Trump aitibua China kwa kuongea na Rais wa Taiwan

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Trump Aaanza Kuitibua China

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uchina, Wang Yi

Wizara ya mashauri ya nchi za nje ya Uchina, inasema kuwa imepeleka malalamiko kwa upande unaohusika wa Marekani, baada ya Rais mteule Donald Trump, kuzungumza kwa simu na rais wa Taiwan.

Rais mteule Donald Trump

Uchina inaona Taiwan kuwa ni jimbo lake lilojitenga na siyo nchi. Msemaji wa wizara alisema, Uchina ni moja, na ndio msingi wa kisiasa katika uhusiano baina ya Marekani na Uchina.

Mazungumzo ya simu baina ya Bwana Trump na Rais wa Taiwan, Tsai Ing-wen, yamevunja msimamo wa kidiplomasia kwa Marekani.

Hapo awali, waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uchina, Wang Yi, alisema mazungumzo hayo ya simu ni “ujanja wa Taiwan usiokuwa na maana”.

Imeelezwa kuwa, ikiwa simu hiyo ni ishara ya mabadiliko ya sera za Marekani kuhusu Taiwan, basi Uchina itajibu kwa hasira.

View image on Twitter
CyweR2sWEAEax68.jpg:small

https://twitter.com/GlobalHabari
Donald Trump akiuka utaratibu wa Marekani kwa kuzungumza na Rais wa Taiwan eneo ambalo Marekani hailitambui kama nchi bali sehemu ya China.
chanzo.GBP
 
Donald Trump's promises on China.

43. Aggressively challenge China's power in the world by declaring the country a currency manipulator, adopting a "zero tolerance policy on intellectual property theft and forced technology transfer" and cracking down on China's "lax labor and environmental standards."

44. Rather than throw the Chinese president a state dinner, buy him "a McDonald's hamburger and say we've got to get down to work."
 
Hii ya China na Taiwan ni kama Tanzania bara na koloni lao Zanzibar. Wanawashikiliwa kwa lazima hawataki kabisa kuona Taiwan ipo huru.

Mimi najiuliza kama majority ya wakazi wa Taiwan wanataka wajitawale tena wakiwa na sababu nzito who are you to stop them?

Kwa upande mwingine nafahamu China hataki kumwachia Taiwan kwa sababu za kiuchumi, na ushawishi kisiasa pia. Wachina waache zao Taiwan wanataka kuwa huru.
 
China nao nilikuwa najua anatawala hong Kong tu kumbe hadi Taiwan, lakini Taiwan wananguvu zaidi kuliko sehemu kama Tibet na Hong kong, hizi no sehemu muhimu kwa ustawi wa China ndio maana anawang'ang'ania sana
 
kumbe taiwan sio nchi ni jimbo, wangeungana kama zanzibar na tanganyika na kuzaa nchi mpya badala ya malumbano ya kupigiana sim
 
Na alivyokuwa anasema China is ripping the US in trade deals, halafu anaongea na Taiwan baada ya kuchaguliwa. Acha China washtuke.
Kaongea pia na Duterte. Tusije sikia kaongea na dogo Kim..
 
Hii ya China na Taiwan ni kama Tanzania bara na koloni lao Zanzibar. Wanawashikiliwa kwa lazima hawataki kabisa kuona Taiwan ipo huru.

Mimi najiuliza kama majority ya wakazi wa Taiwan wanataka wajitawale tena wakiwa na sababu nzito who are you to stop them?

Kwa upande mwingine nafahamu China hataki kumwachia Taiwan kwa sababu za kiuchumi, na ushawishi kisiasa pia. Wachina waache zao Taiwan wanataka kuwa huru.
Mkuu, kanda ya Kaskazini nao wakitaka kujitenga kama alivyoshauri Mh. Nassari nao tuwaache tu waunde hiyo Kaskazini Republic? Ukiruhusu hili basi hutakuwa na nchi na historia imeonyesha kuwa wakati mwingine "the masses" wala huwa hawajui wanachokitaka. Jimbo la Texas kule Marekani wamejaa kiburi cha mafuta na wameshatishia kujitenga mara nyingi lakini wanajua wakijaribu kufanya hivyo si ajabu wakala mkong'oto kutoka serikali kuu ya shirikisho.

Mara nyingi kunakuwa na sababu fungamano za kihistoria, kiuchumi, kijamii, kivita na kisiasa katika migogoro hii. Sina uhakika kama China na Taiwan ni sawa na hii ya Tanganyika na Zanzibar. Itabidi nijisomee zaidi.
 
Trump Aaanza Kuitibua China

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uchina, Wang Yi

Wizara ya mashauri ya nchi za nje ya Uchina, inasema kuwa imepeleka malalamiko kwa upande unaohusika wa Marekani, baada ya Rais mteule Donald Trump, kuzungumza kwa simu na rais wa Taiwan.

Rais mteule Donald Trump

Uchina inaona Taiwan kuwa ni jimbo lake lilojitenga na siyo nchi. Msemaji wa wizara alisema, Uchina ni moja, na ndio msingi wa kisiasa katika uhusiano baina ya Marekani na Uchina.

Mazungumzo ya simu baina ya Bwana Trump na Rais wa Taiwan, Tsai Ing-wen, yamevunja msimamo wa kidiplomasia kwa Marekani.

Hapo awali, waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uchina, Wang Yi, alisema mazungumzo hayo ya simu ni “ujanja wa Taiwan usiokuwa na maana”.

Imeelezwa kuwa, ikiwa simu hiyo ni ishara ya mabadiliko ya sera za Marekani kuhusu Taiwan, basi Uchina itajibu kwa hasira.

View image on Twitter
CyweR2sWEAEax68.jpg:small

https://twitter.com/GlobalHabari
Donald Trump akiuka utaratibu wa Marekani kwa kuzungumza na Rais wa Taiwan eneo ambalo Marekani hailitambui kama nchi bali sehemu ya China.
chanzo.GBP
Ushindani huu mpaka lini
 
Mkuu, kanda ya Kaskazini nao wakitaka kujitenga kama alivyoshauri Mh. Nassari nao tuwaache tu waunde hiyo Kaskazini Republic? Ukiruhusu hili basi hutakuwa na nchi na historia imeonyesha kuwa wakati mwingine "the masses" wala huwa hawajui wanachokitaka. Jimbo la Texas kule Marekani wamejaa kiburi cha mafuta na wameshatishia kujitenga mara nyingi lakini wanajua wakijaribu kufanya hivyo si ajabu wakala mkong'oto kutoka serikali kuu ya shirikisho.

Mara nyingi kunakuwa na sababu fungamano za kihistoria, kiuchumi, kijamii, kivita na kisiasa katika migogoro hii. Sina uhakika kama China na Taiwan ni sawa na hii ya Tanganyika na Zanzibar. Itabidi nijisomee zaidi.
Wengi huwa hawajui kwanini nchi inang'ang'ania jimbo fulani lisijitenge. Maamuzi ya watu/wakazi wa jimbo husika tu hayatoshi kuifanya sehemu imeguke kutoka katika muungano bali kuna vitu vingi vya kuangalia kama ulivyovitaja katika hiyo paragraph ya mwisho.
 
Hivi marekani akitaka kukopa nani anamkopesha kwa hali ya uchumi wa sasa

Naanza kuona Carrot na fimbo zinainyemelea marekani under Trump
 
Huyu mzee Trump hatamaliza awamu yake kabla hajaibua mnyukano wa kiaina, yaani kapiga simu Taiwan hata kabla hajatulia ofisini. Kitu ambacho Marekani hawajafanya kwa miaka 40. Tatizo yeye huwa kigeugeu na hatabiriki, mlichokubaliana wakati anaaga kwenda kulala sicho anachoamka nacho. Marekani wanalo, tena wakae mkao wa kujiandaa kwenye safari yenye matuta makubwa na mashimo.

Halafu yupo kwenye Twitter anawatukana Wachina balaa.

Trump picks Twitter fight with China
 
  • Thanks
Reactions: kui
Mkuu, kanda ya Kaskazini nao wakitaka kujitenga kama alivyoshauri Mh. Nassari nao tuwaache tu waunde hiyo Kaskazini Republic? Ukiruhusu hili basi hutakuwa na nchi na historia imeonyesha kuwa wakati mwingine "the masses" wala huwa hawajui wanachokitaka. Jimbo la Texas kule Marekani wamejaa kiburi cha mafuta na wameshatishia kujitenga mara nyingi lakini wanajua wakijaribu kufanya hivyo si ajabu wakala mkong'oto kutoka serikali kuu ya shirikisho.

Mara nyingi kunakuwa na sababu fungamano za kihistoria, kiuchumi, kijamii, kivita na kisiasa katika migogoro hii. Sina uhakika kama China na Taiwan ni sawa na hii ya Tanganyika na Zanzibar. Itabidi nijisomee zaidi.

Umeiweka sawa sana, natumai Mwanzi1 atajifunza kitu hapa kwanini Tanzania imegoma kuachia Zanzibar pamoja na kwamba wale wanataka huo uhuru, au kwanini sisi tumegomea kuachia Pwani isiwarudie Sultan wa Zanzibar kupitia MRC.
 
Huyu mzee Trump hatamaliza awamu yake kabla hajaibua mnyukano wa kiaina, yaani kapiga simu Taiwan hata kabla hajatulia ofisini. Kitu ambacho Marekani hawajafanya kwa miaka 40. Tatizo yeye huwa kigeugeu na hatabiriki, mlichokubaliana wakati anaaga kwenda kulala sicho anachoamka nacho. Marekani wanalo, tena wakae mkao wa kujiandaa kwenye safari yenye matuta makubwa na mashimo.

Halafu yupo kwenye Twitter anawatukana Wachina balaa.

Trump picks Twitter fight with China

Yaani utawala wake naona utakuwa wa roho mkononi. Sasa kama hii phone call na Taiwan ina maana he just didn't care about the relationship with China au ndio matokeo ya ku diss intelligence briefings wanazosema.

Na hata alivyo ongea na Pakistan kume raise concerns za kuitibua India.

Trump's Ignorant Call To Pakistan's Sharif May Send India An Unwelcome Message
 
Huyu mzee Trump hatamaliza awamu yake kabla hajaibua mnyukano wa kiaina, yaani kapiga simu Taiwan hata kabla hajatulia ofisini. Kitu ambacho Marekani hawajafanya kwa miaka 40. Tatizo yeye huwa kigeugeu na hatabiriki, mlichokubaliana wakati anaaga kwenda kulala sicho anachoamka nacho. Marekani wanalo, tena wakae mkao wa kujiandaa kwenye safari yenye matuta makubwa na mashimo.

Halafu yupo kwenye Twitter anawatukana Wachina balaa.

Trump picks Twitter fight with China

Hakupiga yeye.

Alipigiwa.

Halafu, kwani ubaya wa kuongea uko wapi?

Kwa nini watu wanaona ni sawa kuendeleza uhasama wa kuchuniana?

Kuna maelewano bila maongezi kweli?

Moja ya sababu za mifarakano hapa duniani ni kushindwa na kuacha kuongea na watu ambao hamuelewani nao.

Sasa rais wa Taiwan anampigia simu Trump [ she called him and not the other way round], kibaya ni kipi hapi?

Much ado about nothing.

Talking is good.
 
Trump siyo mnafiki sera zake ziko wazi mie binafsi naona hakufanya vibaya kuongea na kiongozi wa Taiwan .
Je serikali ya Rais Obama na waliomtangulia wameiuzia Taiwan silaha nyingi sana na mpaka sasa kuna meli za kivita za Marekani kwenye bahari ya pwani ya Taiwan kwa ajili ya kulinda Taiwan.
Je Donald Trump kuongea na simu na hawa viongozi waliomtangulia walioiuzia Taiwan silaha kali kali nani bora zaidi?
 
Trump siyo mnafiki sera zake ziko wazi mie binafsi naona hakufanya vibaya kuongea na kiongozi wa Taiwan .
Je serikali ya Rais Obama na waliomtangulia wameiuzia Taiwan silaha nyingi sana na mpaka sasa kuna meli za kivita za Marekani kwenye bahari ya pwani ya Taiwan kwa ajili ya kulinda Taiwan.

Huo ndo unafiki ambao siupendi.

Ni kweli Marekani huiuzia silaha nyingi tu Taiwan na ni stated policy ya Marekani kuilinda Taiwan kwa gharama yoyote ile.

Sasa rais wa Taiwan anampigia simu Trump kumpa pongezi kwa ushindi wake halafu watu wanalalamika.

Hivi ubaya hapo ni upi hasa?
 
Back
Top Bottom