Trapped in the closet= tuko wangapi? Tulizana

Mkurabitambo

JF-Expert Member
Feb 3, 2010
230
57
katika jamii ambayo gonjwa la ukimwi limekuwa tishio tujaribu kurekebisha tabia zetu kwani mnyororo wa VVU ni mkubwa kuukadilia.
kama ni mfuatiliaji itafute nyimbo ya Rkelly iitwayo Trapped in closet uone jisi chain ya VVU ilivyo,au kwa urahisi sikiliza tangazo la TACAIDS liitwalo Tulizana utaelewa na maanisha nini..
UKIMWI UPO NA UNAUA..


 
Zile nyimbo moma. Yaani kama movie. Balaa lilianza pale simu ilipoita alipokuwa amejificha kabatini.
 
Zile nyimbo moma. Yaani kama movie. Balaa lilianza pale simu ilipoita alipokuwa amejificha kabatini. Balaa likazaa balaa juu ya balaa. Yaani mpaka Trafic anakukamata na kukupiga fine wakati katoka kumkunja mkeo. Kweli ile chain ilikuwa ya kufa mtu.
 
acheni mbwe mbwe tokomezeni vifo vya wajawazito, watoto wachanga na malaria, ukimwi sio ishu ni mtaji wa matajiri tu, boda boda zinaua nguvu kazi ya tanzania kuliko ukimwi now days, change ya focus ninyi mnaotajirika kwa fedha za ukimwi
 
Ukimwi umekua mradi wa watu matajili kusaidia waathirika na sio kutoa ushauri ktk jamii namna kujikinga.
 
Kwa anaelewa haisumbui, TACAIDS imebakia kuunda maneno kama wanasiasa, leo tuko wangapi, kesho wataunda mwingine, yote hiyo ni kampeni ya kuombea fedha kwa wafadhili ili waendelee kula kwa masemina yao kibao, matamasha kibao huku waathirika wanaendelea kukosa hata pesa ya chakula.

Wanatapatapa tu si umesikia wajomba zao wa USA wamechomoa!
 
Back
Top Bottom