Tractor za suma jkt, kilimo kwanza!

Hute

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,537
6,458
Nilikuwa naangalia kipindi cha suma jkt hapa tbc one, aise kuna matractor mengi sana, na kwa jinsi wanavyoyasambaza, nimependa kama yangesambazwa tz nzima ili kweli kilimo kwanza hicho kifanikiwe, na tugeuze tz iwe ya kijani kabisa. nawapa hongera viongozi wa selikali kwa suala hili, hata kama mimi si mwana ccm. Mungu ibariki Tanzania.
 
Hayo sio matrekta ni kanya boya. Yanakunywa mafuta zaidi ya V8.

Je wajua ni makampuni ya wajanja aki J..........Bei yake inatisha ndio maana walazimishwa kukopeshwa deni kubwa mno kuna mbgune mmoja aliwahi kusema ni afadhali wandepewa hela wakanune nje kwa miliono nane kuliko moja kuuziwa kwa milioni zaidi ya 20! ili watu wapate kamisheni zao! 2015 ije haraka!
 
ssiamini muyasemayo....ila mimi nimependa sana uhamasishaji huo, hata kama tunapigwa changa la macho, lakini naona tunakoelekea si kubaya sana...
 
Sasa matractor ya suma jkt yamefikaje kwenye juukwaa hili?. Kama umehamasika nenda kanunue.
 
Kwa waliosoma marketing ni rahisi kukuelewa,wewe umependa picha nzuri za matractor na lugha nzuri ya kibiashara.Laiti kama ungejua ni kwa kadri gani wananchi wa Mbeya walivyosikitishwa na mpango wa serikali wa kukibadilisha kiwanda cha zana za kilimo (ZZK) kuwa kiwanda cha pombe,bila shaka huo utumbo wa KILIMO KWANZA usingeupongeza.Kwa tafsiri rahisi ni kwamba unasifia nchi yako kugeuzwa jalala la soko holela huku viwanda vyake vikifa.Pia wanastahili sifa gani magamba wanaowauzia matractor watz kwa bei kubwa kuliko uwezo wao? Tanzania imara haitatokana na unafiki kwani maana ya ukweli ni kutokuwa na element za uwongo3
 
Sasa matractor ya suma jkt yamefikaje kwenye juukwaa hili?. Kama umehamasika nenda kanunue.
na wewe kama hujahamasika nyamaza, ipotezeee, kwani jamii forums ya kwako peke yako bwanaa...alaaa kwenda zako huko
 
Hakuna matrecta hapo kwa bei hata ubora kwa sisi tunaolima estates,ni heri ukanunua marsey furgason used kuliko hayo ya jkt mapya.waulize wakulima wa uyole/ubaruku kwa nini wameendelea kukomaa na powertiler zilizofungwa mashine ya amec ya kupasulia mabo na kusagia,na kwa nini engine zinazokuja na hzo powertiler wanaondoa wanaweka armec?
 
Kunaweza kuwa na elimu hapa!
Hebu tupe tips zaidi sir! Turudi kutumia Valmet za Finland, tutumie matrekta ya Kilimo kwanza (farmtrac) ama tuendelee ku-modify power tillers kwa kuweka injini za Adico, JD, GD na Amec?
 
Back
Top Bottom