Treni ya kati kutoanza safari leo

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Treni ya kati kutoanza safari leo


Na Mwandishi Wetu

SAFARI za treni ya kati zilizokuwa zimepangwa kuanza leo zimesogezwa mbele hadi Ijumaa Januari 21, 2011 kutokana na 'kazi ngumu ya kukarabati daraja' lililopo katika stesheni za Bahi na Kintinku.Taarifa ya TRL jana ilisema kuwa
kutokana mkondo wa mto Bububu kuendelea kutririsha maji mengi, kazi hiyo imekuwa ngumu, lakini tathmini za sasa za wahandisi ujenzi na wataalamu wa Reli zinakadiria kazi kazi hiyo kukamilika Alhamisi.

"Kufuatia makisio hayo mapya ya huduma ya abiria kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma iliyopangwa awali kufanyika Januari 17, 2011 imefutwa na abiria watarejeshewa nauli zao kuanzia Jumatatu Januari 17, 2011 katika stesheni husika walikokatia tiketi za safari," ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Ofisi ya Uhusiano Kampuni ykwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Hundi Lal Chaudhary, iliongeza kuwa hivi sasa kazi ya ukarabati zinaendelea kwa saa 24, ili lengo la kufungua njia kabla ya Januari 21, 2011 lifikiwe.

Wakati huo huo, haduma maalumu ya usafiri wa abiria wa treni itaondoka Tabora leo jioni kwenda Kigoma na kugeuza Alhamisi saa 11 jioni kurejea Dar es Salaam. Uongozi wa TRL umewataka wadau na wananchi kwa ujumla kuwa na uvumilivu wakati kampuni inafanya kila njia kurejesha huduma zake katika hali ya kawaida.

 
Under CCM machinations, nothing seems to work amicably.......................
 
TRL yatoa ratiba mpya ya treni http://www.mwananchi.co.tz/componen...sLXlhdG9hLXJhdGliYS1tcHlhLXlhLXRyZW5pLmh0bWw=
Monday, 17 January 2011 09:48


Mussa Mkama

SAFARI za Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) zilizokuwa zianze leo zimekwama hadi Ijumaa kwa madai kuwa ukarabati wa daraja haujakamilika na kwamba abiria wote watarejeshewa nauli zao leo katika stesheni husika walikokatia tiketi.

Taarifa iliyosambazwa kwenye vyombo vya habari na ofisa habari wa kampuni hiyo kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji Hundi Lal Chaudhary inasema kuwa uamuzi wa kusogeza mbele siku ya kufungua njia ya reli inatokana na kutokamilika kwa ukarabati wa daraja lililopo katikati ya stesheni za Bahi na Kintinku kufuatia kuendelea kutiririka kwa maji mengi kutoka mkondo wa mto Bububu.

Taarifa ilisema tathmini za Wahandisi Ujenzi na wataalamu wa Reli zinakadiria kazi ya ukarabati huo kuwa itakamilika Alhamisi na itaanza kutoa huduma kuanzia Ijumaa wiki hii.

"Tathmini za Wahandisi Ujenzi na wataalamu wa Reli zinakadiria kazi ya ukarabati huo kuwa itakamilika Januari 20, mwaka huu, kufuatia makisio hayo mapya, huduma ya treni la abiria kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma iliyopangwa awali kufanyika Januari 17, mwaka huu, imefutwa na abiria watarejeshewa nauli zao katika stesheni husika walikokatia tiketi," ilisema taarifa hiyo.

Iliongeza kuwa huduma maalumu ya usafiri wa abiria ya treni itaondoka Tabora siku ya Jumatatu (leo) jioni, kwenda Kigoma na kugeuza siku ya Alhamisi Januari 20, mwaka huu saa 11 jioni kurejea Dar es Salaam.

Taarifa hiyo ilisema kazi ya ukarabati inaendelea kwa saa 24 lengo likiwa ni kufungua njia kabla ya Januari 21, mwaka huu.

"Uongozi wa kampuni hiyo unawataka wadau na wananchi wote kwa ujumla kuwa na uvumilivu katika wakati huo mgumu ambapo kampuni inafanya kila njia kurejesha huduma zake katika hali ya kawaida", ilisema sehemu ya taarifa.
 
Back
Top Bottom