Tribute to Halima Mchuka: Alikuwa Mtu wa Watu!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,466
113,551
Wanabodi
Leo saa 11:30 alfajiri nimepokea simu ya Da Mwajuma Mchuka kunijulisha kuhusu huu msiba!.

Hii ni thread ya Tribute kuhusu nilivyomfahamu marehemu, Halima Mchuka.
Kwanza jikumbushe sauti yake

Video kwa hisani ya Aboubakar Liongo.
Pia Baadhi ya Tasirwa mbalimbali za Halima Mchuka
Halima Mchuka 12.jpeg
Halima mchuka 11.jpeg


My Tribute To Halima Mchuka!

Halima Mchuka alipoajiriwa RTD, batch yangu ndiyo iliwatangulia!. Ilitokea tuu huyu dada tukawa tulielewana sana na alikuja kutokea kuwa ni mtu wangu wa karibu!.

Wakati huo akiishi na dada yake anayefanya kazi ATC, Mwajuma Mchuka sisi tukimwita kwa kifupi Da Mwajuma. Da Mwajuma alikuwa anamiliki flat ya familia mbili hapo Ilala Shariff Shamba nyumba ya pili kutoka lile ghorofa refu pale kituo cha Bungoni.

Wakati huo mimi nikiishi Mikocheni, kwa Wazazi, na kufuatia umbali kati ya RTD Pugu Rd (Sasa Nyerere Rd) na Mikocheni enzi hizo lazima upande mabasi matatu.
Kwanza utoke Mikocheni na upandishe kwa miguu njia ya TPDC mpaka kituo cha Maji Machafu (siku hizi Sayansi), pale ndio upande gari ya Mwenge Kariakoo ushuke Magomeni. Upande gari ya Ilala Drive-In ushuke Ilala Boma, upande gari ya Buguruni Kariakoo, ushuke Buguruni kisha utembee kwa miguu mpaka Tazara ndipo uingie ofisini jengo la BH!.

RTD walikuwa na basi moja la wafanyakazi route yangu basi hilo, halipiti, hivyo mimi nilikuwa ni mtu wa kuchelewa kufika kazini kila siku ambazo sikuwa zamu. Siku ukiwa zamu, unafuatwa na gari mpaka nyumbani.

Kufuatia kuchelewa huko, Halima Mchuka akanishauri kwanini nisihame nyumbani na kuhamia eneo la karibu na kazini?. Akasema kama vipi azungumze na dada yake, Da Mwajuma, aniruhusu nitumie chumba kimoja kwenye flat yao ambayo ni two in one, ina vyumba 4 vya kulala, na wao wako watatu, yeye, Halima Mchuka, dada yake Da Mwajuma Mchuka na mdogo wake Rehema, Rehema Mchuka!.

Da Mwajuma alikubali ombi la mdogo wake Halima hivyo mimi nikakaribishwa rasmi Ilala na huo ndio ukawa mwanzo wangu wa maisha ya kujitegemea!.

Asante sana Halima Mchuka kunifungulia milango ya maisha ya kujitegemea!.

Wakati nikiishi hapo yeye na Da Mwajuma walinichukulia kama mwanafamilia, sikuwahi kupika, kufanya usafi au kuosha vyombo, niliishi kama hotelini!. Asante sana Halima Mchuka kwa yote!.

Baada ya kipindi kifupi, Da Mwajuma alihamia kwenye nyumba yake Masaki hivyo kutuachia flat lote zima la two apartments za two bedrooms each, mimi na Halima, ndipo Halima akachukua upande wake na mimi upande wangu ambapo nami nikamkaribisha mtangazaji mwenzangu Aboubakar Liongo, tukiishi maisha ya ujana.

Tuliishi vizuri tuu akaanza Halima kuolewa na Nasoro Mkupama, na kuishi na mumewe kule upande wake, nikafutia mimi nikaoa hapo hapo familia ilipoanza kuwa kubwa, mimi nikahama na kumuchia Abou ambaye nae aliolea hapo hapo!.

Halima ameacha mume, watoto watatu, Amina, Yekini na Prince Naseem.

Thanks a Millions Halima Mchuka, Mungu Aiweke Roho yako mahala pema peponi.

RIP Halima Mchuka!.
Pasco.

Update 1.
Msiba wa Halima Mchuka, upo nyumbani kwa dada yake mkubwa Mwajuma Mchuka, Mbezi Beach nyuma ya maghorofa ya BOT.​
Mazishi ni kesho saa 5 asubuhi katika makaburi ya Msasani. Mwili utaswaliwa katika msikiti wa Msasani kabla ya swala ya Ijumaa.​
Chanzo cha kifo ni shinikizo la damu. Jana mchana alitangaza kipindi cha salaam za mchana TBC-Taifa na inasemekana alitangaza vizuri ajabu!. Kitu cha ajabu jana aliwatumia sms wanae wawili waliopo nchini, na kuwaambia wamsikilize akitangaza akawaambia na muda. Masikini kumbe ndio kama kuwaaga kiaina kwa kuwaambia waisikilize sauti yake kwa mara ya mwisho!. Mara baada ya kipindi ndipo pressure ikampanda, akakimbizwa pale hospitali ya Dar Group na baadae Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mauti yalipomkuta!.​

Update Two.
Mwili utaswaliwa msikiti wa Muhimbili saa 3:30 asubuhi na maziko yatafanyika makaburi ya Msasani.

Update 3.
Leo asubuhi, Mwili wa Halima Mchuka, umeswaliwa katika msikiti wa Muhimbili na kuagwa na umati mkubwa wa waombolezaji ukiongozwa na rais Jakaya Kikwete, mkuu wa mkoa wa DSM, mawaziri, wabunge, likiwemo kundi kubwa la wanahabari.

Msafara kuelekea mazikoni makaburi ya Msasani ukafuatia na hatimaye kuzikwa na umati mkubwa wa watu.

Halima Mchuka pata pumziko la milele...
Amen.
Final Update.

HALIMA M. MCHUKA (18 Mar.1967- 29 Dec. 2011)

Familia ya Mchuka wa Dar es Salaam, pamoja na ndugu wote walioko Miono na Kibindu-Bagamoyo, wanatoa shukrani za dhati kwa wote mlioshiriki kwa namna moja au nyingine katika kipindi kigumu cha msiba wa mpendwa wao, Halima Mohamed Mchuka uliotokea tarehe 29/12/2011 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kuzikwa tarehe 30/12/2011 katika makaburi ya Msasani Dar es Salaam.

Shukrani za pekee ziwaendee, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo,Mhe. Dkt.Emanuel Nchimbi, Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto, Mhe. Sofia Simba, Naibu Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo,Mhe. Dkt. Fenella Mukangara, Waheshimiwa wabunge wa Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam, IGP, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Mstahiki Meya wa Ilala.

Shukrani nyingine ziwaendee viongozi na wafanyakazi wa TBC wakiongozwa na M/Kiti wa Bodi ya TBC, Wilfred Nyachia na Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Clement Mshana, wafanyakazi wastaafu wa RTD, wafanyakazi wa kampuni ya Ndege Tanzania, Madaktari na wauguzi wa hospitali za Dar Group na Muhimbili, viongozi wa vyama vya michezo, waandishi wa habari na watangazaji wa vyombo mbalimbali vya habari, Uongozi wa CCM Wilaya ya Bagamoyo, BAMITA, majirani wa Karakata, Msasani, Mabibo na Mbezi, pamoja na ndugu, jamaa na marafiki wote wa familia ya MCHUKA wa ndani na nje ya nchi. Tunawaomba mpokee shukrani zetu za dhati kwa kutufariji kufuatia kifo cha HALIMA MCHUKA.

Arobaini ya Marehemu itafanyika Miono Bagamoyo siku ya Ijumaa Tarehe 3/02/2012 kuanzia saa 11:00 jioni na Hitma itasomwa Jumamosi ya Tarehe 04/02/2012 saa 3 :00 asubuhi.Nyote mnakaribishwa.

Kwa taarifa zaidi wasiliana na wanafamilia moja kwa moja au kupitia simu namba 0713477790 au 0784737253.Karibuni.


INNA LILLAH WAINNA ILAYHI RAAJIUN
 
Siamini kama ni makosa kukupa pole Pascal kwa msiba huu. Fikisha pole zangu kwa Da Mwajuma, Rehema, Mume na Watoto wa Marehemu pamoja na wanafamilia wote! Ni msiba mkubwa kwa kweli!
 
Pasco,

Pole kwa msiba wa Halima Mchuka, naamini kwa namna ulivyoishi naye umekuwa sehemu ya familia yao.

Mimi namkumbuka nikimsikia akirindima redioni RTD kwenye vipindi vya michezo na hatimaye akitangaza mpira wa miguu.

Ni mwanamke wa kwanza kupata kumsikia akiandaa vipindi vya michezo na kubwa kuliko yote alikuwa ni mwanamke pekee niliyepata kumsikia akitangaza mpira wa miguu "live" kutoka viwanjani. Mara ya mwisho kumsikia akitangaza mpira ilikuwa michuano ya kombe la tusker, wakati huo ikishirikisha vilabu vya Tanzania pekee.
 
Mimi nimesikia taarifa hizi alfajiri kwenye kipindi cha Kombora usingizi ukaishia hapo hapo, pole Pasco, Da Mwajuma na watangazaji wote wa TBC, hakika tutaimiss sana saut ya mwanadada huyu, nakumbuka jinsi walivyokuwa wanatangaza mpira na ndugu Ezekiel Malongo kwa kweli ilikuwa raha kuwasikiliza hata kama timu yako imefungwa bado ungetamani tu kuendelea kuwasikiliza.
 
Pasco.

Pole kwa msiba mzito.Baada ya kusoma bandiko lako mara moja nikapata picha Halima Mchuka alikuwa mtu wa namna gani.

Sina uhakika sana ila nahisi Halima Mchuka na wewe hamtoki mkoa mmoja wala si waumini wa dini moja kama ndivyo basi shukrani za mwanzo ziende kwa Baba wa Taifa letu changa Mwl J K Nyerere ambaye alijitahidi katika uongozi wake wote kutufanya waTanzania wamoja.Alipiga vita ukabila,alipiga vita udini vitu hivi viwili alifanikiwa sana na pengine ndiyo maana Da Mwajuma alikuwa mwepesi sana kukukaribisha Ilala Flat bila kujali kabila lako au dini yako aliutazama uTanzania wako.

Mkuu Pasco nimeanza mbali kidogo si bahati mbaya ila nimeona niwakumbushe viongozi wetu hasa wanasiasa wanaotafuta madaraka kwa msingi wa ukabila ama udini waache mara moja watanzania tumeishi na tunaishi kwa upendo yamkini mfano wako unawakilisha mifano mingi jinsi wananchi tusivyo na huu upuuzi wa ubaguzi.


Mkuu Pasco pole sana hakika umeondokewa na mtu muhimu sana katika maisha yako.
 
rip halima!
hujaelewa thread. hii sio Rip. by the way, niliwahi kumuona mara moja ila nilikuwa naipenda sana sauti yake akiwa anatangaza alikuwa na sauti nzuri, iliyojaa ucheshi na uchangamfu. Pumzika kwa amani maana sote mavumbini tutarudi.
 
Halima Mchuka,ni miongoni mwa Watangazaji walionivutia sana.RIP
Kumbe ndio maana nilikuwa nakuona Kanisani Msimbazi,Siku hizo nikiwa nasoma shule ya msingi Na sekondari.Nilikuwa nafurahi kukuona.Ulikuwa unakaa karibu Na Priva Mtema?
 
Nilimfahamu katikati ya miaka ya tisini wakati wa kurekodi vipindi vya idhaa ya biashara ambapo alikuwa anatangaza viopindi vya m ashirika na taasisi mbalimbali. Alifanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa kwani kuna wakati wa kurekodi vipindi hivyo,ilitokea wawakilishi wa taasisi na mashirika wakawa wanamtegemea yeye kuwapangia ratiba ya kutumia studio moja kila mwakilishi kwa wakati wake bila kusababisha misuguano miongoni mwao. Alikuwa na PR nzuri kwao.
 
Siamini kama ni makosa kukupa pole Pascal kwa msiba huu. Fikisha pole zangu kwa Da Mwajuma, Rehema, Mume na Watoto wa Marehemu pamoja na wanafamilia wote! Ni msiba mkubwa kwa kweli!
Kombo, sio makosa, thanks pole nitazifikisha na update nitawapa!.
thanks
 
Halima Mchuka,ni miongoni mwa Watangazaji walionivutia sana.RIP
Kumbe ndio maana nilikuwa nakuona Kanisani Msimbazi,Siku hizo nikiwa nasoma shule ya msingi Na sekondari.Nilikuwa nafurahi kukuona.Ulikuwa unakaa karibu Na Priva Mtema?
Mhe. Regia Mtema asante. Nilisoma TSJ na Bonga Bar ndio palikuwa outing yetu pale next to Priva!.

Mimi najihesabu ni mtoto wa Ilala tangu nasoma TSJ miaka yangu 10 ya ujana imekatikia Ilala.

Huyu Halima Mchuka na dada yake Mwajuma kwangu ni zaidi ya ndugu!

Huyu ni mwanamke wa shoka kama ulivyo wewe Mhe. Regia!.
 
Asante kwa habari nzuri. Mungu amlaze pema peponi.

Kwa kweli sielewi kwanini unalazimisha iwe tribute tuu acha wa RIP waweke sababu sio wote tunamjua mie simfahamu

Mie sioni y kucontrol thread wakati ni mod ndie mkuu. Ni msiba hakuna haja ya kutoa onyo, just let it flow

Poleni wafiwa

May she RIP
 
Back
Top Bottom