Traffic Police.

Nyangomboli

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
3,501
1,955
Wana jamvi niko safarini kuelekea Mwanza lakini ninachokiona kwa matrafiki wetu kwanza ni usumbufu pili ni wizi au rushwa ya wazi. Tangu kutoka Arusha mpaka Babati tumeweza kusimamishwa zaidi ya mara 10. Majengo, Arusha AirPORT, KISONGO, DUKA BOVU, MTI MMOJA, MAKUYUNI, MINJINGU, MBUYU WA MJERUMANI, MAGUGU, KARIBU NA BABATI SIPAJUI NA AFTER BABATI NA SASA TENA DAREDA. Wanachofanya siku hizi ni wale agents ndiyo wanateremka na wala matrafic hawapandi kukagua gari. Gari imejaza watu wamekalia ndoo. Ni hatari kusema ukweli. Mungu nusuru waja wako.
 
sijui kwanini traffic akikusimamisha lazima akuulize unafanya kazi gani?
 
Hhah Bado ukitoka hapo DAREDA, kuna kingine MITAA YA KWA SUMAYE, then kabla ya kuingia KATESH, then tena kabla ya kutoka KATESH, then kabla ya kuingia SINGIDA bondeni pale, then Njia panda ya kwenda Stand pale, then kabla ya kutoka SINGIDA pale mitaa ya SI.MBA CHAWENE ( AQUA). Ila hamioni hao hawana usumbufu kwani kw amagari madogo hawasimamishi na mabasi ni mwendo wa kuacha BUKUBUKU tu kote huko, USIOMBE SIKU UPITE NJIA YA TANGA CHALINZE MORO utakoma ni mwendo wa TORCH kila baada ya 5KM.
 
Anataka kujua ili apange namna ya kukukaba. Hapa hadi nimechoka. Traffic PoliceTHEN MATUTA. Ni kasheshe
 
Bora hata torch kuliko kuombwa buku kila kilometer 10 na hata hawakagui gari. Hawana aibu tena jamani.
 
Tupe na hali halisi ya barabara.

Mwema sijui anapitia humu? nimejaribu kumtumia post yako #1 kupitia: Feedback lakini inakataa.

Na wewe unaweza mtumia. Naomba hali ya barabara, nna safari ya kwenda Shinyanga, kupitia Arusha na Singida.
 
Wakati mwingine traffic ndo husababisha ajari unakuta kasimamisha gari eneo baya tena polini akidai rushwa!
 
Mmuulize Magufuli...
Tupe na hali halisi ya barabara.

Mwema sijui anapitia humu? nimejaribu kumtumia post yako #1 kupitia: Feedback lakini inakataa.

Na wewe unaweza mtumia. Naomba hali ya barabara, nna safari ya kwenda Shinyanga, kupitia Arusha na Singida.
 
Unategemea kupata nini kutoka kwa traffiki wakati wlio wegi ni watoto wa wakubwa na wengine wamehengo ndio wakapata nafasi hizo.na wote wako kwa ajili yautafutaji tu.kikosi hiki bila kuwa mtoto wa mkubwa au bila kutoa ruswa hupati nafasi.upewe na fasi hivihivi wewe umekuwa nani?.wakati ni kwa ajili ya kuwatajilisha watoto wa wakubwa.
 
sijui kwanini traffic akikusimamisha lazima akuulize unafanya kazi gani?

Kazi kweli kweli! Nadhani huwa wanaogopa kuchukua rushwa kutoka kwa watu wa system (takukuru, usalama n.k.). Usalama barabarani na kazi ya anayeendesha chombo havina uhusiano kabisa lakini ni swali ambalo trafiki huwa wanalipenda sana!
 
Unategemea kupata nini kutoka kwa traffiki wakati wlio wegi ni watoto wa wakubwa na wengine wamehengo ndio wakapata nafasi hizo.na wote wako kwa ajili yautafutaji tu.kikosi hiki bila kuwa mtoto wa mkubwa au bila kutoa ruswa hupati nafasi.upewe na fasi hivihivi wewe umekuwa nani?.wakati ni kwa ajili ya kuwatajilisha watoto wa wakubwa.

Eti traffic watoto wa wakubwa! mambo mengine yanachekesha. Pole sana kwa uelewa huo. Saidi Mwema mtoto wa mkubwa yupi?
 
Mwema ni shemeji wa jk.nilicho kiandika kuhusu traffiki ni hakika na amina.vinginevyo unapinga labda na wewe ni mmoja wao.halafu saidi siyo traffic pole wewe ambae unapinga kitu wakati kipo.
 
Tupe na hali halisi ya barabara.

Mwema sijui anapitia humu? nimejaribu kumtumia post yako #1 kupitia: Feedback lakini inakataa.

Na wewe unaweza mtumia. Naomba hali ya barabara, nna safari ya kwenda Shinyanga, kupitia Arusha na Singida.
ukitaka usisumbuliwe nunua mikate arusha wakikupiga mkono unawaachia mmoja kila kituo utafika saaalama kbs
 
halafu hawa ukitaka kuwatili9a sumu utawaua sana, wanapendaga sana rushwa ya machungwa, nyanya, mikate, machenza, viazi etc
 
Hili jambo nilitaka kulisemea siku mbili tatu kabla ya leo , polisi wana tabia mbovu sana na ni ya kuzidishiana umasikini ,hawa wa Tanga Dar hawachagui aina ya gari ,ni lazima uwe na hela si chini ya laki kumi ,kila polisi anaekusimamisha basi anakutafutia jambo lolote ,kama hamna basi anakuambia mbona hukufurahia kusimamishwa na yeye ,umpe chochote ,shauli zao nitaanza kuwashawishi watu zile hela wanazowapa polisi wazifanyie namna flaniflani ,kazi kwao.
 
Mwema ni shemeji wa jk.nilicho kiandika kuhusu traffiki ni hakika na amina.vinginevyo unapinga labda na wewe ni mmoja wao.halafu saidi siyo traffic pole wewe ambae unapinga kitu wakati kipo.

Sasa shemeji yake ndio mwanawe? halafu ni shemeji yake kwa nani? Na Kikwete ni mtoto wa mkubwa yupi?
 
Back
Top Bottom