Traffic na tafsiri ya Service Road. Faini yake iko Kisheria?

Ambiente Guru

JF-Expert Member
May 21, 2012
2,596
1,071
Wana FJ, Tahadhari wanaoendesha magari Bagamoyo road na kuchepukia service road hapo Namanga.
Traffik watega hapo. Wanachukua faini kwa wale wanaopita service road iliyo mbele ya Exim Bank. wanaweka vikosi viwili hapo kwa kazi hiyo. Hata uwe unaingia ATM, Dispensary ya Watoto au Jengo la Air Tel wanakudaka tu.
Ukiwauliza tafsiri ya service road wanasema ni barabara ya waenda kwa miguu.

Naomba mwongozo wa wana JF.
IGP sijui anakubaliana nalo hilo?. Jana wamechukua pesa zangu. Sioni mantiki yake kwani ni barabara pana ya lami inayoingiza watu kwenye ATM ya benki ya Exim, kuziba pancha, kununua matairi nk. Polisi kama taasisi ya serikali inatakiwa kutumikia vyema jamii. Otherwise few members Police department may be tarnishing the image of the force by poor understanding of the law. We call upon the IGP to make sure traffic policemen understands well the regulations and no misinterpretation.

Candid to my Country

Anonymous
 
Jamaa ni wajinga,utakuta wanakusumbua hata kama unatoka kwenye nyumba ambayo ipo service rd.
 
Pale ubungo huwa wanatega kituo cha mafuta cha Engen. Wanakaa upande ambao magari yanayotoka kujaza mafuta hapo kituoni hutokea. Hawana stori na mtu, wapo kikazi zaidi, sura ya mbuzi wanakusanya mapato.

Kimtindo wanamwaribia biashara huyo jamaa, kwa sababu kila mtu ataogopa kuingia hapo kituoni kwa kuhofia kudakwa anapotoka.
 
Bongo hamna sheria imekuwa ni kama nchi ya manyang'au. Kila mtu anafanya anachoona kinamfaa. We fikiria mtu anakukamata kwa 'trafiki case' halafu anakung'ang'ania ulipe faini papo hapo, hiyo ni sheria ya wapi?. Wanatake advantage ya watu kutojua haki zao chini ya sheria ya usalama barabarani.
 
Pale ubungo huwa wanatega kituo cha mafuta cha Engen. Wanakaa upande ambao magari yanayotoka kujaza mafuta hapo kituoni hutokea. Hawana stori na mtu, wapo kikazi zaidi, sura ya mbuzi wanakusanya mapato.

Kimtindo wanamwaribia biashara huyo jamaa, kwa sababu kila mtu ataogopa kuingia hapo kituoni kwa kuhofia kudakwa anapotoka.

Kama niliingia sawa sawa, hapa wataniua, yaani siwapi hata senti tano.... huu ujinga mimi siiukubali kabisa....
 
Mimi wakinisimamisha napandisha vioo halafu uso wa kauzu kama hawapo napita
 
Service road zote zinachakachuliwa na traffic. Mi naona hawaelewi maana ya service road. Kama wanasoma hapa jamvini wasome wapate elimu. Service road ni barabara inayopeleka magari kwenye ofisi na viwanda vilivyopo sehemu hizo. Kwa mfano Pugu road a.k.a Nyerere road kuna viwanda vingi na si rahisi utoke main road uingie kiwandani hivyo wakaweka service road. Hao waenda kwa miguu wanotengenezewa service road mi sijawahi ona hilo!! Ni uonevu tu. Mie nadhani traffic wanaona raha tunavyopata tabu na foleni ndefu za barabarani. Kama nimekosea mtu anielimishe hapa!!!
Wana FJ, Tahadhari wanaoendesha magari Bagamoyo road na kuchepukia service road hapo Namanga.
Traffik watega hapo. Wanachukua faini kwa wale wanaopita service road iliyo mbele ya Exim Bank. wanaweka vikosi viwili hapo kwa kazi hiyo. Hata uwe unaingia ATM, Dispensary ya Watoto au Jengo la Air Tel wanakudaka tu.
Ukiwauliza tafsiri ya service road wanasema ni barabara ya waenda kwa miguu.

Naomba mwongozo wa wana JF.
IGP sijui anakubaliana nalo hilo?. Jana wamechukua pesa zangu. Sioni mantiki yake kwani ni barabara pana ya lami inayoingiza watu kwenye ATM ya benki ya Exim, kuziba pancha, kununua matairi nk. Polisi kama taasisi ya serikali inatakiwa kutumikia vyema jamii. Otherwise few members Police department may be tarnishing the good image of the government by poor understanding of the law. We call upon the IGP to make sure traffic policement understand well the regulations and no misinterpretation.

Candid to my Country

Anonymous
 
Tukubali kuwa hakuna sheria za barabarani Dar es salaam. Practically hakuna na hii ni sababu ya " ujuaji wetu".

Tusilaumu ujuaji wetu nod unafanya tupigwe notification kila kukicha.

Tuombe mungu atupe kizazi kijacho kinachoweza kuelewa maana na ustaarabu wa taratibu na sheria za barabarani.
 
Nakubali mkuu, wengi wetu tunaoendesha magari sheria za usalama barabarani hatuzifuati, mfano service road hiyo ya bagamoyo rd kutokea mjini wengi huitumia kutanua na kwenda kuingilia pale ofisi za Zain-ni wachache kama wapo wanaoitumia kwa ajili ya kuingia kwenye ofisi zilizopo jirani- kuwalaumu trafiki kwa hili ni kuwaonea kwani haya tunayataka wenyewe (wanapowatandika faini mi nafurahi zaidi kwani huwa nina kereka sana nikiwa kwenye foleni halafu mtu mwingine anajidai yeye wa mjini sana na kutanua!!)
 
hiyo ndio maana ya service rod???
 
Back
Top Bottom