Tribute to Halima Mchuka: Alikuwa Mtu wa Watu!

Mkuu Ngongo ni kweli, ni kweli hatukua dini moja wala kabila moja na nilikaribishwa kwao.

Ni kweli heshima kwa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kuwezesha watu wa makabila tofauti kuishi pamoja kama ndugu na kusaidiana zaidi ya ndugu!.

Japo mimi ni Mkiristu wa RC, nilipokaribishwa nami nilimkaribisha rafiki Muislamu, Aboubakar Liongo na tuliishi kama ndugu. Wakati wa mwezi Mtukufu wenzangu walifunga, wakati wa kufuturu nilikaribishwa nikafikia wakati hata kula home naona noma mpaka nikaja kujikuta na mimi nafunga kiukweli na kufuturu kiukweli na hata mambo ya ujana kipindi cha mwezi Mtukufu ilikuwa no!.

Hawa wamekuwa nibzaidi ya ndugu, nilipopata ajali, Da Mwajuma alijitoa sana by then Halima alishapata stroke!.

Baada ya ajali yangu na matibabu ya Afrika Kusini na India kutoketa matokeo mazuri, Abou nae alinikaribisha Ujerumani kujaribu maana hao ni mabingwa wa tiba. Huu ni uthibitisho wa upendo wa dhati kwa sisi Watanzania bila kujali dini wala makabila yetu.

Asante Ngongo!.
Mayalla, hii imenigusa sana natamani watanzania wengi tungekuwa na upendo huo wa kutanguliza utanzania wetu na uafrika wetu badala ya udini. Pole sana, wape pole ndugu wengine, nakumbuka jinsi Mwalimu wangu wa Mass Communications pale SAUT alivyokuwa anamsifia Halima kwa ujasiri wake wa kutangaza mpira na hata juhudi zake kikazi maana kuna wakati mwalimu wangu huyo ali wahi kuwa Mkurugenzi wa Halima! Poleni sana.
 
Poleni sana kwa msiba mkubwa uliowafika. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi na awape nguvu na faraja wafiwa wakiwemo Mume, watoto, ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu kwao~AMEN
 
Mayalla, hii imenigusa sana natamani watanzania wengi tungekuwa na upendo huo wa kutanguliza utanzania wetu na uafrika wetu badala ya udini. Pole sana, wape pole ndugu wengine, nakumbuka jinsi Mwalimu wangu wa Mass Communications pale SAUT alivyokuwa anamsifia Halima kwa ujasiri wake wa kutangaza mpira na hata juhudi zake kikazi maana kuna wakati mwalimu wangu huyo ali wahi kuwa Mkurugenzi wa Halima! Poleni sana.
Kolero, asante, huyo atakuwa ni Nkwabi Ngwanakilala, batch yangu ya watangazaji 12, ndiyo ilikuwa batch ya mwisho ya David Wakati (RIP) akiwa mkurugenzi, ndipo akaingia Nkwabi, na ndiye aliyewaajiri akina Halima. Hata hiyo flat ya Ilala tuliokuwa tunakaa na Halima, ni Nkwabi aliidhinisha ofisi itulipie kodi, maisha wakati wa Nkwabi yalikuwa mazuri sana, baada tuu ya Mkwabi kuondoka, yale mambo mazuri yote yalisitishwa, hali iliyopelekea watangazaji zaidi ya 15 tukatimka!
 
Rip halima
tulikupenda sana sis lakini mungu alikupenda zaidi,,.namkumbuka zaidi akiwa anatangaza mpira wa yanga na reli akusita kueleza hisia zake binafsi alikuwa ni mohamed hussein mmachinga anafunga goli akanifurahisha kwa kupiga kelele ya gooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo kama dk 3 hivi na kusema sisi 3 wao sifuri..kila akicheza yanga akusita kujiita sisi kadhaa hata kama tunafungwa ...upendo wako autofikiwa kamwe tunamwomba mungu awape nguvu familia nzima kwa wakati huu mgumu waliokuwa nao ni wakati mzuri wa kumkumbuka halima kwa kutenda yale mema na mazuri aliokuwa akitenda ,halima alikuwa haujii ugomvi jamani unamkorofisha anasema samahani yeye unabaki na swali mmh imekuwaje huyo ndio halima mchuka
bwana ametoa bwana ametwaa
raha ya milele umpe e bwana na mwanga wa milele uangaziweeee weee halima upumzike kwa amani
aaaminaaa!!!!!!!!!!
 
Pole sana Pascal na ndg wote....namkumbuka sana marehemu kipindi cha RTD alivyokuwa mcheshi na mwenye upendo..alikuwa ananisaidia sana katika kuchagua nyimbo na kukirecord kipindi nilichokuwa nakitangaza cha NASACO....alikuwa ni mdada mwenye tabasamu wakati wote mfanyapo kazi nae....nakumbuka pia aliahidi wakati anajifungua mtt wake wa kiume kumpa jina la Yekini kwa heshima ya mshambuliaji hatari wa Nigeria enzi hizo aliefunga goli la kwanza la nchi hio kwenye World cup...Rashid Yekini......ama kweli chema hakidumu....upumzike kwa amani dada Halima Mchuka...bwana alitoa na bwana ametwaa...ameen.
 
Kolero, asante, huyo atakuwa ni Nkwabi Ngwanakilala, batch yangu ya watangazaji 12, ndiyo ilikuwa batch ya mwisho ya David Wakati (RIP) akiwa mkurugenzi, ndipo akaingia Nkwabi, na ndiye aliyewaajiri akina Halima. Hata hiyo flat ya Ilala tuliokuwa tunakaa na Halima, ni Nkwabi aliidhinisha ofisi itulipie kodi, maisha wakati wa Nkwabi yalikuwa mazuri sana, baada tuu ya Mkwabi kuondoka, yale mambo mazuri yote yalisitishwa, hali iliyopelekea watangazaji zaidi ya 15 tukatimka!
Mayalla ni kweli ni huyo na alikuwa anajisikia vizuri sana kusikia kijana wake akichapa kazi kivile na hasa kuwa Mtangazaji wa kike wa kwanza katika sehemu yetu hii kutangaza mpira na kwa uhakika vile, any way, Halima alikuwa role model kwa wasichana wa darasa langu pale Nkwabi alipokuwa anawahusia wasichana wakati wote ku-aim higher na kujaribu daima hata kile ambacho kinafikiriwa si uwezo tu peke yake unatakiwa bali uwe mwanaume ndipo ufanye.Nina uhakika Mwalimu wangu habari hizi amezipokea kwa masikitiko ila basi hatuna jinsi, ni kumshukuru Mungu kwa maisha ya Halima ya hapa duniani, tuendeleze yale tunayoyaweza tunayojifunza kutoka kwake.
 
Pole Mayalla kwa kuondokewa na mtu wako wa karibu. Lakini pia pile kwa mumewe na watoto wake. Mara zote huwa nasema kwamba vifo vinapotokea huwa ni ujumbe kamili kuwa nasi hatuna budi kujiandaa kwani kila nafsi lazima itaonja mauti na hakuna mtu anayeijua ile siku atakayokwapuliwa.
 
Poleni sana kwa msiba. Mwenyenzi Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki cha majonzi.

Inna lilah wa inna ilayhi raji'oon.
 
Update 3.
Leo asubuhi, Mwili wa Halima Mchuka, umeswaliwa katika msikiti wa Muhimbili na kuagwa na umati mkubwa wa waombolezaji ukiongozwa na rais Jakaya Kikwete, mkuu wa mkoa wa DSM, mawaziri, wabunge, likiwemo kundi kubwa la wanahabari.

Msafara kuelekea mazikoni makaburi ya Msasani ukafuatia na hatimaye kuzikwa na umati mkubwa wa watu.

Halima Mchuka pata pumziko la milele...
Amen.
 
Ametangulia tu, sote ndiyo hatma yetu bali njia ya kufikia alikoenda dada yetu Halima anaijua Mwenyezi Mungu PEKE YAKE. Ndio maana tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kila linalotokea, kwa kuwa kila linalompata binadamu Mungu anayo sababu ya kuachilia hilo. Marijani alishaimba kwamba Zuena alimtoka ilhali Marijani hakuwa na uwezo wa kumwambia Mungu amrudishie Zuena wake aliyeondokea Sarenda bridge kabla hawajasawazisha mambo kibao.

Dr Remi naye hakurudi nyuma alipoelza jinsi kifo asivyokuwa na huruma. Kama mtu ametoka kwa udongo atarudi kwa udongo, kwa udongo. Kilichobaki ni kutiana moyo tu, kujiweka sawa tayari kwa kupanda usafiri tusioujua siku yoyote kuwafuata wapendwa wetu huko wanakoenda na hawarudi tena. Kujiweka tayari ni kujipanga swasawa kama Rose Mhando anavyotuasa. Tuache kiburi cha uzima, kufa kupo. Familia ya Halima itiwe nguvu kwa kuambiwa ukweli kwamba sasa dada yetu hayupo tena nasi, kinachobakia ni kuendeleza mazuri yote aliyokuwa anahangaikia wakati wa uhai wake kama ambavyo kina Mayalla wanavyoyakumbuka machache sana, mabaya aliyoyafanya ni katika harakati ya kujitambulisha kuwa ni binadamu wa kawaida ambaye kukosea ni muhali.

May God, the ONLY GOD teach us how to overcome this terrible part of our life, being responsible and fearful to God.
 
pole sana kaka pascal na watanzania wote kwa ujumla.kwa wasikilizaji wa RTD tunawakumbuka vizuri wewe na dada Halima.Binafsi nawakumbuka wakati munatangaza kipindi cha DISCO SHOW kilichokuwa kinarushwa siku ya ijumaa kuanzia saa 5:15 hadi saa 5:45 usiku,hakika mulikuwa munatushika sana vijana.
MUNGU AILAZE ROHO YA HALIMA MCHUKA MAHALA PEMA PEPONI AMIN.
 
Halima huyu si alisoma shule ya Msingi Mpakani kule Manzese? Au Halima mchuka yule wamefanana jina na Halima Mchuka huyu marehemu. Mungu ailaze roho ya marehemu Mahala pema peponi!!

Yeye mbele siye nyuma!!
 
Paskali mayala poleni sana......
...ila sasa hivi katika taarifa ya habari naona umesema halima alikukaribisha kuishi nae japokuwa wewe hukuwa muislamu....mhh sikutegemea kama ungeweka hilo neno hapo.....ina maana hizi deen hawakai pamoja???
 
Paskali mayala poleni sana......
...ila sasa hivi katika taarifa ya habari naona umesema halima alikukaribisha kuishi nae japokuwa wewe hukuwa muislamu....mhh sikutegemea kama ungeweka hilo neno hapo.....ina maana hizi deen hawakai pamoja???
Aliyenikaribisha ni dada yake Halima, anaitwa Da Mwajuma. Ni kweli kukaribishwa kuishi sio upangaji, ni more than upangaji, japo sijafanya utafiti rasmi lakini fanya utafiti utagundua its not easy
 
Noted!


Mhe. Regia Mtema asante. Nilisoma TSJ na Bonga Bar ndio palikuwa outing yetu pale next to Priva!.

Mimi najihesabu ni mtoto wa Ilala tangu nasoma TSJ miaka yangu 10 ya ujana imekatikia Ilala.

Huyu Halima Mchuka na dada yake Mwajuma kwangu ni zaidi ya ndugu!

Huyu ni mwanamke wa shoka kama ulivyo wewe Mhe. Regia!.
 
20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom