Traffic police fuatilieni tatizo hili

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,621
2,567
Baadhi ya makondakta wa daladala wanatoa tiketi ambazo haziendani na namba za magari yenyewe. Zamani nilipokuwa nikipewa tiketi, nilikuwa naitunza na baadaye kuitupa bila kusoma imeandikwa nini.

Baadaye, niliamua nikipewa tiketi niwe naisoma na kuona kama inaendana na namba za gari yenyewe na route ya gari. Tangu nianze kufanya hivyo, nimegundua kwamba tiketi haziendani na namba za magari lenyewe. Sijui ni kwa nini makondakta wanafanya hivyo.

Lakini kama litatokea tatizo fulani, mfano, ajari au abiria kupoteza mzigo au mtoto au mgeni itakuwa vigumu kwa abiria huyo kubaini gari alimojipakia na pia kama ni kitu cha dharura itashindikana kutoa ushirikiano kwa mamlaka husika kwa ufuatiliaji vile tiketi siyo za gari lenyewe.

Kwa hili, naomba traffic police walifuatilie kwa karibu na makondakta wanaopatikana wakifanya ulaghai kama huo wapewe adhabu zitakazowafunza kuwa wawajibikaji katika kazi zao.

Inafaa pia abiria wapewe maelekezo ili kama watabaini vitu vya namna hiyo, waweze kupeleka matatizo yao kwenye mamlaka husika na ikiwezekana wapewe namba za simu za mkononi ili wawasiliane na mamlaka hizo.
 
Back
Top Bottom