True story; inasikitisha sana, nani alaumiwe?

Kima mdogo

JF-Expert Member
Sep 17, 2011
303
46
Wanandoa hawa walikutana na wakiwa na hali duni kimaisha, wakaoana na kujaliwa kupata mtoto 1 wakike. Kadiri siku zilivyoenda MUNGU akawajalia wakafanikiwa kimaisha na wanamiliki mali kadhaa. Miaka 7 ikapita mke akabeba mimba kwa bahati mbaya mimba ikatoka, akamweleza mama mkwe wake hapo ndo matatizo yalipoanza. Mama mkwe na Mume wakaanza kumsengenya kuwa hazai. Mama mkwe akafikia hatua ya kusema mwanae aoe mwanamke mwingine. Mke akawa analia na Mungu kila siku,Siku 1 mama mkwe akaja akamkuta mke huyo anaumwa akasema wala haumwi ni mamizimu ya huko kwao,huyu dada aliumia sana kwani hajui uchawi wala mizimu akamweleza mumewe maneno aliyoongea mama yake, mume kumuuliza mama yake akakataa katakata na kudai kuwa mwali wake kamsingizia ili asije kwa mwanae, kwa bahati nzuri Mke akapata ujauzito mume wake akaanza kumnyanyasa, kumtukana na kumnyima hela ya matibabu kwa shinikizo la mama yake kuwa alimsingizia, pia mama huyo akasema huyo mtoto hatazaliwa ng'o, kwa ufupi Mume na mama yake waliungana kumnyanyasa mwanamke(mke).

Mke yule akawa anaomba Mungu na kumwambia mumewe kuwa ni kweli mama yake amemwambia yy ni mchawi na anamauvimbe hazai lakini mume hakumwelewa na manyanyaso yakaendelea,mke akapata matatizo makubwa ikabidi madaktari wampasue wamtoe mtoto wa miez 7 kwani alinyongwa na kitovu karibu afe. Wiki 3 baada ya kujifungua mama mkwe akaja akamwambia niletee mtoto nimkague nataka niondoke,yule mke akashindwa kumpa mtoto akamwambia mumewe aje ampe yeye,mume hakuja na mama akaondoka,siku zikapita yule mume akamwambia mkewe kw hataki mtoto mke akamwambia atawajibia kumlea mwenyewe,ikabidi baba wa kijana aingilie kati na kumuonya kijana wake kuwa mama yk anapenda kuongea uongo na kukana hivyo asimnyanyase mke wake,kijana akakurupuka akaongea uongo kuwa mke wake amemuita mama yake mbwa,kwakweli mke yule aliumia sana akawa anafunga na kuomba Mungu,miez 2 baadae yule mama akaanza kuumwa kupima akakutwa na uvimbe kwenye kibofu na presha na sasa anaumwa sn,je nani anamakosa na nini kifanyike? Ushaur please
 
Wanandoa hawa walikutana na wakiwa na hali duni kimaisha, wakaoana na kujaliwa kupata mtoto 1 wakike,kadri siku zilivyoenda MUNGU akawajalia wakafanikiwa kimaisha na wanamiliki mali kadhaa,miaka 7 ikapita mke akabeba mimba kwa bahati mbaya mimba ikatoka, akamweleza mama mkwe wake hapo ndo matatizo yalipoanza,Mama mkwe na Mume wakaanza kumsengenya kuwa hazai,mama mkwe akafikia hatua ya kusema mwanae aoe mwanamke mwingine,Mke akawa analia na Mungu kila siku,Siku 1 mama mke akaja akamkuta mke huyo anaumwa akasema wala haumwi ni mamizimu ya huko kwao,huyu dada aliumia sana kwani hajui uchawi wala mizimu akamweleza mumewe maneno aliyoongea mama yake,mume kumuuliza mama yk akakataa katakata na kudai kuwa mwali wake kamsingizia ili asije kwa mwanae, kwa bahati nzuri Mke akapata ujauzito mume wake akaanza kumnyanyasa,kumtukana na kumnyima hela ya matibabu kwa shinikizo la mama yk kuwa alimsingizia, pia mama hy akasema hy mtoto hatazaliwa ng'o,kwa ufupi Mume na mama yk waliungana kumnyanyasa mwanamke(mke)
Ndo umehitimisha au? maana naona km inaeleaelea hewani!
 
  • Thanks
Reactions: Sal
endelea kujifunza tunga hadithi.. practice makes perfect.
 
  • Thanks
Reactions: Sal
Mama wakwe wanafuata nini kwenye nyumba za watoto wao.
Kusalimia sawa, lakini wakiweka kambi ndio matatizo kama hayo yanaibuka!
Loh! wazazi wasiingilie nyumba za watoto wao. Hapo ukute huyo bi Mkubwa
nyumba yake imemshinda!
 
haya makitu ya kuoa huku mkiendelea kusikiliza kila mnaloambiwa na mama zenu kuna siku watapangiwa zamu oh!huu ni upuuzi gani nausoma hapa,logic ya huyo mwanamke kutokuzaa inatoka wapi?na ananyimwa matunzo kwa sababu mama mkwe kasema asipewe na mwanaume nae dume zima na kengele chini kweli linafanya hivo!kisa cha kumtesa dada wa watu!ndo mana mabinti siku hizi hawataki hii ya habari ya kutafuta wote bora tu wanavukuta mshahenyeka wee ye aje atumbue tu!na mwisho wa siku ukianza kuleta habari za mama kasema hili mama kasema lile huyo anatimua!wanaume wa aina hii wamefanya wanawake wamekuwa makatili na wabinafsi sana kwenye mahusiano,sasa hapo mtu amejibana,wameinuka kiuchumi leo eti mchawi!pumbav jazz bend!
huyo dada sijui hata nimwambie nini maskini!sasa yuko wapi na ana hali gani?anafanya kazi?ana ndugu walio karibu?
 
Usiseme ya kutunga maana hapa jf hatujuani pia tuko wengi haya mambo yanatokea duniani tembea uyaone,sikiliza yapo haya kama bado mdogo kuwa uyaone sio magorofa.
 
hakyamungu patachimbika,ndo maana mi ctaki mtu wa kuanza nae maisha,bora nivikute tu
 
Wanandoa hawa walikutana na wakiwa na hali duni kimaisha, wakaoana na kujaliwa kupata mtoto 1 wakike,kadri siku zilivyoenda MUNGU akawajalia wakafanikiwa kimaisha na wanamiliki mali kadhaa,miaka 7 ikapita mke akabeba mimba kwa bahati mbaya mimba ikatoka, akamweleza mama mkwe wake hapo ndo matatizo yalipoanza,Mama mkwe na Mume wakaanza kumsengenya kuwa hazai,mama mkwe akafikia hatua ya kusema mwanae aoe mwanamke mwingine,Mke akawa analia na Mungu kila siku,Siku 1 mama mke akaja akamkuta mke huyo anaumwa akasema wala haumwi ni mamizimu ya huko kwao,huyu dada aliumia sana kwani hajui uchawi wala mizimu akamweleza mumewe maneno aliyoongea mama yake,mume kumuuliza mama yk akakataa katakata na kudai kuwa mwali wake kamsingizia ili asije kwa mwanae, kwa bahati nzuri Mke akapata ujauzito mume wake akaanza kumnyanyasa,kumtukana na kumnyima hela ya matibabu kwa shinikizo la mama yk kuwa alimsingizia, pia mama hy akasema hy mtoto hatazaliwa ng'o,kwa ufupi Mume na mama yk waliungana kumnyanyasa mwanamke(mke)

Uandishi huu unanifanya nimkumbuke mwalimu wa Kiswahili darasa la kwanza na la pili kwenye mdaya ya sehemu gani tuweke nukta, koma au alama ya kuuliza.
 
Uandishi huu unanifanya nimkumbuke mwalimu wa Kiswahili darasa la kwanza na la pili kwenye mdaya ya sehemu gani tuweke nukta, koma au alama ya kuuliza.

Umeongea kweli ndugu uandishi gani huu? halafu story yenyewe inahang tu, tafadhali mleta story jipange.
 
Ndo umehitimisha au? maana naona km inaeleaelea hewani!

Kwa kweli,nilijua niko peke yangu.....tulia basi uiandike vizuri,najua inakuuma,but tuangalie na sisi wasomaji wenzio......Huyo mama mkwe ni mkorofi tu..hata hivyo huyo dada asimuache mungu kabisa....
 
Hii imekaa kibongo muvi sana hata hitimisho lake halieleweki au ndo scrip zenyewe??
labda ni mimi sijui kuelezea ila ni ukweli kabisa na mama huyo kwa sasa ni mgonjwa sana na anatibiwa KCMC na wiki ijayo atafanyiwa operation, mume anahaha afanyaje mana alimtesa sana mke wake pamoja na kumtukana mama wa mke wake alipomsaidia mwanae kumpeleka hospitali alipokua anasumbuliwa na ujauzito na mumewe akagoma kumpeleka mkd hospitali.
 
Tuwapende wazazi na ndugu zetu ila inapokuja suala la ndoa na mke wako heshima ni lazima iwepo. Kwa ufupi ukitaka ndoa yako ife kifo cha asili ingiza hasa mama yako na dada zako. Baba wakwe hawana shida hata kidogo. Ndoa ni makubaliano ya watu wawili tu na kila mtu atamwacha baba yake na mama yake na mume utaambatana na mkeo, tazama mtakuwa mwili mmoja!!! Alichokiumba Mungu mwanadamu asitenganishe. Mungu hakukosea, alijua ndugu ni sumu ya ndoa.
 
Kwa kweli,nilijua niko peke yangu.....tulia basi uiandike vizuri,najua inakuuma,but tuangalie na sisi wasomaji wenzio......Huyo mama mkwe ni mkorofi tu..hata hivyo huyo dada asimuache mungu kabisa....
natumia simu hvy imebidi niandike mara 2,endelea kusoma utakuta hitimisho
 
Mke yule akawa anaomba Mungu na kumwambia mumewe kuwa ni kweli mama yake amemwambia yy ni mchawi na anamauvimbe hazai lakini mume hakumwelewa na manyanyaso yakaendelea,mke akapata matatizo makubwa ikabidi madaktari wampasue wamtoe mtoto wa miez 7 kwani alinyongwa na kitovu karibu afe. Wiki 3 baada ya kujifungua mama mkwe akaja akamwambia niletee mtoto nimkague nataka niondoke,yule mke akashindwa kumpa mtoto akamwambia mumewe aje ampe yeye,mume hakuja na mama akaondoka,siku zikapita yule mume akamwambia mkewe kw hataki mtoto mke akamwambia atawajibia kumlea mwenyewe,ikabidi baba wa kijana aingilie kati na kumuonya kijana wake kuwa mama yk anapenda kuongea uongo na kukana hivyo asimnyanyase mke wake,kijana akakurupuka akaongea uongo kuwa mke wake amemuita mama yake mbwa,kwakweli mke yule aliumia sana akawa anafunga na kuomba Mungu,miez 2 baadae yule mama akaanza kuumwa kupima akakutwa na uvimbe kwenye kibofu na presha na sasa anaumwa sn,
malipo ni hapa hapa duniani
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom