Tragical Errors and Miscalulation of CCJ!

Pasco, it was never a joke. It is not an easy thing to start a party simply by saying tunataka uing'oa CCM. Chama ni lazima kiwe na taswira ya namna yake ambayo itakitofautisha na na wengine wote.

Wengi hapa wanakimbilia kusema kuwa na Itikadi na Sera si za msingi, wanasahau kuwa bila kuwa na utambulisho na imani ya kinachoeleweka, si rahisi kujenga political base kwa Tanzania. Ama kila mtu analenga kwenye short term goals, kuing'oa CCM, lakini hawafikirii beyond kuing'oa CCM na kitakachotokea baada ya kuing'oa CCM!

Kama miaka 20 ya Upinzani haijatupa funzo la kujifunza na kuelewa kuwa bila kuwa na Itikadi na Sera zinazoeleweka, kamwe huwezi kuwa na mvuto au uwezo wa kuleta mshikamano wa kuiondoa CCM.

Leo hii kila mwaka wa uchaguzi, vyama viliyoko vinapigana vikumbo kugombania nani ana mgombea maarufu zaidi ili kuchukua jimbo au urais. Wamekaa chini mara kadhaa kutaka kujenga ushirika, lakini wameuvunja na kununiana.

Turudi pale ilipoanzishwa NCCR, kila mtu alikuwa huko, lakini kutokana na kila mtu kuwa na fikra na mtazamo wake na badala ya kujenga mfumo, itikadi, sera na taswira moja na wote kushikamana, chama kika sambaratika!

Leo hii hatuwezi kuing'oa CCM ambayo inajiita Chama cha Kijamaa na kukimbilia kuingia madarakani kumfunga Mkapa, Rostam, Lowassa au mafisadi, kisa wananchi tumechoka kunyanyaswa na kuonewa.

Hatuwezi kuwa na uimara ilhali CCM bado ni chama kilichojijenga kisera na kiitikadi ndani ya Watanzania na ni rahisi sana kwa CCM kurudi madarakani katika muda mfupi sana na kuwafanya Wapinzani waonekane wajinga machoni pa Watanzania.

Kuiangusha CCM, si watu wawili ambao wanaisumbua nchi, inapaswa kuingia na nguvu za kuhakikisha CCM inashindwa kihoja, kisera na kiitikadi. Leo tukishawafunga kina Lowassa je tutakifuta CCM usajili au kudai tukitaifishie mali zake kukivunja nguvu? Kama kuna mawazo kama hayo ni dhahiri basi sisi hatuna tofauti na CCM.

Wanapodai CCM inawenyewe, ingawa kwa dhihaka tunawatukana kuwa ni mafisadi, lakini wenye CCM bado ni wananchi na kuna kundi kubwa sana la wafuasi wa CCM ambao ni safi na ni rahisi kwa wao kujipukut mavumbi baada ya kuanguka na kujijenga upya na kuwa Chama mbadala!

Tusikimbilie kuing'oa CCM au kukimbilia Ikulu kisa eti tutaondoa onyonge wa Mtanzania kwa siku mmoja! Tusisahau kuwa iwehe vile, katika miaka 25 ijayo, CCM inauwezo wa kuwa na asilimia 45-70 ya viti vya Bunge, na hiki ni chama kimoja tu, tofauti na vyama vingine ambavyo vitapaswa kujikusanya viti viwili vitatu ili vipate umoja wenye nguvu huku kati yao hawaaminiani!

Kule kwenye hoja ya Mtei, Shalom kanipa majibu kuwa mwaka huu, kati ya viti karibu 400 vya ubunge, CHADEMA inatarajia kupata viti 70, ambayo ni asilimia 17, CUF nao labda watapata idadi hiyo hiyo hivyo kuwafanya jumla yao kua kiwango kidogo sana juu ya theluthi moja.

HIvyo miswaada yote ikija Bungeni, bado CCM itaipitisha na kuiburuza, na tusisahau kuwa CCM imeshaanza kujianda kujisuka upya na kujijenga kwa uchaguzi wa 2015 na si huu wa mwaka huu tena.

Wakati nimeandika PPPT, nilitamka wazi lengo si kukimbilia uchaguzi mkuu au kuwa na malengo ya muda mfupi ambayo hayana matunda ya kudumu bali ni kujenga chama imara ambacho kitaanzia kwenye vijijiji, na kuishi na Watanzania katika kila ngazi na kadri matunda ya mahusiano yetu yatakavyokuwa yakiongezeka, ndivyo basi uimara utakapoongezeka na kutufikisha kwenye lengo la kuomba dhamana ya kuwaongoza Watanzania.

CCM inayoogopa CCJ, si Chama bali ni kundi la watu wachafu waliokichafua Chama kwa matakwa binafsi na kukitumia Chama na dhamana ya kuongoza nchi kwa maslahi binafsi na hivyo kuendekeza Uhujumu na utawala mbovu.

Sisi tunapaswa kuwaogopa wale CCM makini ambao wanajijenga kimywa kimya kuchukua hatamu za Chama chao, hawa ni wale vijana kati ya miaka 18-45, ambao wamesha kula yamini ya Ujamaa na Kujitegemea na si hawa wa miaka 50-80 ambao wameshaloea utamu wa madaraka na wameshindwa kumkomboa Mtanzania kutoka Umasikini, Ujinga na Maradhi.

It is all about strategy na hili ni wazi kama watu kam CHADEMA wakiwaachia kina Mnyika na Zitto ambao ni vijana wakawa Sauti kuu na nguvu ya Chama, itakuwa ni rahisi sana kwa CHADEMA na hata CUF kuweza kupata nguvu kubwa na ufuasi wa kweli kwenye sanduku la kura.


Rev thanks kwa maelezo yako lakini mimi natatizo dogo tu katika hili jambo la CCM unayoiongelea hasa hapo kwenye red colour; hivi CCM bado ni CCM ya 1977 pale ilipo anzishwa kiitikadi au ndo imebaki kama ilivyo leo CRDB bank kwamba si ile iliyoanzishwa by then kwaajili ya rural development ila imebakia nembo tu kwaajili ya kuvuta wateja? Why I ask this kama CCM bado kipo kiitikadi kama ilivyo kuwa 1977 yaani zile alama mbili ya jembe na nyundo kwa maana halisi basi I dont need CCJ lakini mimi ninachokiona CCM is more of the last words in red colour na wana waandaa hao unaowaita vijana kukomaza hiyo itikadi yao ndo maana nashindwa kuitetea CCM popote pale kama ambavyo ningependa kufanya hivyo IFF it would have been that of 1977 kiitikadi.
 
hivi CCM bado ni CCM ya 1977 pale ilipo anzishwa kiitikadi

Unaulizia CCM ama TANU? Kuna ndugu yangu mmoja wakale alikuwa akijadiliana na ndugu yangu mwengine wasasa. Nilichoweza kugundua katika ubishani wao ni kuwa mmoja alikuwa akiongelea TANU akidhani ndio CCM na mwengine alikuwa akiongelea CCM ambayo siyo ile TANU ya ndugu yangu wakale.....

omarilyas
 
Dadaangu Felister,

CCM ya sasa ya kina Lowassa, Shein, Karume, Magufuli ni CCM mpito, ukiangalia sana hawa ndio wale walioandamana kuliunga Azimio la Arusha, wakajifanya Wajamaa na kisha wakakutana Zanzibar 1992 na kugeuka kuwa Mabepari!

Vijana wa CCM, wao hata kama itabidi wafanyie Katiba ya CCM marekebisho na kuondoa neno ujamaa, hawa wamedhamiria kung'oa na kufuta madhambi ya hawa CCM mpito.

Majuzi nilimuuliza Mzee Mwanakijiji, kama anakumbuka mwaka 1984 palipotokea vurugu za Zanzibar zilizomg'oa Jumbe madarakani. Kulikuwa na edition ya jarida la Africa Now ambalo lilionyesha mgawanyiko wa kiitikadi ndani ya CCM ambapo kulikuwa na hard liners kama Seuf Khatibu, Kingunge, Getrude, Nassor Moyo, Paul wa Sozigwa na wengine ambao nimewasahau majina.

Lakini turudi kwa hawa watatu wa kwanza, Seif Khatib, Kingunge na Mongella. Leo hii hawa si hardliners, bali wamegeuka kwa matajiri lakini wanaendelea kuwaimbia Wananchi vumilieni maisha kwa kuwa nchi kubwa zinatunyanyasa.

Sasa kundi jipya la CCM, ni vijana wa leo, wanaelewa kinachotokea duniani na zaidi wana mtazamo na fikra tofauti na wapita njia. Ingawa si rahisi kuwaamini, lakini hawa wana kiu ya kutimiliza lile alilodhamiria Mwalimu Nyerere, la kuleta maendeleo kwa Taifa, kuondoa Ujinga, Umasikini na Maradhi.

Wanaweza wasiwe Wajamaa wa mwaka 1967 au 1977, lakini watakuwa ni damu yenye chachu mpya yenye Uzalendo na kuona uchungu kwa nchi yao.

Wengi wettu tulitegemea mabadiliko haya yangeanza na Kikwete, lakini tukajisahau kuwa yeye alishakuwa ndani ya CCM mpito siku nyingi!

CCM ya vijana itajiandaa kushindana na wengine kutoka CUF, CHADEMA, TLP, NCCR pindi safu za hawa Wazee wa mpito zitakapomalizika, na hii si mbali sana ndio maana unawaona kina Nape na Mnyika wakiamka, kina Serukamba na Zitto wakijitutumua na wengine wengi.

Vijana katika kila chama ni wazi inabidi waanze kushika hatamu, wazee wamepitwa na nyakati na ni heri legacy yao iwe ni kwenye busara, ushauri na kupatanisha na si kuongoza au kufanya kazi. Watupishe sisi vijana, tuko tayari, wang'atuke!
 
Rev.Kishoka,
Mkuu nadhani bado wanipeleka ambako mimi siko kabisa. Swala zima la hoja hii linahusu zaidi CCJ na sio Chadema hawa tumejaribu sana kuwafahamisha mengi ya msingi lakini kutokana na sababu zao wameshindwa kuyatekeleza. At least walikuja na sababu zao na hakika Dr.Slaa, Zitto, Mzee Mtei na hata Mbowe wamekuwa hapa wakijibu maswali mengi sana toka wakati ule.

Na katika kuchambua mchele toka ktk pumba tuligundua kwamba hata ndani ya Chadema wenyewe kuna mvutano, hawakuwa huru kuchukua ushauri usiofungamana na itikadi yao.. may think itikadi was a problem..hivyo hata walipokutana kuweka muafaka na vyama vingine ambavyo pia vilikuwa na mvutano walishindwa kuunda kitu kimoja..

Majibu yote anayojibu Mwanakijiji leo ni yale yale niliyoyasikia toka kwa Chadema - itikadi itikadi...lakini baada ya muda wao walikuja kubaliana Muafaka baina ya vyama likaingia swala la Uwakilishi hapo tena ngoma mpya ikazuka hadi kila chama kikachukua mkondo wake. Hakika tatizo halikuwa itikadi bali viongozi wenyewe hawakutaka kuwepo muungano kwa sababu ya maslahi yao - Ubinafi.

Kwa hiyo sisi kama wananchi tumejifunza nini?.. kwanza viongozi wa vyama hivi hawataki kusikiliza wananchi na bahati mbaya hata Mwanakijiji ambaye alikuwa na moyo mkubwa wa kukosoa hataki kukosolewa..Tabia ile ile ya viongozi waliopita na haswa ukiangalia kwa makini uziwi huu unatokana na imani ya itikadi..

Kumbuka wananchama wa JF hapa ni waumini wa itikadi tofauti na kila mmoja analiona lake ni bora lakini mnachoshindwa kuelewa ni kwamba sote tunaamini UMOJA wetu ndio pekee utaweza kukomboa, na huu umoja hauwezi kupatikana kwa kutumia imani ya itikadi moja kwa sababu wananchi walio wengi ni maskini na wanataka kusikia sio jinsi gani watatoka ila nani atawatoa.. Ukiweza kunielewwa hapo utaelewa kkwamba yoote mnayozungumza ni kuhusu JINSI gani mtawatoa.... Hii ni lugha ambayo Wadanganyika wameizoea na CCM wanaitumia kila siku ya Mungu..lakini hakuna lolote.

Sasa nikirudi kwa CCJ nazidi kuisikia lugha ile ile ya vyama vilivyopita na hakika hakuna kitu nakiogopa sasa hivi kama matumizi ya Itikadi.. trust me nchi imeshakua ya Makafiri hivyo unapotangaza dini moja iwe Uislaam au Ukristu na hasa kwa makafir maskini waliokwisha kata tamaa ya maisha ni bora kwanza wape maisha, wape tumaini la Uhai huku taratibu ukigawa biblia yako.

Lakini kuitangaza Biblia (itikadi) pasipo miujiza mkuu wangu sidhani kama utawapata wengi kwani hata Mungu sii Mjinga kuwapa uwezo wa mijujiza Mitume wake badala ya kuwakabidhi vitabu tu..Nadhani ndivyo tulivyokuwa tukiwashauri Chadema kujiuza kwa wananchi vijijini wafanye miujiza hata kidogo kuliko kutumia fedha nyingi ktk helikopta, kutangaza serikali za majimbo na kadhalika..

Mkuu wangu, nafasi waliyokuwepo wananchi sasa hivi ni sawa na kusema na makafir (wasioamini) wakidai tuonyeshe miujiza ili tukuamini hiyo itikadi yenu! na kina sisi hapa tunasema miujiza ya CCJ inaweza kuwa tu ikiwa watapata nguvu ya kibinadamu ambayo hutokana na UMOJA..Waliposhindwa Chadema sii lazima washindwe wao, na pengine Chadema wanaweza kuwapa vikwazo vilivyowakwaza kisha CCJ wakajiweka ktk nafasi bora zaidi..

Binafsi naamini kabisa hizi itikadi haziwezi kufanya kazi kwa sababu Tatizo letu sisi ni UONGOZI BORA, na wananchi wote tuna mashaka na WATU viongozi na sio chama na itikadi zake. Hivyo itikadi haiwezi kuwa kigezo cha kiongozi bora hata kidogo, ila nia ya hao viongozi inaweza tu kuthaminika ikiwa wataweza kusikiliza ushauri wetu, mahitaji yetu na zaidi ya yote kuonyesha Uzalendo wao kwa Taifa.

Hizi hadithi za CCJ nazikumbuka sana wakati wa Chadema wakiwa juu. Mimi mwenyewe nilivutiwa sana lakini baada ya kugundua kwamba kuna mapungufu ktk utawala wake nimebakia muumini tu wa itikadi. Hii haina maana sina imani na chama ila kusema kweli sina imani na baadhi ya watu ndani ya chama hicho kama ilivyokuwa CCM, CUF, TLP, NCCR.. woote hawa sina imani na viongozi wake.

Kwa hiyo CCJ inapokuja na itikadi safi ni sawa na kitanda kilichotandikwa vizuri na shuka safi hali kuna kunguni wamejificha ktk magodoro inanipa shuku kubwa zaidi..nitarudia kusema tatizo kubwa la vyama vyetu ni UONGOZI hakuna chama kinachonyoosha mkono kutuokoa isipokuwa hadi za kufanya hivyo pindi tukiwapa nafasi wao..Na kibaya zaidi viongozi wa CCJ wamejificha chini ya magodoro na matendego ya chama wakituonyesha shuka safi (itikadi). How can we trust Ideology without people behind it...

Mkuu CCM atatushinda kila siku kwa sababu hizi.. Wao wanajua fika kwamba Wadanganyika wanataka sana kudanganywa..Na hadi siku mtume wa kweli atakapo kuja nina hakika ishara zitakuwepo...hadi sasa sidhani kama CCJ wameweza kuutumikia utume vizuri kwani mara zote shetani amewashinda kwa kila hatua. Na kibaya zaidi bado wanatoa sababu za kujiamini na itikadi, mkuu hii ni sawa na Mkandara nayejaribu kukuvuta wewe kuingia Uislaam.. Sii kazi ndogo hata kidogo na pengine haiwezekani!
 
Rev; wakati kujinadi kiitikadi ni jambo linaloonekana kuwa njia sahihi, unfortunately sidhani kama linaweza kufanya kazi katika siasa za Tanzania. CCJ walikuwa na njia nzuri kiasi cha kutosha kama wangefanikiwa kupata usajiri, yaani kama wangeweza kuchukua ile krimu nzuri ya CCM kwa njia ya surpriset, basi wangeweza kuteka wafuasi wengi kwa muda mfupi na huenda kushinda viti kadhaa vya ubunge. Ingawa nina imani kuwa wasingeweza kuiondoa CCM madarakani kamwe, kile kitendo cha kupunguza idadi ya wabunge wa CCM na kuongeza wabunge wa upinzani zaidi bungeni kingelikuwa ni mwanzo mzuri hasa ukizingatia kiwango cha elimu ya uraia walichanacho watu wetu.
 
Rev Kishoka

Mkuu suala la itikadi(idiology) ni zuri lakini ni gumu sana hasa kwa nchi zetu za kiafrika zilizo masikini, idiology is necessary but not sufficient, ni vigumu sana kuuza itikadi(idea/maneno) kwa watu nyenye njaa, mtu anayehitaji angalau apate mkate mkavu atafune sijui kama atakuelewa ukimwambia asubiri kwanza blue band.

Ni sawa na Mkandara anavyosema kuanza kumfundisha mfa maji anayezama mbinu za kuogelea , kwa hali ilivyo sasa watanzania wanahitaji mtu(kiongozi) wa kuwatoa walipo wameshachoka kusikia nyimbo za ujamaa sijui ubepari sijui milengo na nini,

Nikikuuliza Mrema na Mtikila walikuwa na itikadi gani miaka ya 90s sijui kama utaniambia, kwa nini basi walifanikiwa angalau kwa kiasi chao.

Naona wewe unapoongelea itikadi unaifananisha na sera kuwa mtakaa siku moja kuiandika nakusubiri utekelezaji. Itikadi(idiology) ni imani na imani haijengwi kwa siku moja inabidi uipe muda ijijenge yenyewe ndani ya mioyo ya watu, ni sawa na muumini wa dini anapobatizwa si kuwa tayari umeshajengeka kiimani.

Kishoka kudhani kuwa vijana wa CCM waliopo watageuka itikadi za wazazi wao ni ndoto, fahamu kabisa kuwa vijana kama kina Ridhwani au January wamelelewa ndani ya CCM na matunda wanayokula wanajua fika yanatoka wapi sasa kufikiri siku moja mtoto atajikatia mirija yake mwenyewe haiwezekani anatakiwa mtu toka nje kuikata hiyo mirija.
 
Afande Kamanda,

Kama ukirudi kule kwenye thread ya PPPT, nilijieleza kwa undani kuwa lengo si kukimbilia Uchaguzi, balini kujijenga kwa ajili ya malengo ya muda mrefu. Ndiyo maana nang'ang'ania suala la itikadi na nilieleza kwa ufasaha kabisa ni vipi PPPT itafanya kazi kwa kuanza kwenda vijijini kujijenga na kushirikiana na Wananchi na kuwalisha itikadi ya PPT.

Ndio kuna ulazima wa kukiondoa CCM madarakani, tena kwa haraka sana, lakini vyama vilivyoko kwenye uwanja wa Vita sasa hivi, vimeshindwa kabisa kujipanga katika miaka 20 iliyomalizika na huu ni uchaguzi mkuu wa nne na bado Upinzani haujapata footing nzuri ya kuweza japo kupata theluthi ya Bunge!

Sasa swali ni hili, katika miaka hii 20, waliowatangulia CCJ wamejijenga vipi kiimani (Kiitikadi) kwa Watanzania ? Ikiwa mpaka leo Watanzania pamoja na shida zote bado hawana imani na Upinzani wala hawaonyeshi kudiriki kujaribu kuwapa Wapinzani nafasi ya kuuliongoza Taifa letu, hatuoni kuwa kuna kasoro kubwa sana ?
 
Na hapa pa kutothamini itikadi ndio kunapowamaliza watanzania. Itikadi ni muhimu katika maisha/mfumo wa kisiasa kama ilivyo imani/dini kwa maisha ya kijamii ya binadamu. Kutothamini itikadi ni kutoa nafasi kwa siasa za longolongo/siasa za matumbo/populism.....Itikadi ni muhimu lakini lazima iwe ni itikadi ya dhati na sio ya kuvutia watu tu kama ambavyo CCJ walitaka kufanya na Ujamaa na kujitegemea. Na hapo ndipo ugomvi wangu na CCJ unapoanzia. Itikadi ka ya Ujamaa na Kujitegema na jina la Baba wa Taifa ndio misingi ya Utanzania wetu na ni HARAMU kwa mtu yeyote kutumia kama mtaji wa kulinda maslahi yake ama ya kundi fulani....

omarilyas

watanzania wana itikadi ya dini lakini sio ya siasa
siasa za tanzania ni rhetoric only ni group dogo sana la watu ndio linajua mambo ya itikadi

watanzania wengi wako ccm kwa ajili ya zimwi likujualo na upinzani wa kusuasua. watu wengi ambao nimepata kuwauliza kwa nini umeipigia kura ccm jibu lao ni moja tu sasa ni wapigie nani. Mrema alipata watu wengi sana ambao walitoka ccm na sasa wamerudi
na hiyo ni dhairi kabisa kuwa tz ni rhetoric na sio itikadi.

lakini kama wewe unadhani ccm wana itikadi naomba uniambie itikadi yao ni nini na je wanaccm wana relate vipi na hiyo itikadi??

note: ccm sio chama cha wafanyakazi tena na wala JK hataki kura zao. Maneno yao ya sasa hivi ni "maisha bora kwa kila mTZ", "mkukuta", "kilimo kwanza", "kasi mpya ari mpya" , and many more.
 
Rev. Kishoka,
Mkuu ktk swala la PPPT nadhani wengi tulikuunga mkono itikadi,sera na Ilani zake.. na hakika tunawaunga mkono CCJ kwa itikadi,sera na ilani zao pia lakini tumepinga kuwa itikadi isiwe ndio factor kubwa ya kuwania ushindi dhidi ya CCM..(katika Kujitangaza.)

Hili ndilo tunakataa pamoja na kwamba sisi wote humu tunaelewa wazi umuhimu wa itikadi ktk chama. Na nadhani pia unakumbuka kwamba nimewahi kulizungumzia sana jambo hili hapa JF ya kwamba hakuna chama chenye itikadi na kinafanya ibada zake kulingana na itikadi. Vyama vyote vinakwenda ili mradi vinapingana na CCM au kuweka ushindani kutokana na msisitizo wa IMF.

Leo utawasikia CCM wakijiita Progresive sijui liberal lakini ndani yake wamejaa pia conservative. Chadema wenyewe pamoja na kuwa conservative wameonyesha nia zaidi ya kuwa mrengo wa kati kushoto na sii kulia..CUF,TLP na kadhalika wote hawa ni sawa na waumini wasiokuwa na itikadi, whatever works for them..in fact, it has always been a question of dialectic rather than Philosophy..

Kama alivyosema Semilog, watu wetu wana dini zao lakini hawana itikadi ndio maana nikasema huko nyuma chukulia kuwa sisi wote ni Makafir. Na bado Semilog kafanya uungwana ktk matumizi ya lugha lakini ukiniuliza mimi nitakwambia hata hizo dini hatuna..zipo kama dini kwa jina lakini hakuna mtu anafuata ibada za dini hizo kikamilifu - Hakuna! Tumejaa unafiki mtupu, watu kudanganyana kuwa waumini wa dini kwa sababu tmezaliwa ktk dini hizo na sio kufuata mafundisho yake na kufanya ibada ipaswavyo...Hao Wakristu na Waislaam wa kweli hawajai hata mkononi... Hii ndio Bongo yetu!
Na hakika leo hii tumepoteza kabisa maana ya dini na hata Itikadi..
 
Na hapa pa kutothamini itikadi ndio kunapowamaliza watanzania. Itikadi ni muhimu katika maisha/mfumo wa kisiasa kama ilivyo imani/dini kwa maisha ya kijamii ya binadamu. Kutothamini itikadi ni kutoa nafasi kwa siasa za longolongo/siasa za matumbo/populism.....Itikadi ni muhimu lakini lazima iwe ni itikadi ya dhati na sio ya kuvutia watu tu kama ambavyo CCJ walitaka kufanya na Ujamaa na kujitegemea. Na hapo ndipo ugomvi wangu na CCJ unapoanzia. Itikadi ka ya Ujamaa na Kujitegema na jina la Baba wa Taifa ndio misingi ya Utanzania wetu na ni HARAMU kwa mtu yeyote kutumia kama mtaji wa kulinda maslahi yake ama ya kundi fulani....

omarilyas

Omarilyas,
Hupaswi kuwa na ugomvi wowote na CCJ kwa sababu sidhani kwamba unawajua viongozi na wanachama wote wa chama hicho kuweza kubashiri bila shaka yoyote na kuwahukumu kwamba wana nia ya kutumia itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea na jina la Baba wa Taifa kama mtaji wa kujipatia ama kulinda maslahi.

Kama wewe ulivyoweza kubaini kwa dhati kabisa kwamba itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea na jina la Baba wa Taifa ndio misingi ya Utanzania wetu, bila shaka CCJ nao wamebaini hivyo hivyo na kuamua kwa dhati kabisa kuichukua itikadi hiyo kama yao na kuitangaza bila kuionea haya ama kumung'unya maneno wakiamini kwamba ndiyo ilikuwa itikadi na dira sahihi kwa maendeleo ya nchi yetu. Jambo ambalo vyama vingine vimeshindwa kufanya.

Kama kweli tunamthamini Mwalimu na tunayathamini yale aliyolitendea Taifa hili kupitia itikadi yake ya Ujamaa na Kujitegemea basi tuombe kumtendea haki kwa kuwaacha Watanzania wenye nia wajaribu kutumia haki yao ya kidemokrasia, kutoka kwenye chama kimoja kwenda kingine ama kuunda chama. Tusiwahukumu kabla hata hawajafanya chochote zaidi ya kutangaza nia hiyo. Huenda wangeweza kufanikiwa kuliletea taifa maendeleo yanayolenga watu wote kwa kurejesha misingi bora itakayoendelea kujenga Utanzania wetu.

Pia, sidhani kwamba Mwalimu aliwahi kuacha wosia kwamba jina lake ama Itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea vina “hatimiliki!” Mwalimu alifanya kazi kubwa usiku na mchana kujenga taifa changa lililotoka kupata uhuru wake na alifanya hivyo kwa manufaa ya Watanzania wote na si ‘kundi’ la wateule wachache, alifanya hivyo na kupata mafanikio makubwa kupitia itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea. Lakini, hakufanya hivyo kwa matarajio kwamba atakapoondoka duniani basi jina lake na itikadi hiyo vikejeliwe ama vitundikwe ukutani vitundikwe ukutani na kusahauliwa umuhimu wake kwa Taifa. Sidhani pia kwamba alitaka Watanzania waogope ama kuwa na wasiwasi kum-enzi kwa kuifufua itikadi hiyo na kulitumia jina lake, achilia mbali watu kutishiwa kwamba ni HARAMU kufanya hivyo!
 
Bibi Ntilie,
Itikadi ni muhimu lakini lazima iwe ni itikadi ya dhati na sio ya kuvutia watu tu kama ambavyo CCJ walitaka kufanya na Ujamaa na kujitegemea.
Mimi nadhani Omarilyas kaunga mkono matumizi ya itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea ila yaonyesha CCJ wametaka kuitumia visivyo..Bila shaka swala zuri ni kumuuliza hao CCJ walitaka kufanya vipi kinyume cha Ujamaa wa Mwalimu huku wakitumia jina lake?.
 
Bibi Ntilie,
Mimi nadhani Omarilyas kaunga mkono matumizi ya itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea ila yaonyesha CCJ wametaka kuitumia visivyo..Bila shaka swala zuri ni kumuuliza hao CCJ walitaka kufanya vipi kinyume cha Ujamaa wa Mwalimu huku wakitumia jina lake?.

Mkuu,
With all due respect, ninaomba Omarilyas atueleze CCJ wametaka vipi kuitumia itikadi hiyo ama jina la Mwalimu visivyo? Nani mwenye uwezo wa kuingia kwenye nyoyo za viongozi na wanachama wa CCJ kuweza kujua kwa dhati kabisa kwamba itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea ama jina la Mwalimu linatumiwa visivyo na CCJ ambacho hata hakijaanza kazi kwa kuwa usajili wa kudumu hakijapata.

Kwa maoni yangu, dhambi ya CCJ inayowakera watu ni ile ya kuanzisha Chama hicho katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu na kutangaza wazi kwamba kinataka kipate usajili wa kudumu mapema ili kiweze kushiriki uchaguzi huo. Maswali yakaanza:

Swali la kwanza lilikuwa: Kina nani hawa? Mwenyekiti Kyabo na wenzake ni ‘makanyaboya' tu. Tayari ubaguzi hatari ukawa umeishajengeka kwenye vichwa vya watu kwamba Kyabo na wenzake hawawezi kuanzisha chama cha siasa kana kwamba wao sio Watanzania na hawana haki kufanya hivyo.

Kwa nini waende kulia kwenye kaburi la Mwalimu? Tukawahukumu - ni wasanii hawa! Bila sisi wenyewe kujiuliza ni nani miongoni mwetu ambaye ameweza kufanya kitendo cha kuchukua muda wake kwenda kuzuru kaburi la Baba wa Taifa kama kweli tulimthamini kiasi cha kuamini kwamba itikadi yake ndiyo iliyotujengea Utanzania wetu? Tuna uhakika gani kwamba machozi ya Kyabo na wenzake hayakuwa yanatoka moyoni? Lini tumepewa ‘u-Lucifer' wa kuweza kuingia ndani ya mioyo ya watu na kujua kilichomo?

Wapo wengine wanaodhani kwamba CCJ imeanzishwa kwa madhumuni ya kuwapokea Wabunge akiwemo Spika Samuel Sitta endapo wataenguliwa kwenye kuwania ubunge kupitia CCM. Kwa hiyo bila hata kujua kuwa watu hao kweli watajiunga na CCJ, na kabla hawajaonyesha dalili yoyote ya kutaka kujiunga, chama hicho kimeishahukumiwa kwamba kinafanya dhambi kubwa kwa kutumia visivyo na kujitangaza kwamba kitatumia itikadi ya Ujamaa na jina la Mwalimu. Hata kama walionyesha dhamira ya kutaka kujiunga na baadaye wakaghairi je hilo si nafuu kwa wana CCJ ambao wana nia ya dhati ndani ya mioyo yao ya kutaka ku-enzi jina la Mwalimu na itikadi yake?

Wapo wenzetu wengine wanaomfahamu Mzee Mwanakijiji ambaye sisi wengine hatumfahamu wala jina lake sahihi hatulijui lakini tumemjua kutokana na uandishi wake mahiri wa makala zinazotetea haki za wanyonge na Taifa la Tanzania kwa ujumla. Kwa kuwa hayuko nchini humu anakula kuku wake nje hangepaswa sana kuwa na sababu ya kuhangaika na maskini wanaoishi kwa kipato cha chini ya dola moja kwa siku. Hivi sasa tumeendelea kuujua zaidi msimamo wake kwa kuipigia debe CCJ bila hata kuambiwa kwamba yeye ana cheo chochote kwenye chama hicho. Naamini kundi hili lenye kumfahamu Mwanakijiji ndio haswa ‘wachawi' wa CCJ humu JF. Huenda wanamuona ni mwenzao tu, anawezaje kuwa miongozi mwa walioanzisha chama hicho; bila kujali mapenzi aliyonayo 'Mzee' huyo kwa taifa lake.

Tatizo letu Watanzania tuna hulka ya kudharauliana na kupigana vita bila sababu zozote za msingi. Badala ya kuzingatia madhumuni ya kuanzishwa kwa CCJ, tunakihukumu kwa kuangalia nyuso za waliomo na wasiokuwemo CCJ! Kwangu mie la muhimu ni yale ambayo CCJ wangeliweza kufanya kama wangepata usajili wa kudumu na si mbinu wanazotumia kupata usajili huo. Hata kama wakimtaja Mwalimu ama kuitumia itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea kama alivyosema Bibi Ntilie, vyote viwili havina ‘hatimiliki' vinaweza kutumiwa na Mtanzania yeyote mwenye nia njema na nchi hii. Sidhani kwamba Kyabo Mwenyekiti wa CCJ et al ni wahalifu wasioitakia mema nchi yao!
 
Back
Top Bottom