tshirts inayoongoza kwa mauzo dar na arusha

Mbona sielewi elewi??? yaani mtu unafurahia kuvaa Tshirt inayokunadi kwamba wewe ni dhaifu???
 
duh, halafu ina my favorate colors...nimeipenda sana...iko duka gani hii mkuu?
attachment.php
 
hahaha, mbona haya maajabu sasa? jamaa mtamchanganya hata miaka hii miliwili sijui mitatu atashindwa kuimaliza...mwacheni basi atulie atufanyie maendeleo hata kidogo kuliko kuyakosa kabisa.
 
IRINGA,MBEYA NA NCHI NZIMA INASUBIRIWA KWA HAMU SAAANA TU...! hmm

Nileteeni Mwanza nisambaza kanda yote ya ZIWA. Tuko tayari kuongeza gharama za usafirishaji hata kama laki tutanunua tu, acha tule mchicha kwa mwezi mzima kuliko kikosa ukumbusho huu. Nitahamasisha watu waiweke kwenye frem idumu centuries!!
 
watamkamatisha na bangi, we subiri...sasaivi polisi watachuukua bange zile wanazovuta watamkamata na kumwekea mfukono halafu watasema wamemkamata na bange....watamwandikisha maelezo ya onyo kinguvu na atapelekwa court.....chezea sisiemu wewe,....haiko ijua ehee
 
Nipo safarini naaelekea A-Town, nikifika nitakubeep unielekeze mtaa wenyewe, nataka mbili za kutokea na First Lady wangu. Nimependa jina la DHAIFU COLLECTION, size XL bana.
 
In a serious note,

Zikitoka tichirt zilizoandikwa ccm dhaifu nitainunua kwa gharama yoyote walau mimi na nyumba yangu tuwaonyeshe kuwa hatuwataki madarakani kwa kuwa ni wadhaifu wameshindwa kutuletea maisha bora kama walivyoahidi zaidi ya kutuibia mali zetu na kujilimbikizia huko marekani anakoenda kila siku.

Thirt hiyo msisahau kuweka mmea wa alama ya ccm ya bangi ina rangi gani????????

Dhaifuuuuuuuu
 
Mkuu wewe umepata? Mimi nimeenda asubuhi, wakasema hawauzi na iko kama nilikuwa nauliza kitu kigeni sana maskioni mwao...
 
hahaha, mbona haya maajabu sasa? jamaa mtamchanganya hata miaka hii miliwili sijui mitatu atashindwa kuimaliza...mwacheni basi atulie atufanyie maendeleo hata kidogo kuliko kuyakosa kabisa.

Haya maendeleo unayozungumzia ni yapi? Shule za kata? Vibarabara visivyo na viwango? Mahospital bila dawa, madaktari au vifaa? Wizi wa maliasili zinazozolewa na malori kila upande wa nchi na udongo wake? Jamani mimi ninashindwa kabisa rais wa Tanzania na uongozi mzima wanafanya nini hadi tuwe maskini kiasi hiki. Maendeleo ya polisi wanaookota rushwa waziwazi kila kona ya nchi badala ya kulinda sheria, raia,au mali zao? Mimi sioni maendeleo yeyote toka kwa hawa viongozi wetu. Wamezoea kutukimbia na kukimbilia India kutibiwa. Hao wahindi wapokuwa wanasomesha madaktari wake Tanzania ilikuwa wapi? Ninawakumbusha kuwa uharibifu wa mazingira ya taifa zima yanatuumiza wote. Hayo mifisadi yanachokisahau ni kuwa yanavuta hewa ile ile tunayovuta sisi maskini, tofauti tu ni kuwa wana pa kukimbilia kupata matibabu kwa kutumia kodi zetu. Naridia, hakuna maendeleo yeyote yaliyoletwa na rais huyu ila maangamizi kama tunavyojionea yakifanyika bila aibu yeyote ile.
 
Back
Top Bottom