Yote anayoyasema Rais J.P.M. yanawezekana kwa asilimia 70. Kinachotusumbua watanzania ni hali ya kujiona hatutaweza na kujiviisha umasikini kwa kufuata yale tu tulioambiwa na waliotutangulia na hasa wakoloni.Utasikia mtanzania anasema wazi wazi hata kabla hajatafakari kuwa: "sisi ngozi nyeusi hatuna tunaloliweza" au "sisi watanzania bado sana" hii utaisikia hata katika mambo ambayo tunaweza kufanya wenyewe.Ukiangalia maliasilia ya nchi hii ambazo hazijatumika kabisa kuzalisha mali ni nyingi kuliko zile tunazozitumia hivi sasa tena kwa kiwango cha chini kabisa.Mali zetu nyingi hazisimamiwi vizuri na hivyo kuwafaidisha wachache waliominiwa kuziendesha.Ufisadi,uzembe, kutokujali, masihara ndio yanayotugharimu na kushindwa kupiga hatua. Mimi naamini sana kuwa iwapo JPM ataendelea hivi bila kulegeza kamba, na hasa akizidisha usimamizi zaidi na kuwaadhibu wazembe wachache wanaotuharibia kama mchwa,nathubutu kusema miaka yake mitano ikiisha tutakuwa na maendeleo makubwa ambayo wengi wanayaona kama hayawezekani.
Miaka inazd kwenda kwan rais tangu ateuliwe anamiaka mingap madarakan,?ukpata jibu jiulze n mangap katekleza kwa muda aliokaa madarakn?ahadi zinaendelea sijui kampeni hazijaisha bado? tuliambiwa fly over ikaja njia sita ikaja reli ya standard gauge,zote zimebaki kwenye makaratasi yao na miaka inakwenda kasi tu
Saaana....Watu wana hofu tu. Kujenga treni ya umeme haichukui muda mrefu siyo gharama kubwa. Serikali inaweza jenga under PPP law. Ulaya ni vitu vya kawaida. You must think big.Nampongeza JPM ktk hili. It is very possible kutekelezwa. Maendeleo ni kuthubutu(to dare). Ukiwa na hofu huwezifanya jambo la maendeleo.
Umeme upo wapi bana?
Hata likijengwa ni kwa ajili ya kujitangaza kisiasa tu si kutatua matatizo ya wananchi.
Amini usiamini, nimeomba niingiziwe umeme katika mashine ya kusaga. Kila kitu kimeshapita na nimeshalipia, leo hii ni mwezi wa pili sijaingiziwa umeme, kisa eti waya za 3 phase hazipo. Naendelea kusubiri. Pazuri hapo!!!!!!!!