Truworths, Identity and 4u2 to close shop in Tanzania over endless losses

Kikwete alivyoona foleni hazipungui barabarani akatangaza kuwa uchumi umekuwa na ametengeneza middle class ya kutosha,kumbe hajui kuwa hizo Toyota ni mikopo na wakopaji wengi wanaingia mitini kulipa.Wenzetu Ghana,Kenya serikali zina sera thabiti za kutengeneza middle class wakati Tanzania ina sera ya kutengeneza MAFISADI.Kwa Serikali makini middle class ndio engine ya maendeleo.
 
hii habari imekaa kikenya mno
mbona mafuruki anaongeza tu maduka. Wameshindwa biashara kwa ajili ya ulanguzi wao. Hili ni soko huria kwa hiyo mteja anaenda pale bei inapokuwa nafuu. Wao walikuwa wanauza nguo za low quality halafu expensive kupita uk yet uk wages ziko juu na rent juu kupita tz.
Hamna kitu muhimu kama ushindani, jamaa wameshindwa kwa ajili ya bei na low quality.

Kuhusiana na hasara serikali itakayoipata- hamna watu ambao ni wakwepaji wa kodi kama haya makampuni ya kigeni, halafu kitu kingine kibaya zaidi ni capital flight- wakipata hela kidogo transfer nje. AMKENI muwaangalie hawa watu kwa jicho lingine

Kuhusiana ukubwa wa kodi, bei zitashuka zenyewe kutokana na supply.
Halafu hiyo average ya $40 per sq m ni uongo. Dar ni expensive lakini siyo 40. Hizi habari zinazoandikwa na wakenya inabidi muwe waangalifu.

Kuhusu kuregulate kuna maeneo mawili moja jinsi ya madalali/estate agents kuoperate na nyingine mda wa kulipa kodi, lakini suala la bei market itachukua mkondo wake
 
Ukitaka kujua kama Tanzania is a hopeless country

Hakuna mtu aliyefanya analysis kuwa hawa jamaaa wakiondona how much loss Taifa litaingia

Hakuna mtu aliyejaribu kukaa na hawa jamaa waka address matatizo wanayokabiliana nayo

and of course no one cares

Nchi ya "KUBAHATISHA" na "KUIGA"..... usitegemee kitu cha ajabu!
 
Awe mkweli huyu jamaa anadai kuwa Dar kuna MALL 2 tu?
MLIMANI CITY
SHOPPERS PLAZA-Msasani
SHOPPERS PLAZA-Masaki
MAYFAIR PLAZA
SEACLIFF VILLAGE
QUALITY CENTRE
Bado nyingine ndogo ndogo...O'bay Shoping Centre,JM Mall,Tevi etc kingine kinachofanya WaTZ tusiwe na utaratibu wa ku-shop ni utitiri wa Boutique na Groceries stores zilizopo kila baada ya mita 10... Kampala,Lusaka,Nairobi,Kigali hakuna hilo pole zenu wa-Kenya...

Mkuu wangu tofautisha malls na viduka. Nadhani hata hivyo Tanzania hatuna mall hata moja tuna vishopping centre vichache. Kodi za hivyo vishopping centre ni ajabu. Real estate business kwa Tanzania bado ipo chini mno na hivyo wawekezaji wanafanya market skimming wanapata super economic profit.

Ila nimeshangaa juzi NSSF wanaenda kujenga mall huko Kenya na kuna watu wakasema humu kwamba inalipa zaidi Kenya kuliko hapa. Lakini mbona taarifa hii inaonyesha kwamba rent ni ya juu kwa Tanzania, kulikoni huu uwekezaji wa NSSF huko Kenya.

Jana nimepita nikakuta jamaa wameishafunga maduka yao! Pamoja na hayo watanzania tunavaa mitumba hatuna utamaduni wa.kwenda kununua hiyo minguo yao. Ukitaka kuwapatia watanzania wekeza kwenye pombe. Nadhani samaki samaki inapata faida kubwa kuliko maduka yote yaliyopo Mlimani City.

Nakubaliana na Mama Dr. kwamba tunaenda kushuhudia anguko la uchumi kutokana na mambo ya pango.
 
Mkuu Tusker Baridi, hawa jamaa wameshindwa tuu kufanya biashara kwa sababu bei zao sio attractive kwa level ya middle class ya Tanzania japo nakubali ni kweli reantal fee ya nyumba ni kubwa, ukweli ni kuwa hao waiowatarget kama middle class kwa bei zao, wan ao aford sio middle class bali ni high class ambao wana access kupata kila kitu huko vinakotoka.
Acha wajiondokee tuu nao walikuwa wanatukamua sana!.
Kabla ya kufunga biashara kutoka na kupata hasara iliyochangiwa na uchache wa wateja, kuna mambo mengi ambayo unaangalia na kubwa likiwa ni bei ya bidhaa.Hawa jamaa wame operate kwa hasara mwaka mzima, kama walishindwa kupunguza bei ili waweze kushindana maduka mengine ni lazima ilikuwa nje ya uwezo wao.

Mimi nina six kids, (3 girls na 3 boys) last December ile nyingine, nilitoka na family for X-mass shopping, nikaanzia W-Store pale mjini, nilipata vitu vya maana vya only small ones. Takaingia duka la pili lile la jeans za Levi Straus, ndio hili la hawa jamaa, kabinti kakapenda jeans, kuuliza bei naambiwa TZS 138,000, binti anang'ang'ania kuwa etiu ni fashion ya sasa iliyotoka na mama yao akasupport, Kaka yake na dada yake ambao ni ma teenager, wakashauri "Dada kama ....anaitaka jeans hiyo, nipe 50,000 tuu nikamnunulie mahali!. Kusema ukweli tulitoka bila kununua chochote humo ndani!.

Maadam wale wawili wadogo wameshapata nguo, wale wawili wakubwa wakaomba wapewe pesa wao na waende na wadogo za "mahali" wakawanunulie nguo. Niliwapa, japo concern ya mama yao, wasije wakatinga Kariokoo kutuzolea mchina, my boy akasema no, mchina tunamjua, wee leta pesa tunakuja na nguo za ukweli!. Kilichofua walirudi na nguo za ukweli za level ile ile ya maduka makubwa!. Ndipo wakasema kuna viduka tuu mitaa vinaleta nguo za ukweli na bei ni poa!. Kama ni hivyo, nani aende Mlimani city akachinjwe?
Sababu mojawapo ya hili duka kufunga milango lipo kwenye hii post yako...Hakuna duka lolote wanaweza kuagiza Levis kutoka LS&CO na wakalipa kodi halafu wakafaniwa kuuza kwa 50,000 lazima awe ni Mchina na kukwepa kodi.Haya maduka makubwa yatakuja na kuondoka hata kama kodi za pango zikishuka kama serikali haita dhibiti bidhaa feki na ukwepaji kodi.

Kukimbia maduka makubwa yanayolipa kodi na kwenda kununua kwenye maduka yanayokwepa kodi ni kuunga mkono ufisadi;wanachofanya wao na wachofanya Barrick Gold ni moja.

Original plus kodi haiwezekani Tanzania
 
kuna ukweli fulani lakini kuna vitu havijazungumzwa.....

culture...........

wakenya siku nyingi wana western culture hata kwenye shopping....

vitu kama nyanya za kopo na kwenda supermarket kenya ni kawaida....

Tanzania kuna culture ya east zaidi .....bazaar culture......hata india hakuna malls nyingi kama south africa...

infact Kenya ina MALLS nyingi na miaka miingi kuliko India......

sasa sisi wa TZ ukitaja tu Kariakooo......nchi nzima anaelewa unazungumzia nini....

the largest shopping mall aka bazaaar shops in africa maybe......
 
kuna ukweli fulani lakini kuna vitu havijazungumzwa.....

culture...........

wakenya siku nyingi wana western culture hata kwenye shopping....

vitu kama nyanya za kopo na kwenda supermarket kenya ni kawaida....

Tanzania kuna culture ya east zaidi .....bazaar culture......hata india hakuna malls nyingi kama south africa...

infact Kenya ina MALLS nyingi na miaka miingi kuliko India......

sasa sisi wa TZ ukitaja tu Kariakooo......nchi nzima anaelewa unazungumzia nini....

the largest shopping mall aka bazaaar shops in africa maybe.....
.
Dont worrym Kariakoo soko linavunjwa very soon
 
Back
Top Bottom