nitachukua package ipi kati ya zilizokuwepo baada ya kupewa maelezo na kushauriwa nitumie landline ili niweze kupata huduma nzuri zaidi. Niliwafahamisha kuwa ninayo landline nyumbani kwangu na hivyo nikaambiwa atatumwa fundi kuja kuangalia eneo. Ni kweli fundi alikuja na baadae walinitaka nikalipie. Nililipia connection fee ya Tshs. 25,000 na baada ya hapo ikawa kimya. Baada ya kuwafuatilia nikataarifiwa kuwa siwezi kupewa huduma hiyo kwa sasa kwa kuwa wameishiwa modem. Nikaulizia uwezekano wa kununua modem yangu mwenyewe wakasema sawa ninunue halafu niwataarifu waje kufunga. Pamoja na kulipia hiyo gharama ya internet ya mwezi mmoja tarehe 21 January 2010, mpaka leo fundi hajaja kuniunganishia hiyo huduma. Ukienda pale ofisini kwao wanakwambia fundi alikuja hakukuta mtu nyumbani, ukimpigia fundi simu kuuliza anadai alikuwa busy sana bado hajaja!!! (Contradiction)

Swali langu ni je hali hii imeishamkuta mtu mwingine au imetokea kwa bahati mbaya kwangu tu? Je hawa jama zetu kwa mtindo huu ni kweli wamejiandaa kufanya biashara kwa ushindani? Je wakubwa huko makao makuu wanajua madudu yanayofanywa na watendaji wao hawa?

Natabiri kufa na kuzikwa kwa TTCL muda si mrefu endapo hali hii haikutokea kwa bahati mbaya tu.

Tiba

ndo kawaida yao ni wazembe ninachoshangaa kwann wanapoteza pesa nyingi kutanga
 
PIGA # 100 katika cmu yako landline omba watu wa broadband, utahudumiwa, wanajitahidi kwa kweli!!!!!!!!!!1111

Wakuu,

Kumbe JF inasadia mambo mengi sana. Kupiga kelele tu jana sasa hivi nimepigiwa simu mafundi wako nyumbani kwangu wanachakarika kufunga hiyo internet. Nawashukuru wote walionipa mchango wa mawazo. Nitawafahamisha performance yake ikoje nikishaanza kutumia.

:smile-big: happy for u bro !
Sasa, vipi ? ina fanya kazi vizuri ?
mi natafuta kununuwa internet, lakini sijue kama ttcl ipo UNLIMITED ? na shs ngapi ?
plz can u advise ?
 
Duh! mzee, hii post ya February umeifufua! we mkali
 
Back
Top Bottom