TSN yapata hasara bilioni 19

...kama magezeti ndo haya Daily News na
HabariLEO,TSN wasitarajie kupata faida hata siku moja,sidhani kama bado kuna mtanzania makini anaweza kupoteza pesa yake kununu hivyo vipeperushi vya propaganda za magamba...

Hiyo kamati naishauri izungukie pia TBC 1 & 2,unaweza kuta nako kunamiss 19b zingine
 
Sikumuelewa Mh Zito pale. Amesema hawajapitia hesabu, then anasema wamegundua hasara. Anasema ni hasara, lakini hawajaiba ila imetokana na makosa ya kihasibu. Bado naona kuna kitu nyuma ya pazia isijekuwa ni kisiasa zaidi na kulipa kisasi cha mwaka 2010.
 
Ningeshangaa sana kama kingesikia wana faida, sawa na Gaeti la Uhuru ambalo nadhani sasa hivi ni kama free copy complimentary ya maofisini nalo ushangae kupata hasara!!
 
Hiyo kamati naishauri izungukie pia TBC 1 & 2,unaweza kuta nako kunamiss 19b zingine

...mkuu mbona hiyo TBCCM ilisha-kufa siku nyiiingi baada ya kuondoka Tido,unacho kiona hapo ni limsukule la stesheni ya tv...
 
Hawa ndio wenye TSN supermarket na petroleum stations

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

Sio hiyo we mtu!!! Umechambua kikawaida sana! Ni Tanzania Standard Newspaper mazee!

Haina uhusiano na Acronym TSN ya fuel stations and Supermarket babu!
Kabsa!
 
Gazeti la Taifa linalotumika kufungia maandazi, Ambalo wasomi wameacha kulinunua
 
Gazeti la Taifa linalotumika kufungia maandazi, Ambalo wasomi wameacha kulinunua

Hayo ni mawazo yako. Hadi tunapozungumza Daily News ndilo linaloongoza kwa mauzo nchini upande wa magazeti ya kiingereza.
Na wasomi unaowasema hawaamini jambo lolote hadi liwe limechapishwa DN.
Ila kwa upande mwingine Habari Leo kweli haliuziki na halina mvuto kabisa.
 
Yaani ni kula tu.... no one anaguswa.... haaaa raha kweli Tz....tshs 19 billions ka mchezo tu... Na wanajibu kirahisiiii .... HASARA......
 
Katika taarifa ya habari leo saa mbili usiku STAR TV wametangaza kuwa kampuni ya magazeti ya serikali TSN inayochapisha Daily News na HabariLEO imepata hasa ya shilingi bilioni 19 na hayo yamegundulika wakati wa kikao cha kamati ya Bunge ya POAC chini ya Uenyekiti wa Zitto Kabwe na kikao kimevunjika.

Zitto ameeleza kuwa watendaji wa TSN na wajumbe wa Bodi wote wameitwa Dodoma kujieleza

My Take:
Hasara bilioni 19 inashangaza sana; Mkumbwa Ally na wenzake wamekula na kusaza!

Nani anasoma ***** wao?
 
Nilitarajia wapate hasara kubwa zaidi kuliko hiyo iliyotangazwa kwani habari wanazochapisha huwa hazina tija kabisa kwa jamii na nchi yetu kwa ujumla. Magazeti yanayoendeshwa na kugharamiwa kwa kodi za wananchi yamegeuzwa magazeti ya ccm ulitegemea ni nani katika zama hizi atanunua magazeti yasiyojali maadili ya uandishi yanayojaribu kwa nguvu zote kuugeuza ukweli kuwa uongo na uongo kuwa ukweli? Rest In Peace HABARI LEO na DAILY NEWS kwani hayana tija.
 
kwa hayo mashirika, hasara wakati mwingine inasabishwa na maamuzi ya serikari kuu, mfano inawezeka hasara hiyo inatokana na jengoo pale makataba squre, hujui hizo transaction zinakwenda vipi?

Katika taarifa ya habari leo saa mbili usiku STAR TV wametangaza kuwa kampuni ya magazeti ya serikali TSN inayochapisha Daily News na HabariLEO imepata hasa ya shilingi bilioni 19 na hayo yamegundulika wakati wa kikao cha kamati ya Bunge ya POAC chini ya Uenyekiti wa Zitto Kabwe na kikao kimevunjika.

Zitto ameeleza kuwa watendaji wa TSN na wajumbe wa Bodi wote wameitwa Dodoma kujieleza

My Take:
Hasara bilioni 19 inashangaza sana; Mkumbwa Ally na wenzake wamekula na kusaza!
 
OMG Na hizi nazo ni hela zangu!

Katika matumizi ya mshahara wangu ambayo inaniuma kuliko kula matapishi ni kulipa kodi halafu kodi hiyo inatumika kukutukana {kupitia makala zinazochukiza zinazochapishwa na magazeti ya serikali...sehemu ya kodi yangu}
 
Ijulikane ninkampuni ya CCM na wala sio Serikali maana matendo na habari zao zimekaa kichama kama TBC no wonder wanakula hasara maana mteja kwao ni **** sio Mfalme
 
Back
Top Bottom