Treni laishiwa mafuta katikati ya pori

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,775
3,610
treni.jpg

Katika hali ya kushangaza treni la Kampuni ya Reli (TRL) iliyokuwa ikitoka Mpanda kuelekea Tabora Machi 23 mwaka huu, iliishiwa wese (mafuta) katikati ya pori na kuwaweka roho juu abiria waliokuwa wakisafiri.

Akizungumzia tukio hilo Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Athumani Mfutakamba alisema kitendo kilichofanyika ni cha kinyama na hakikubaliki katika utendaji wa kazi za shirika hilo na kwamba wamejipanga kuhakikisha matatizo kama hayo hayatokei tena.

Alisema kwamba haiingii akilini treni kuishiwa mafuta njiani wakati bajeti ya mafuta inajulikana.

Tayari watumisho watatu akiwemo dereva wa treni wa Kampuni ya Reli (TRL), wamesimamishwa kazi katika sakata la kusababisha treni ya abiria kusimama porini baada ya kuishiwa mafuta.

Mhandisi wa TRL, Muungani Kaupunda alithibitisha hilo.

E-mail: meezy@youngmaster.co.tz
 
Haki za abiri?!, wamelipwa fidia ya kuwekwa roho juu na kucheleweshwa kufika wanakoenda?!
 
umelala usingizi wa namna gani? tukio la 23rd ndo unaibuka nayo 30th?
 
Nchi hii inavyokwenda utadhani ni kambi ya mafunzo ya 'wanamazingaombwe' kila kituko kisicho patkana popote duniani hapa utakipata. Tusubiri ndege ya atc kuishiwa wese angani
 
Nakuunga mkono: ona maajabu haya, gari la rais kukataa kuwaka baada ya kuweka mafuta machafu; rais kulalamika kuwa bank ya CRDB sasa siyo ya ushirika tena hivyo inabidi kuunda bank nyingine itakayo jihusisha na ushirika; rais kuwashitaki madaktari waliogoma kwa wazee wa dsm; nchi kutokuwa na ma-DC kwa miaka 2 nk.........
 
Haki za abiri?!, wamelipwa fidia ya kuwekwa roho juu na kucheleweshwa kufika wanakoenda?!

sio kwa tanzania mkuu fidia ndo hiyo ya kusimamisha watu kazi na kuwarudisha kwa madai ushahidi hautoshi
 
Ingekua china wangekua ndugu washawazika mda mrefu,kwakua ni tz basi hz movie zipo nyingi sana,hayo
Maneno ya naibi waziri ni soundtrak tu
 
Back
Top Bottom