TRAWU yaitaka TAZARA kusimamisha shughuli za treni kwa sababu za kiusalama

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,710
2,226
Trawu yaibua mapya Tazara
Na Mwandishi wetu
5th March 2012
Waziri wa Uchukuzi Omari Nundu
Chama cha Wafanyakazi wa Reli Nchini (Trawu), kimemtaka Waziri wa Uchukuzi Omari Nundu kutoyachukulia matatizo ya Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (Tazara) kuwa ni ya kisiasa na kuwa ni mepesi, bali achukue mikakati zaidi kwa nia ya kuleta mabadiliko.
Aidha Trawu, imeitaka Serikali kuwafukuza kazi mara moja Mkurugenzi Mtendaji, Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Meneja wa Fedha, Meneja Mipango, Meneja wa Masoko, Meneja Ugavi, Mhandisi Mitambo, Meneja Usafirishaji pamoja na Meneja Teknohama na Habari kwa kile ilichodai kuwa wameshindwa kuiendesha Tazara kama kampuni.
Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Katibu wa chama hicho, Erasto Kihwele alisema kuwa Trawu kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya Waziri, aliyotoa hivi karibuni kwa vyombo vya habari juu ya matatizo ya Tazara, ambayo yamekuwepo kwa zaidi ya miaka 10 sasa.
Kihwele alisema matatizo yote yalikabidhiwa kwa Waziri huyo alipotembelea kwenye Ofisi za Shirika hilo Aprili 2011 na aliahidi kuwa angerudi Tazara ndani ya mwezi mmoja ili kuona mabadiliko na maendeleo, jambo ambalo hajalifanya kwa mwaka mmoja sasa wakati hali ya shirika hilo ikizidi kuwa mbaya.
Aliyataja baadhi ya matatizo ya shirika hilo kuwa ni pamoja na kutokulipwa kwa wakati mishahara ya wafanyakazi, shirika kushindwa kununua mafuta kwa ajili ya shughuli za kiuendeshaji, mizani mibovu, mikataba mibovu isiyo na tija, kushindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi NSSF, pamoja na kushindwa kulipa pensheni kwa wastaafu.
"Pamoja na maelezo mazuri ya Waziri, kwa vyombo vya habari, lakini hayaonyeshi ufumbuzi wa kudumu wa matatizo hayo, chama kinahesabu maelezo hayo kama zima moto, kitu ambacho hatukubaliani nacho," alisema.
Kihwele aliongeza kuwa wafanyakazi wa Tazara wanataka mishahara yao kuanzia sasa ilipwe kwa ukamilifu ili michango ya Hifadhi ya jamii iweze kupelekwa kunakostahili na kwa wakati, hali itakayowawezesha wafanyakazi kupata mafao yao yanayotolewa na mifuko hiyo, kama vile matibabu, mazishi, uzazi na kuumia kazini.
Aidha Trawu imelitaka shirika hilo kusimamisha huduma ya usafiri wa treni kwa sababu za kiusalama
MY TAKE
Kama watendaji wanataka shirika lisimamishe shughuli zake kwa sababu ya usalama na izo shughuli bado zaendelea.Nundu huoni kuwa unaweza sababisha ajari kama ya Dodoma au mumeona watz wamezoea kufa kwa halaiki.
Kaeni na hao wafanyakazi mtatue kero zao ingawa that statement it may be accompanied with sabotage if not worked upon!
 
Back
Top Bottom