Tsh. 1.4 billion spent on rehabilitating the Mtwara RC’s

Hizo zinaenda mtwara na Kurudi Dar es Salaam wizarani ujenzi nyingine zitakuwa zilisaidia ubunge wa Hawa Ghasia na Uraisi wa KIkwete hawa ni michwaa wanapekenya mpaka ndani ya mninga tukiwaacha bila kuwapiga risasi vizazi vijavyo hawatapata kitu CCM na serikali yake ovyo kabisa
 
Mkuu hayo ni yale ambayo tumeweza kuyasikia na kuyasoma Ni mangapi ambayo yako chini ya carpet hatuyasikii Mikataba mingapi ambayo imesainiwa na watu wamekula ten percent zao bila hata kujua Shangaa IPTL kuna mtu analipwa bilions of money na serikali kwa ajili ya kununua mafuta ya mitambo na hapo hapo IPTL inaiuzia Serikali hiyo hiyo iliyotoa pesa za kununulia mafuta umeme kama sio usaniii ni kitu gani Yaani UTU na UBINADAMu haupo na watu wanajijali zaidi wao na familia zao

Hawa jamaa hawana UTU wala UBINADAMU kwahiyo kwavile hawana utu wanaweza kuishi huko kwa Cameroon wanakowatetea mashoga!

Ndinani & Rocky;

Nawapata kwa undani hoja zenu. Ni kweli Swala la ndoa za jinsia moja kama ambavyo Taifa limetaka kubebeshwa limetikisa na kuamsha hamasa kubwa. Reactions kwa Uongozi wa Taifa, taasisi mbalimbali na jamii yote ya Kitanzania vimedhihirisha mshikamano wa Ustaarabu na utamaduni wa nidhamu ya Kitanzania inapofikia maswala serious kama haya.

Tunaweza kuangalia swala hili kwa upana zaidi na tutaona kuwa TUMEJARIBIWA kuhusu maadlili yetu kijamii na Kitaifa dhidi ya Mahitaji yetu Kijamii na Kitaifa. Na Kufanikiwa, maendeleo ya kweli na ustawi ki maisha ni msururu wa kuyashinda majaribu mbalimbali . Hasa tunapokuwa kuwa tested MORAL VALUES as an Individual or as a Nation.

Kuna tofauti gani Taifa linapoingizwa kwenye Majaribu ya Ndoa za jinsia moja na taifa hilo hilo linapoingizwa kwenye Majaribu ya UBADHIRIFU WA FEDHA ZA WALIPA KODI kupitia mifano tunaoujadili kwenye hii thread, au IPTL na mifano mimgine mingi? Tumesikia watanzania mbalimbali wakiomboleza kuwa UTU NA UBINADAMU wetu hauwezi kuwekwa rehani kwa misaada mbalimbali toka kwa nchi kama uingereza. lakini Mimi nahoji UTU NA UBINDAMU wa Tanzania haujawekwa rehani kwa mifano kadhaa ya ufujaji wa fedha za walipa kodi? matumizi mabaya ya Uongozi, Mgawnayo usio sahihi wa rasilimali za Taifa? Hatuna budi kuangalia swala la Utu na ubinadamu kwa UJUMLA wake sio kwenye nyanja moja tu.

Yuko wapi Kiongozi wa Dhati atuongoze kurejesha UJUMLA wa Uadilifu, Utu na Ubinadamu wa MTANZANIA katika nyanja zote za kijamii na Kitaifa ili kuondokana na aibu ziszo za lazima?
 
Mkuu Azimio Jipya kila ukisoma hapa unapata jipya ambalo lionazidi kukuumiza kichwa
Leo tena ile hela ya EPA kuna kampuni zimeikwapua karibu Bil 20 na hazina mpango wa kurudisha
Aliyekuwa kwenye kitengo cha EPA enzi hizo BOT ndio yeye yeye alioletewa pesa hizo eti za kuendeleza kilimo kwanza TIB na kakopesha makampuni ambayo hayana uwezo wa kulipa
Mtuhumiwa unamkabishi the same money iliyosemekana alioversee kutolewa kwake
Na ndio maana hawa wazungu wanatuona hamnazo wanatupa masharti ya ajabu maana wanaona akili hatuna
 
Tuhoji sasa .. hakuna kiogozi aliye na UTU na UBINADAMU .. hata wa kuanzia na kuja na utatuzi?

Kama hakuna kiogozi wa Tanzania mwenye UWEZO huo ... Utsemaje shhhhhhhhhh Wacha .. kwa Cameroun? That means kama viongozi Kabla ya kukimbilia kumjibu waziri mkuu wa Uingereza .. TUJIHOJI NA KUJITAFITI.

KIONGOZI GANI LEO ANAJEURI YA KUSEMA YEYE ANA UTU NA UBINADAMU ...kwenye kusimamia Ustawi wa jamii na Utu wa Taifa?[/QUOTE]
 
Yes Mkuu ,

About 25% imekwenda kwenye jumba moja tu ... huko shuleni usiombee .. Ndio maana tunalazimika kusema na kuulizia hata kwa mtizamo wa kawaida .. Hakuna hata kusutwa na dhamira? Hakuna hata kuhurumia hao watoto ...wanapokaa chini, hao waalimu wasio kuwa na nyumba nk.

Tuhoji sasa .. hakuna kiogozi aliye na UTU na UBINADAMU .. hata wa kuanzia na kuja na utatuzi?

Kama hakuna kiogozi wa Tanzania mwenye UWEZO huo ... Utsemaje shhhhhhhhhh Wacha .. kwa Cameroun? That means kama viongozi Kabla ya kukimbilia kumjibu waziri mkuu wa Uingereza .. TUJIHOJI NA KUJITAFITI.

KIONGOZI GANI LEO ANAJEURI YA KUSEMA YEYE ANA UTU NA UBINADAMU ...kwenye kusimamia Ustawi wa jamii na Utu wa Taifa?
Nimependa sana ulischosema, hasa kwenye tujihoji na Kujitafiti kuhusu UTU NA UBINADAMU WETU kabla ya kunyooshea vidole wengine! ni rahisi sana kupiga kelele juu ya Ushoga na kusahau kuwa Ufujaji wa mali ya umma uko kwenye kundi hilohilo la Ukosefu wa Utu na Ubinadamu!
 
Solution,

Labda nikuulize swali, Cameroun anafokewa na kukanywa tena kwa maneno makali kuwa asirudie tena wala asiendele kuchezea heshima ya Mtanzania pale inapogusa Uadilifu na tamaduni zake Kwa kuhusisha maswala ya ndoa za jinsia moja. Hivi Utamaduni wa mtanzania ni UPI? Kwani Kiogozi au Mtu mwingine aliyeweka mkataba feki wa madini ameutetea vipi Utamaduni wa Mtanzania? Si kweli kuwa hata huyo hakuutendea haki Utu na heshima ya Mtanzania? Sasa iwe vipi Cameroun akemewe peke yake?
 
Hizo zinaenda mtwara na Kurudi Dar es Salaam wizarani ujenzi nyingine zitakuwa zilisaidia ubunge wa Hawa Ghasia na Uraisi wa KIkwete hawa ni michwaa wanapekenya mpaka ndani ya mninga tukiwaacha bila kuwapiga risasi vizazi vijavyo hawatapata kitu CCM na serikali yake ovyo kabisa

Froida,

Nimevutiwa na matamshi hapo kwenye Buluu, Kwa binafsi ya mawazo yangu ningependa Watanzania tufunguke macho na ikibidi tusiwe kama watu tusiona au tuliopofuka. Kuruhusu mchwa kupekenya kwenye mininga ..pia ni jambo la kudhalilisha utaifa na jamii yetu.

Kama tunaamua kusimamia utamaduni na heshima ya zetu, tusigawanye heshima na maadili. Tunapotishiwa ndoa za jinsia moja tunakurupuka tena kwa ghadhabu, lakini tunapo tishiwa mikataba feke, na uogozi usio na uadilifu kwenye nyanja mbalimbali za kijamii na kiserekali tunajiona watakatifu.. hii sio sawa!

Hivi Mtu unatoa wapi jeuri ya kumkemea Cameroun ..huku umeshindwa kukemea wavunja uadilifu na maadli mabali mbali ya jamii? Huku kitengo unachokiongoza .. kinaharufu ... ya kushuka kwa maadili yote yenye kusimiamia Utaifa na uzalendo?

Tujihoji kabla ya kukurupuka kwa makundi ... kuangalia kwingine... Maana inawezekana wengine wakakemia .. HADHARANI lakini ..kimya kimya wakawa wa kwanza kumuoba waziri mkuu wa uigereza MISAADA YA FAMILIA ZAO!!
 
Solution,

Hivi Utamaduni wa mtanzania ni UPI?
Nafikiri ilibidi hoja ianzie hapa kabla hata ya kumnyooshea vidole Cameroun! ingebidi tujaili kwa kina UTAMADUNI WA KITANZANIA. Kama utamaduni wetu NI kuheshimu na kuenzi UTU NA UBINADAMU, kumnyooshea Cameroun vidole ni sawa. lakini kama Hatuuenzi UTU wala Ubinadamu kwa vitendo bali tunapiga makelele tu, hakuna haja ya kunyoosha kidole kwa mtu yoyote yule!
 
Nafikiri ilibidi hoja ianzie hapa kabla hata ya kumnyooshea vidole Cameroun! ingebidi tujaili kwa kina UTAMADUNI WA KITANZANIA. Kama utamaduni wetu NI kuheshimu na kuenzi UTU NA UBINADAMU, kumnyooshea Cameroun vidole ni sawa. Lakini kama Hatuuenzi UTU wala Ubinadamu kwa vitendo bali tunapiga makelele tu, hakuna haja ya kunyoosha kidole kwa mtu yoyote yule!

Mkuu usiguse kidonda,

Utatonesha wengi, Mimi ungeniuliza swali kuwa kuanzia ngazi ya Uongozi wa BALOZI hadi kufikia uogozi wa KITAIFA .. ni viogozi wangapi wanaouenzi UTU na UBINAADAMU wa kitanzania kwa maswala yote ya KIJAMII ... Ningesema 20%!!

Wakuu zangu,
Nadandia treni kwa mbele....Sisi Watanzania ni Wanafiki kwa hiyo lolote lawezekana. Tupo ktk denial hivyo lolote lisemwalo sii lazima linatoka ktk roho zetu. Yasiwaumize vichwa haya maswala ya Cameroon kwa sababu tunauchukia Ushoga ili hali tunaishi kama Mashoga..Kama tunavyoyakubali ya Biblia na Kuran na radhi kufa kutetea, lakini nani mcha Mungu baina yetu?
 
Kama kawaida nchi hii ni mwendo wa kula tu, Fedha za wavuja jasho wa nchi hii zinaliwa tu kiurahisi rahisi na hakuna mtu wa kuhoji na hakuna mtu atakayechukuliwa hatua. Ndio maana ukarabati wa magogoni hautakaa uishe.
 
Mkuu Azimio Jipya kila ukisoma hapa unapata jipya ambalo lionazidi kukuumiza kichwa
Leo tena ile hela ya EPA kuna kampuni zimeikwapua karibu Bil 20 na hazina mpango wa kurudisha
Aliyekuwa kwenye kitengo cha EPA enzi hizo BOT ndio yeye yeye alioletewa pesa hizo eti za kuendeleza kilimo kwanza TIB na kakopesha makampuni ambayo hayana uwezo wa kulipa
Mtuhumiwa unamkabishi the same money iliyosemekana alioversee kutolewa kwake
Na ndio maana hawa wazungu wanatuona hamnazo wanatupa masharti ya ajabu maana wanaona akili hatuna

MR Roky;

Bado nasema tuna tatizo lililofichika na hatutaki kuliona hadi likue na kukomaa na mataifa ya nje kama uingeerza kuanza kulitumia. Hatujiulizi inakuwaje Taifa kama uingereza kuwa na ujasiri wa kutupangia aina na namna ya kuoana? Nasema wamegundua kuwa sisi kama binadamu hatujitambui na hatujiwezi.

Nitaulizwa ushahidi. Nitajibu tena kuwa mtu mzima anapokuchezea na Malipo ya EPA kama post inavyoonyesha .. Mtu aliye mwerevu .. anakudharau. Mataifa mengine yanagundua kuwa hawa ni wa kufanyiwa lolote! Na kweli wanatujaribu!!

Si tu atakupangia aina ya NDOA ..Kuna siku atakuapngai Lini na lini utakuwa na Mkeo na siku nyingine ...utataikiwa usiulze mkeo yuko wapi. Kwani ukuliza sana ..Utakatiwa misaada! Huu sio ubinadamu na ni kuikiukwa kwa UTU wa mtu. Lakini nafikiri tunayataka wenyewe na tumeyalea na sasa yamekomaa!!

Inawezekanaje hayo kufikiwa. Kwa kuwa Tumepoteza Heshima zetu na uadilifu kama jamii na Taifa. Kila taasisi ya kijamii, kichama na hata kiserekali hakuna inayoridhisha kimaadili hivyo zote ni legelege ... UDHAIFU unaozaa.... Kukosa ufanisi na uzalishaji kwa jamii nzima. Hilo linatupelekea Kuwa omba omba kila kona ya dunia .. Ona sasa masharti tulipoewa na uingereza ..!!Hivi kweli sisi vilema wa nini mpaka kusemwa hivyo hadharani?

Tunahitaji Mapinduzi na ukombozi mpya sio tu wa KIAKILI bali ..KIMAADILI NA KIUTU!! Wengi wa watu wanao liangusha taifa tayari ni wasomi wazuri sana ... hakuna digirii amabazo hawana .. wanachokosa ni UTU na UDILIFU ...

Tujadili pamoja ...shule ya UTU NA UADILIFU iko wapi ... ?
 
Mkuu Azimio Jipya kila ukisoma hapa unapata jipya ambalo lionazidi kukuumiza kichwa
Leo tena ile hela ya EPA kuna kampuni zimeikwapua karibu Bil 20 na hazina mpango wa kurudisha
Aliyekuwa kwenye kitengo cha EPA enzi hizo BOT ndio yeye yeye alioletewa pesa hizo eti za kuendeleza kilimo kwanza TIB na kakopesha makampuni ambayo hayana uwezo wa kulipa
Mtuhumiwa unamkabishi the same money iliyosemekana alioversee kutolewa kwake
Na ndio maana hawa wazungu wanatuona hamnazo wanatupa masharti ya ajabu maana wanaona akili hatuna

kuna mzungu aliwahi kututukana nikiwa huko kwao nasoma alisema the only place ambayo tunafit best sisi wabantu ni kwenye forest na wanyama huku kwingine tunajilazimisha na hatufit! Na alikuwa specific bantus!
 
Wakuu zangu,
Nadandia treni kwa mbele....Sisi Watanzania ni Wanafiki kwa hiyo lolote lawezekana. Tupo ktk denial hivyo lolote lisemwalo sii lazima linatoka ktk roho zetu. Yasiwaumize vichwa haya maswala ya Cameroon kwa sababu tunauchukia Ushoga ili hali tunaishi kama Mashoga..Kama tunavyoyakubali ya Biblia na Kuran na radhi kufa kutetea, lakini nani mcha Mungu baina yetu?

Mkuu treni haijafika mbali!!

Mkoloni karudi ..hachezei mbali ..kaizuia...!!

Kikubwa Mkuu wangu siamini macho na masikio yangu ... Tiafa limetakwa Mkuu!!
Tumedhalilishwa. Nimesikia viongozi mabalimbali wakipaza sauti zao juu na kukemea!. Wamekemea kwa nguvu kuptia kila vyombo vya habari. Nikapata shauku kuwatizama na kuwaona.

Lo! Nikashaangaaa. ! Hawa wanapata wapi Jeuri ya Kufanya hayo wafanyayo! Nasikiliza kwa makini nasikia ...WANATETEA MAADLILI YA KITANZANIA .. Nikazidi kushangaa.. Maadili na Utu wa Mtanzania nikashaanga tangu lini hawa wamekuwa wanfanya haya? .. Sauti za juu hivyo baada ya kutamkiwa aina ya ndoa na mzungu wa ulaya? Nikajiuliza hivi Hawa waanelewaje Maadili ya jamii na Taifa labda akili mwao tu lakini sio kwa Vitendo... Mbona wanafanya mzaha na rasilimali za Taifa... Mikataba ya AIBU, Mgawanyo wa rasilimali Kwa kukiuka haki, utu na heshima ya Jamii mbalimbali za Kitanzania .. Nikalazimika kuona kuwa hapa kuna tatizo ..inawezekana kuwa la kinafiki ...Lakini wanapata wapi jeuri ... Hiyo .. Nikajua huu ni UPOFU .. Leo tumetakiwa kusikiza Wapinga UTU wa Kiigereza watupangie aina ya ndoa .. hawana adabu hawa ..Kesho ..watakuja watatupangia ..aondoke na binti yangu nyumbani ...nikizoza .. nakatiwa msaada..Hivyo nifunge mdomo!

Mkuu ... hapa tunakwendawa wapi?

Ni kweli wametusoma ... Wametuona hatujiheshimu ... ona Jumba la huko Mtwara .. limemeza Tsh Ngapi ... na watu wanapita na kushuka wanafurahia dili imejibu ...Mkuu wametusoma ... wametutambua na wamejiridhisha ... wameona hawa majuha ...hawana chembe ya utu wa kuwapelekea hata kuipenda Nchi yao hata kidogo, Uzalendo umekufa , wametuona na wametuelewa ..hawa wapitisha bakuli ..dunia nzima ... Hawana soni wala aibu ..heshima hawa ...Leo ..Tumesiwa hadharani ...Mkuu hapa tunafanyaje? kama Taifa na kama jamii?
 
Azimio Jipya,

Nakuelewa sana lakini jambo moja lazima tulitazame kwa makini sana. Kuruhusu Ushoga ni jambo jingine kabisa tofauti na kuruhusu ndoa za mashoga yaani swala hili linaingia katika kurekebisha sheria zetu za wanandoa UTU na Mila zetu. Ushoga upo na sidhani kama kuna sheria ya kuupiga vita kiasi kwamba iwe issue kubwa..lakini sidhani umewahi kuona ama una ushuhuda wa ndoa za watu wa jinsia moja hapa nchini hata kisiri, na kama wapo na wanaishi kama wanandoa basi hesabu yao haifikia hata 1000. Kwa hiyo hatuwezi kubadilisha sheria zetu kwa mapenzi na matamanio ya watu 1000 kwa sababu tu Uingereza wamesema wakati wao karibu nusu ya population yao Ushoga ni sehemu ya maridhio ya matamanio yao na kushusha presha ya mkonga..Kesho tunaamrishwa kuzitambua ndoa za watu na mipira au sanamu maanake wazungu wana mapenzi sana na vitu vya kuchonga kuliko binadamu.

Kwa hiyo tunarudi pale pale WATU na MAZINGIRA, kwetu bado hatujafika huko waliko Uingereza na ikitokea kwamba Ushoga umechukua nafasi kubwa ya maisha ya matamanio ya Watanzania tutakubali na kubadilisha sheria zetu... Wao leo wana Subways matreni yakienda chini kwa chini tena kwa madai ni haki ya wananchi ktk usafiri.. Sasa ni lazima nasi tufike huko leo hii jamani? Mimi binafsi yangu ninapowaona wazungu wamemfunga kamba ya shingo hana muda wa kufanya mapenzi wala kujichana na mbwa wenzake huingiwa huruma sana kwa mbwa hao japokuwa wao wanaonyesha mapenzi makubwa.

Hawa wazungu mkuu wangu hawatupendi yaani wangeweza wangetufukuza Ulaya nzima lakini wamebanwa na sasa hivi wanaweka sheria ngumu sana kwa mtu mweusi kuhamia Ulaya mbona sisi hatuwalazimishi wao hata kulegeza tu sheria kwa sababu hakuna sababu yao kutuchukia isipokuwa kwa weusi wetu. USA wamejaa Warusi, Waromania, Schec waliongia tu toka kuvunjika kwa East block wengi kuliko mataifa yote na wanajiona nyumbani kuliko mtu mweusi mwenye generation tano zilizopita ndani ya US. Kwa hiyo tunahitaji msomamo wetu katika hili la ndoa, hatuwachukii mashoga lakini hatuupendi Ushoga na ndio maana sio maarufu ktk wanandoa...
 
Mkandara ;

Umepanua mtizamo wa hoja yenyewe! Na itatupa namna pana ya kulitizama swala zima lenyewe.

Mimi hoja hii imenipa fursa si kuchambua aina ya ndoa na mahusiano ya mke na mume yaweje? Nimeshikilia hoja ya MAADILI NA UADILIFU WA KITANZANIA KWA UJUMLA! Hoja nyingi zimetolewa kwa MADAI YA KUSIMAMIA maadili ya Jamii na KITAIFA! Ndio Mimi nikajiuliza Maadili ya Kitanzania si ndoa au hoja ya ushoga peke yake. Mbona hili ndio limeshikiwa bango kiasi hiki? .... Au Kuna kitu sijaelwa nini?

Kusema kweli nimevutiwa na VUGU VUGU ZIMA LA KUOGELEA MAADILI, UADILIFU, UTU NA UBINADAMU WA MTANZANIA kama unavyochochewa na Hoja ya Ushoga ndoa zao nk! Mimi hapa hoja sio ushoga. HATA KAMA MADA HII INGECHOCHOWA NA TABIA NYIGINE INAYOPELEKEA KUVUNJA MAADILI YA KIJAMII NA KITAIFA ... ingenivutia vilevile!! Tuuache ushoga na aina zake na jamii zake nk!!

Nikisikia IKULU leo inashikia Bango ..walevi wa Gongo, Madawa ya kulevia, Watu kutokupenda na kuwajibikia KAZI (Uvivu), Nyumba ndogo .. Nk ..lazima ningeshituka sana .. Nigeuliza kwa nini sasa? Ikulu, dini mbalimbali, jamii nzima ..zinazungumzia Maadili ya Kitaifa? Tena Watanzania wote wameungana ..Bila dini, Bila Kabila, bila kuangalia vipato Nk ... Jambo hili hakika ..Lingenivutia... Ningependa kuangalia FORCES BEHIND!!

Ningehoji, Maadili, Uadilifu ... Ni nani huyo anayelisemea hilo ...anatania au ..amekurupuka...? ..AMEWAHI KUYASEMEA MANGAPI KIUADILIFU NA KIMAADILI YA MTANZANIA ...

Ningejiuliza kwa nini asiogelee nyumba ndogo, ubadhilifu wa mali za umma, Ufisadi, ugawanyawaji mbovu wa rasilimali za Taifa, rushwa na tabia nyingine zenyekudhalilisha Ubinadamu na hadhi ya Mtanzania!? Nigelazimika kuangalia kama kweli kauli, fikra na matendo yake ..Yanamaanisha Kusimamia MAADILI YOTE YA TAIFA ...AU YALE TU ANAYOCHAGUA KWA AJILI YA KUJIJENGA KISIASA ..AU.. Kwa sababu tu ya misukumo ya kulazimishiwa!! Ni kweli anaamini kile anachosema?

Nini kinazuia Swala la Tabia nyingine kadhaa kinyume na utu na ubinadamu kisiasa, kijamii na kiserekali zisikemewe kwa nguvu hii hii ya Ushoga? Mimi Nafikiri hapa kuna tatizo.

Huko nyuma tumeona Viongozi mbalimbali wasivyo na UADILIFU WOWOTE inapokuja maswala ya Maadili ya taifa Kiuchumi, Kisiasa au Kiuongozi!! Leo viongozi hao hao wanaposimama kuonyesha HASIRA KALI na kwamba wana misimamo, uadilfu, maadili ..Ahhh !! Tutawaamini je? Wameyatoa wapi ...overnight? ... Isije ukawa ni usanii mwingine!!?

Ninachosema kama kweli wakati wa kuogelea MAADILI YA TAIFA UMEFIKA .... Jambo hilo lisfanyiwe mzaha!! Lifanywe si kutizama ushoga peke yake, hilo ni tatizo moja kati ya mia moja yanayofanya MAADILI NA UTU WA TAIFA!!
 
Kama kawaida nchi hii ni mwendo wa kula tu, Fedha za wavuja jasho wa nchi hii zinaliwa tu kiurahisi rahisi na hakuna mtu wa kuhoji na hakuna mtu atakayechukuliwa hatua. Ndio maana ukarabati wa magogoni hautakaa uishe.

Matukio kama yako mengi! Nafikiri huu ni Ukiukwaji wa Uadilifu na maadili mema ya Kijamii na kitaifa! Viogozi wakishindwa kuyasemea haya ... Wataaminikaje ..kuja kuusema ndoa za jinsia Moja?

Mkuu Azimio Jipya kila ukisoma hapa unapata jipya ambalo lionazidi kukuumiza kichwa
Leo tena ile hela ya EPA kuna kampuni zimeikwapua karibu Bil 20 na hazina mpango wa kurudisha
Aliyekuwa kwenye kitengo cha EPA enzi hizo BOT ndio yeye yeye alioletewa pesa hizo eti za kuendeleza kilimo kwanza TIB na kakopesha makampuni ambayo hayana uwezo wa kulipa .Mtuhumiwa unamkabishi the same money iliyosemekana alioversee kutolewa kwake
Na ndio maana hawa wazungu wanatuona hamnazo wanatupa masharti ya ajabu maana wanaona akili hatuna

Soma sehemu ya gazeti hili. Heri tubaki masikini.... Ili KUSIMAMIA UTU NA MAADILI YA MTANZANIA ... Mbona kichekesho ... Kufujwa kwa Hizo fedha za EPA ... hakuonekani na kuchukuliwa kuwa ni janga ya kupotea kwa MAADILI YA UTU NA MAADILI YA MTANZANIA?

MEMBE: HERI TUBAKI MASKINI
na Tamali Vullu
RAIS Jakaya Kikwete amekataa kumpokea balozi mpya kutokanchi moja ya kigeni baada ya kubainika kuwa amefunga ndoa na shoga.
Siri hiyo iliwekwa wazi jana na Waziri wa Mambo ya Nje naUshirikiano wa Kimataifa Benard Membe alizungumza na waandishi wa habarikuelezea msimamo wa Tanzania kuhusiana na kauli ya Uingereza ya kuzitaka nchizinazopokea misaada kutoka nchini humo kuhalalisha vitendo vya ushoga.
Membe alisema tukio hilo lililomshtua Rais lilitokeamwanzoni mwa mwaka huu, pale alipopokea barua kutoka nchi moja (hakuitaja)ikimtaka wampokee balozi wao mpya na mkewe, lakini walipobaini kuwa mke huyo nimwanaume Rais Kikwete alikataa.

Alisema baada ya kugundua hali hiyo, Kikwete akiwa haaminikile alichokisia alitamka maneno machache "Toba Yarabi" na kuagiza balozi huyoasikubaliwe kabisa. Waziri huyo alisema hata baada ya nchi hiyo kukataliwa,ilibembeleza sana kwa siku kadhaa ikidai kuwa kusingekuwa na madhara yoyote kwabalozi huyo kufika nchini na mke wake (shoga) na kwamba angetimiza wajibu wakekikamilifu. "Waling'ang'aniamsimamo wao, lakini baada ya siku nne walituelewa na kusema kuwa sisi nimarafiki wao na hivyo waliheshimu msimamo wa Tanzania na kuahidi kuwawasingemleta tena balozi huyo na mkewe," alisema.

Membe alisema amelazimika kusema jambo hilo kuonyesha kuwaTanzania inapinga kwa nguvu zote tabia za ushoga na kueleza kuwa haiko tayarikutunga sheria ya kuruhusu ushoga nchini.

Akizungumza kwamkazo, Membe alisema Tanzania iko tayari kwa lolote na hata kubaki na umaskiniwake kuliko kupokea misaada yenye masharti ya hovyo. "Tunataka kutunzaheshima yetu. Kama wanadhani misaada itatolewa kwa masharti hayo wakae na fedhazao, hatukubali kutekeleza jambo hilo," alisema.

Akiungana na viongoziwa dini walioitaka serikali isikubali wala kutishwa na nchi hiyo, Membe alisemaTanzania haiwezi kutekeleza sharti hilo hata kama ni maskini na itaendeleakuheshimu misingi ya maadili ya taifa inayokataza mambo ya ushoga.

"Hii ni nchi inayofuata maadili na haiko tayari kupokeaushauri katika suala hilo...hata nchi ikiwa kubwa kiasi gani, linapokuja sualala utaifa, hatutakubali kuyumbishwa hata kidogo," alisisitiza Waziri Membe.

Waziri Mkuu waUingereza, David Cameron, hivi karibuni alitishia kusimamisha misaada kwa nchizinazopinga haki za mashoga na kuzitaka zile zinazopokea misaada kutoka nchinihumo ikiwamo Tanzania zikubali sharti hilo.

Membe alisema kuwa staili ya sasa ya kuunganisha misaada nasuala la ushoga ni tamko hatari ambalo linaweza kuvunja uhusiano na nchinyingine.
"Tamko hili linawezakuvunja Jumuiya ya Madola na ikitokea ikawa hivyo, Waziri Mkuu wa Uingerezaanapaswa kuwajibika," alisema Waziri Membe.
Aliongeza kuwa katiya nchi 54 za jumuiya hiyo, 13 pekee ndizo zinazounga mkono suala hilo na kuonyakuwa suala hilo si la kushabikia hata kidogo. Hata hivyo, waziri huyo alisema suala hilo halikuwa ajendakatika mkutano uliomalizika hivi karibuni nchini Australia, bali Waziri Mkuuhuyo aliibua katika vikao vya viongozi wakuu wa nchi.

"Suala la ushoga halikuwa ajenda na wala halikuzungumzwakwenye mkutano ule; alichofanya Waziri Mkuu huyo ni kuibua suala hilo katikavikao vya viongozi walipokuwa wakijadili haki za binadamu. Hii ndiyo sera yachama chake cha Conservative.

"Hata hivyo jambo hilo lilikataliwa na lilipofika kwenyemkutano walizungumza kwa mafumbo, lakini tulikataa," alisema.

Alisema sheria za nchi za mwaka 1971 ambazo Tanzaniaimeziridhia kutoka kwa Waingereza zinakataza suala hilo na kutamka kuwalinapofika suala la ndoa au mahusiano ya kimapenzi linahusisha watu wa jinsiatofauti.

"Wote tunajua msingi wa familia ni mume na mke ambaowanaweza kuzaa watoto...pia sheria ya makosa ya jinai inaeleza msimamo ndiohuo, hivyo kwenda kinyume ni makosa ambayo mtu anaweza kufungwa kifungokisichopungua miaka 30 jela," alisema na kuongeza kuwa kwa msimamo huo serikalihaivitambuia vikundi vya kishoga vilivyoko nchini.

MY TAKE

Ni kweli hapa Tanzania kwa sasa kuna Utamaduni wa kutetea MAADILI YA KITAIFA ... kwa hali yeyote ile hata ikibidi kuukubali kuyafia? Kwani kudiriki kusema kuwa hata kama ni kuwa UMASIKINI na tuwea lakini UTU KWANZA, UBINADAMU KWANZA NA UZALENDO KWANZA ....haya ni ya kweli?

Waziri anaamini kwa anachokisema?
 
Nakubalina na wewe kabisa ktk hoja zako na ndio maana watu wengi hawafahamu kwamba WATU na MAZINGIRA ndio huitengeneza jamii na sii kuiga vitu. Tanzania kama Tanzania tuna matatizo yetu hili neno MIIKO na MAADILI lina uzito mkubwa na tofauti kubwa, lakini sii kila nchi ina mapungufu sawa hivyo mnalazimika kutunga sheria (miiko) kutokana na kupotea kwa maadili yetu na sii yao.

Mimi nadhani Membe hana kosa maadam ni Uingereza ndio wanataka sisi tufanye vitu kwa mtazamo wao hali jambo hili kwetu halina mvuto, nikiwa na maana Ushoga upo na hawanyimwi haki zao la wala sijasikia shoga kauawa kwa sababu ya ushoga isipokuwa tuna matatizo mengine mengi sana ktk wigo pana la maadili ikiwa ni pamoja na yote uloandika..

Hivyo wakati sisi tunakabiriwa na matatizo ya Ufisadi, ubadhilifu wa mali za umma, ugawanyawaji wa rasilimali za Taifa, rushwa na tabia nyingine zenye kudhalilisha Ubinadamu na hadhi ya Mtanzania wao wana tatizo kubwa la UBAGUZI ambalo sisi hatuna. Wao wanafanya usafi wa ndani kulingana na matatizo ya WATU wake nasi tunatakiwa kufanya usafi ktk matatizo ya jamii yetu.Labda nikukumbushe tu kwamba wao walipokuwa na sheria za mtu mweupe kuoa mtu mweusi ni haramu, ilifikia wakalazimika kisheria kubadilisha sheria hizo ktk kuutazama UTU wa binadamu, lakini hili halikuwa tatizo kwetu kwani hatukuwa na ubaguzi kama wao, tuweke sheria tusiweke isingebadilisha hali halisi kwa sababu haikuwa mila wa desturi ya Mtanzania kumbagua mtu ktk maswala ya mapenzi au ndoa.

Wakati wao hadi majuzi tu, Queen haruhusiwi kuoa nje ya dhehebu la dini yake sisi rais au kiongozi yeyote anaweza kuoa toka dini yoyote na hatuwezi kutunga sheria kulazimisha watu kuoa toka dhehebu lolote..Hivi kweli tunaweza kuwalazimisha nchui za ulaya kutambua ndoa za kiislaam ama kiasili hata kama mtu ana wake wangi na wakakubaliana na mtazamo wetu? - Sidhani!

Kwa hiyo, Watu na Mazingira yake ndio hutengeneza itikadi, sera na sheria za tawala ktk ujenzi wa Taifa. Nina hakika huyo huyo Cameron ukimwambia kama anaweza ku date au kuoa mwanamke Muislaam hatakubali kabisa na sidhani kama atakuwa na jibu zuri. Wala Uingereza hawawezi kuifanya sheria kwa sababu Tanzania mapenzi hayana dini.. Na anafungwa na hiyo miiko na Maadili yao ambayo sisi huku kwetu hatuna miiko hiyo isipokuwa ni swala la watu wenyewe.. Na ndio maana haswa ya kuchukua msimamo wa kwamba Tanzania ni nchi isiyokuwa na dini isipokuwa wananchi wake ndio wenye dini, Uingereza hawawezi kuchukua msimamo kama wetu hata kama tunaiona haki kubwa ktk mtazamo wetu.

Mwisho, sidhani kama kuna tatizo lolote ktk majibu ya Membe kwa waingereza maadam wao ndio wametaka sisi kumtambua huyo mke mume wa Balozi kwa sababu wao nd hii ni halali na ipo ktk katiba yao..Sisi maswala ya MATAMANIO hayapo ktk miiko na maadili yetu kwa sababu hatujawahi kuwa na ubaguzi watu ktk maswala ya Mapenzi..Wao walikuwa na ubaguzi ambao uliathiri maisha ya watu wengi na ndio maana wakatunga sheria na kuwapa haki zao ktk ukujenga usawa..Sasa sisi tuna matatizo ambayo wao hawana na tunatakiwa kutunga sheria kulingana na mazingira yetu. Ni sheria kwa kila nyumba UK na Ulaya kuwa na Heating system (heater) kutokana na baridi ambalo linaua lakini sisi hatuwezi kuweka sheria kama hiyo kwa sababu mazingira yetu yanaifanya Heater au airconditon kutokuwa lazima..

Yeye Cameron kama anamtaka shoga aje tu Tanzania atapewa na atajirusha wala hakuna atakaye mnyanyasa isipokuwa huko kwao UK ndiko watammaliza ingawa kwao Haikuharamishwa...Huu wote ni UNAFIKI wa binadamu.
 
Nakubalina na wewe kabisa ktk hoja zako na ndio maana watu wengi hawafahamu kwamba WATU na MAZINGIRA ndio huitengeneza jamii na sii kuiga vitu. Tanzania kama Tanzania tuna matatizo yetu hili neno MIIKO na MAADILI lina uzito mkubwa na tofauti kubwa, lakini sii kila nchi ina mapungufu sawa hivyo mnalazimika kutunga sheria (miiko) kutokana na kupotea kwa maadili yetu na sii yao.

Mtizamo wa swala la Ndoa za jnsia moja, ingawa kwenye mazingira yetu ya Tanzania limechukuliwa na wengi kama swala kinyume na Desturi na misingi ya ubinadamu wetu! Sidhani hapa Tanzania kama kwa vyovyote vile linakubalika.

Na viongozi wengi wameltolea macho hilo kwa nguvu zote na kuonekana kama mashujaa wakubwa!

Binafsi siwaoni mashujaa wa utetezi wa desturi nzuri na Tamaduni za Mtanzania ... Huku wakiacha mambo mengine mengi yaliyo na uzito wa desturi nzuri na desturi za Mtanzania... ni unafiki ... Tungeanza kuonyesha ujasiri wetu wa kuutetea Utanzania wetu kwa kuzuia ubadhirifu wa RasiliMmali na mali za Umma.
 
Back
Top Bottom