Traffic police arusha.

Ni habari ya uhakika kabisa ambayo nimeifanyia uchunguzi wa kutosha. Wakiingia kazini hawa askari wanapewa jukumu la kila mmoa hataruhusiwa kuondoka alipopangiwa hadi akamate magari 20 ambayo yatalipa notification ya 30,000 each! Tunapelekwa wapi?

Siyo kweli ilikuwa kila mmoja ni lazima akamate magari matatu ambayo yana makosa hasa kipindi kile cha foleni kubwa Arusha ambapo watu walikuwa wanatanua tu hasa kutoka Mbauda, Kisongo jambo ambalo siyo gumu kabisa maana kuna watu wana vichwa ngumu sana barabarani.

Na kwa kukujuza tu hilo ni agizo toka serikalini ili kupunguza makosa barabarani na kuongeza pato la taifa kwa kupitia fines & penalties.
 
Sijakurupuka Inno laka, ni utafiti wa kweli nilioufanya kwa makini na kubali kataa ndivyo ilivyo: hujakamata magari 20 yatakayolipa notification ya 30,000 @ kwa siku hutapata posho/renumeration.

Wala asibishe kama haamini mwambie aendeshe gari mchana barabara za mosh arusha.namanga arusha.mirongoine na kisongo.kama pale ngaramtoni ya chini hakuna gari inayopita bure
 
Juzi wamenisimamisha Boma wakachukua 5000, pale KIA (less than 5 KMs from BOMa) wakata 20000 nikagoma wakachukua 10000. Kufika King'ori (Pia Less ama equal na 5 KMs from KIA) wakasimamisha nikaona ushenzi nikasepa, kufika KIKATITI (almost 5 KMs from King'ori) wakasimamisha tena nikasepa wakanifuata kwa gari, kufika USA nikawekewa Barrier nikapeleka Gari kituoni wanataka All Charges plus mafuta ya kunikimbiza kama 150,000 nikawaambia sina kama vipi bakini na gari.
Nikaita Taxi nikiwa pale pale, wakaona hiyo Confidence wakaogopa wakanipa gari yangu nikasepa.
Kwao ni kawaida sana na kama wewe ni muoga ukitoka Sakina mpaka ufike Moshi mjini unakuwa umepoteza zaidi ya 150,000 barabarani.

Kama Huamini njoo ujionee na gari yako isiwe na Kile kitambaa (alama) ya CCM ndani uone utatoa bei gani kutoka tu Mianzini mpaka Usa-River.

Kuna siku nilikuwa natoka Arusha nakwenda Moshi, kufika Moshi nikakamatwa. Wakakagua gari yangu wakaona haina makosa isipokuwa nilikuwa sina stika ya week kwa nenda kwa usalama. Akaniambia inabidi nukushitue kidogo, nikamwambia wapi???? Hapa hapa au polisi, maana nina haraka kidogo tehe tehe tehe. Akaingia ndai ya gari nikaondoka kwa kasi sana, akanipiga mkwara nikamwambia nina haraka sana na nimekwambia na hivi ulivyopanda gari hii itabidi unifuate ratiba yangu, nipo serious. Akaniuliza unafanya kazi gani nikamwambia haukusu kazi yangu. Nikaenda mpaka idara ya maji Moshi kule karibu na nyuma ya uwanja wa ndege, nikaingiza gari ndani. Kwa akili yake akajua ofisi za jamaa zetu wae wanaolalamikiwa sana kuhusiana na sinema ya Ulimboka, nikamwacha kwenye gari nikamwambia nakuja sasa hivi.

Nikaingia ndani kurudi sikumkuta, kuuliza nikaambiwa alichukua boda boda akasepa, inahitaji confidence lakini ndiyo hivyo.
 
Mmbangifingi! Trafki wanapaswa kunufaikaje zaidi ya kupunguza ajali na kuhakikisha sheria zinafuatwa? Wale watumiaji barabara wanalipa faini na kuipeleka kunakohitajika wala sio matumbo binafsi?
Vitabu vitakuwa fake malipo yanaingia matumboni mwao, otherwise hata wao hawana wanachonufaika kama zote zaenda serikalini kweli
 
Mmbangifingi! Trafki wanapaswa kunufaikaje zaidi ya kupunguza ajali na kuhakikisha sheria zinafuatwa? Wale watumiaji barabara wanalipa faini na kuipeleka kunakohitajika wala sio matumbo binafsi?

Mkuu,,polisi ya Tz sio hivo.ushasahau kashfa ya askari aliyekamatwa Chang'ombe Dar akiwa na Certificate of Competences fake? Na wale wa Ubungo na vitabu vya Notifications fake? HAawana time/focus ya kupunguza ajali bali kujitafutia rizki ya kila siku
 
A town daah mpaka ninavyo ongea wameshakula elfu mbili yangu na jioni wanakula elfu hiyo ni kawaida hapa frency corner hiace za ungalimited na zipo zaidi ya hiace 80 nimejaribu takukuru wana ruka ruka kuja .zinaniuma kinoma hizi elfu tatu za kila siku .
 
Da, mkuu ni kweli kabisa kuhusu Trafiki Arusha ni noma yaani ni ujinga mtupu hapa mjini tu unawza kusimamishwa mara 4 alafu ujinga zaidi wanasimama kwenye junction hivyo wanasababisha foleni zisizo na msingi. mfano utasimamishwa technical then mianzini ukipita huku makongoro unakutana nao pale kituo cha polisis ni kero balaa.
 
Hii habari ni ukweli maana hata mimi nilikamatwa juzi traffic alisimamisha gari na akaingia ndani ya gari na akasema inakosa twende kituoni, nilipofika kituoni wakasema side mirror imechakaa wakanandikia 30,000 ila kiukweli ilikuwa iko poa sana wala haina mkwaruzo......Traffic wa Arusha wanaambiwa na officer wao kila mmoja apeleke magari kadhaa kila siku kituoni so hakuna wanachofanya zaidi ya kuhesabu amepeleka magari mangapi kituoni.
 
Siyo kweli ilikuwa kila mmoja ni lazima akamate magari matatu ambayo yana makosa hasa kipindi kile cha foleni kubwa Arusha ambapo watu walikuwa wanatanua tu hasa kutoka Mbauda, Kisongo jambo ambalo siyo gumu kabisa maana kuna watu wana vichwa ngumu sana barabarani.

Na kwa kukujuza tu hilo ni agizo toka serikalini ili kupunguza makosa barabarani na kuongeza pato la taifa kwa kupitia fines & penalties.


wewe nadhani unaongea hauko Arusha matraffic wa Arusha huwa h awaangalii makosa bali ni magari mangapi amepeleka kituoni
 
Back
Top Bottom