Trafiki wa ubungo tumewachoka!

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,877
2,758
Hii ni kwa wote wanaotumia junction ya ubungo mataa. wale trafiki wanapendelea sana hii barabara ya Morogoro na kupuuzia hizi za Mandela na Sam Nujoma. wakati mwingine kwa makusudi kabisa wanapuuzia hizi barabara. wasidhani wao ni wajanja sana. kama kuna aliyewatuma kufanya huo upuuzi basi anataka kuwaponza. awali walishapigwa na wanajeshi. sasa hivi watapigwa na wananchi wenye hasura zao. haiwezekani gari itoke Mbezi ipite mataa wakati anayetoka Tabata na yuko hapo songas awe anang'aa macho tu. Hii inachosha akili na mwili na madhara yake yanaweza kuwa si madogo. nadhani kamanda wa kikosi cha barabarani atapewa habari hizi. WAAMBIE VIJANA WAKO HII IS ALMOST ENOUGH. watu kusubiri dakika 20 mataa kisa magari ya morogoro road yanaruhusiwa ni ubinafsi na si ustaarabu. asitake wananchi wabuni njia mbadala ya kukomesha hili tatizo, njia ambayo italeta madhara kwa wanausalama na raia pia. nadhani ujumbe huu umefika
 
Mkuu, endelea tu kuchoka maana siku wakiwa hawapo pale, utakufa.

Mimi nawaaminia hawa jamaa. Wanajua wanachokifanya. Ukitaka kutesti zali hebu jaribu tu kupita yale makutano ya Afrika Sana pale Sinza mida ya saa 1 jioni. Halafu fikiria Ubungo itakuaje.
 
Mkuu, endelea tu kuchoka maana siku wakiwa hawapo pale, utakufa.

Mimi nawaaminia hawa jamaa. Wanajua wanachokifanya. Ukitaka kutesti zali hebu jaribu tu kupita yale makutano ya Afrika Sana pale Sinza mida ya saa 1 jioni. Halafu fikiria Ubungo itakuaje.
mkuu, suala sio wasiwepo bali waruhusu magari kwa uwiano unaofaa. Haiwezekani kuruhusu magari ya moro road kwa dakika 10 kisha ya Mandela kwa dakika mbili!
 
Back
Top Bottom