Treni za Mwakyembe

bado wajichanganya majibu nshakupa
ticketi unaweza kukata kwa siku au wiki au mwezi
kama huna hakuna kupanda treni hatuko katika dunia ya ujamaa kwa sasa
huwezi kuchukulia tatizo la mahali fulani ukalinganisha na mahali pengine
kujaribu kutuhubutu jambo ndio kinachotusumbua watanzania hatutaki kuthubutu bali kuwa na visingizio vingi
kama wewe.
wewe ndio unapotosha hoja, mimi sijapinga ila nimetoa changa moto nipinge jambo zuri kama hilo kwa lengo gani?
hayo yote uliyoandika yapo sijui ticket machine reader kivukoni ferry ipo iliwekwa sasa kaangalie kama inatumika na magari na watu bado wanajichanganya, nenda Ubungo bus terminal kuna milango iliwekwa ya kuzunguka lengo likiwa ni kuruhusu mtu mmoja kwa kwa wakati lakini wameifunga na kamba na haizunguki na watu wote wanagombania kupita na wengine bila tiketi na vyote hivyo chini ya wizara hiyo hiyo kama sikosei sasa kwa nini nisihoji ufanisi wa hiyo treni?

 
Hiyo sio hoja ya msingi sana ya kudhani treni likianza halitakuwa na ufanisi
acha lianze tutaona mafanikio yake
wengi tunalisuburi kwa hamu sana
Nafikiri una uwezo mkubwa sana wa uelewa tofauti na watu wengi sana hapa, wanaongea vitu kama vile wako sayari nyingine na wanashabikia vitu bila kufanya tathimini ya kutosha hivyo vitu vyote Dar vipo mfano kituo cha mabasi Ubungo kuna milango wa kuzunguka (Revolving door) iliwekwa (kwa pesa nyingi!) ili mtu mmoja mmoja aingie nakuzuia chaos, kaangalie sasa hivi wameufunga na kamba na hauzunguki, ukienda feri ambayo wamajenga kwamba unanunua ticketi kuna sehemu unapanchi geti linafungunguka unapita (mtu mmoja mmoja) lakini hawatumii matokeo yake wameweka mtu, na kuna chaos ya ajabu mpaka magari yanatumbukia baharini, sasa vitu kama hivi kwa nini niamini kwamba hii treni itakuwa tofauti? kama wizara ya uchukuzi wameshindwa kufanya kivuko kiwe efficient wataweza treni?

 
Back
Top Bottom