Traffic wala rushwa waziwazi daraja la Mlalakuwa (Mikocheni) mnatukwaza sana raia

Rah_sputin

Member
Nov 3, 2009
83
10
Kipindi cha UNU ( Usalama barabarani na Uraia) - kinaendelea sasa hivi TBC.
Traffic anafundisha raia usalama na utumiaji Mzuri wa barabara.

Nani asiyejua chanzo cha matatizo makubwa barabarani ni hao hao traffick wanaoomba rushwa waziwazi bila hata soni?

Wale mnaopita barabara ya Old Bagamoyo road mtakubaliana nami kuwa
hawa matraffic wanatia aibu hasa siku za jumamosi.Wanajazana pale utadhani wako kwenye mafunzo ya vitendo jinsi ya kuomba na kupokea rushwa!

Hivi serikali inaridhika na mtindo huu? Kama mnabisha piteni pale kati ya saa 3 asubuhi na saa 7 -8 mchana mjionee "maajabu' na aibu ya kufedhehesha jeshi la polisi hasa askari wa usalama barabarani.

Au tuwaleteenii picha ya kinachoendelea tuwaumbue kama Jerry Muro alivyowafanyia?
 
Mkuu,,bora uwaumbue kwa picha kabisa itasaidia hata walio nje ya dar kuona live unyambilisi wanaoufanya nao pia kujirekebisha/kuchukuliwa hatua. hapa ni kama umepiga porojo tu bila vielelezo!
 
Ma-Dereva wengi hapa Tanzania wanaendesha magari bila makaratasi na pia wanaendesha magari mabovu! Na hiki ndiyo chanzo cha "rushwa"!

Kama huna tatizo lolote na gari lako na udereva wako rushwa unatoa ya nini?
 
Back
Top Bottom