TRA yakamata mitambo ya Dowans

JAna usiku nilipokuwa naangalia ITV nilisikia habari ya serikali kuingia Kampuni ya kuzalisha umeme ya dowans, sikuelewa hasa ilikuwaje kwani nilipata habari hii kwa ufupi sana.
Mwenye datas zaidi naomba atuwekee.
 
Ni upuuzi tu...............but we are approaching the end.
..you r right,toka mwaka jana baada ya termination ya contract TRA walikuwa wp? lakin pia hii mitambo kuendelea kubaki kwenye yard ya TANESCO ina maana gn? dowans walitakiwa mitambo yao hapo haraka!!!! je wanalipa security charges kuiacha hapo?
 
Jioni ya leo TRA wakiongozana mawakala wao Majembe walifika kuliko mitambo ya Dowans wamefunga kufuli zao na kukamata magari ya wafanyakazi wa Dowans,pia waliagiza mitambo isiuzwe wala isihamiswe. Cha ajabu nasikia haupita muda walirudi tena wakiwa wameloa jasho na kufungua kwa amri kutoka Ikulu. ikulu ina ubia na Dowans??!!



As per in red above we will appreciate if you table the proof from State house directing TRA and Majembe team as explained above.


si vizuri kumchafua rais wa nchi yetu kwa mambo kam hayo,hivi kweli kama wanadaiwa kodi kubwa kiasi hicho Rais anaweza tena kufanya haya yanayosemwa hapa jamvini?

we better be realistic on our presentation.

Thanks
 
hii itambo mbona longtime tra wameizuia?sio issue ya jana wala leo,basi tu media nao imeamua kutoa as if ni kitu mpya
 
Jioni ya leo TRA wakiongozana mawakala wao Majembe walifika kuliko mitambo ya Dowans wamefunga kufuli zao na kukamata magari ya wafanyakazi wa Dowans,pia waliagiza mitambo isiuzwe wala isihamiswe. Cha ajabu nasikia haupita muda walirudi tena wakiwa wameloa jasho na kufungua kwa amri kutoka Ikulu. ikulu ina ubia na Dowans??!!

Khaaah.........!
icon8.gif
icon8.gif
 
Khaaah.........!
icon8.gif
icon8.gif

Next Level!
Mihimili ya Dola inagongana hizo ni dalili tosha kwamba dola imefikia ukiungoni. Last year msanii mmoja kwa jina Jakaya Mrisho Kikwete aliweka saini decree ya kuondolewa mitambo ya DOWANS kutoka pale TANESCO baada ya kuvunja mkataba mimi nashangaa huyo ni Rais wa aina gani ambaye anatoa Amri hazitekelezwi tena amri hiyo ina happy birthday bado anadhani kweli yeye ni rais au ni mdoli?
Alitoa amri kwamba Richmond wasilipwe hata senti tano lakini wakalipwa 33million US dOLARS na wakakopa USD 72million na Bank Kuu plus Hazina wakampatia huyo mdudu DOWANS guarantee it means mashine by implication ni za Serikali and one Buudy in the name of Dr. Idris Rashid akisaidiwa na ZITTO KABWE wakataka Tanesco wainunue hiyo mitambo iliyowekwa poni and the same president akatabasamu giza likatishiwa kuwepo August 09 na iilpotimia Oktoba likawepo kwa kutangazwa mgao wa umeme na akaamka usingizini akaagiza iwashwe mitambo ya IPTL aliyoagiza akiwa Waziri wa Fedha back in 1995 akitokea kuwa waziri wa nishati and you say hajui na ni mchumi I don't know how. IPTL costs about USD 500,OOO PER day huku ikizalisha umeme ambao ukiuzwa bei yake haizidi USD 200,000 PER day and this guy smiles and assumes business as usual then tumpeleke mirembe pamoja na Sophia Simba!!! nAWASILISHA Damn it!!!
 
Tehe nimefurahi kumwona yule jamaa msimamizi wa mitambo aliyekataa kutaja jina lake akasema mkawaulize wenye mitambo yeye si msemaji wa kampuni, anaitwa mr mwandenga, ni engineer, miaka ya 90 alikuwa tanesco naona kumbe alifuata green pastures kwa fisadis

Namie namkumbuka hasa pale mlimani alikuwa kipanga sana.Nadhani kwa ukifaa wake na uchapakazi wake tulipokuwa naye TRIANGLE -Zimbabwe aliamua kurudi home,masikini sijui DOwans walimdaka wapi? Yawezekana kwa utaalamu wake aliobobea katika mitambo ya kufua umeme.
Anyway mjomba, yawezekana hajui chochote kweli.Tusimlaumu kwa hilo.waandishi wangewatafuta wasemaji ili tujue kunani na mihela yote hiyo.
Ila tusi-attack personality yake tujadili hoja iliopo jamvini
 
Kaazi kwelikweli
Hata kama hao TRA wakamate hiyo mitambo hakuna chochote kitakachofanyika.Ni mara ngapi serikali inatangaza kuwakamata mafisadi halafu hawafanywi chochote?Tumechwoshwa na mambo ya kizushi.Kina White hair wapo wanakula vitita vyao vya kuifisidi nchi na kina Chenga.
 
Makufuli yaliyoifungia Dowans yaondolewa kinyemela


Mussa Mkama na Patricia Kimelemeta


MAKUFULI yaliyokuwa yamewekwa katika lango kuu la kuingilia katika eneo la mitambo ya Kampuni ya Dowans, inayojihusisha na ufuaji wa umeme wa dharura, yameondolewa kinyemela.


Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Dowans, Stanley Munai, hatua hiyo imefanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kupitia wakala wake wa kukusanya madeni sugu, Kampuni ya Udalali wa Mahakama ya Majembe Auction Mart.


Munai alisema hata hivyo, hatua hiyo imefanywa bila kuufahamisha ungozi wa kampuni yake.


Mkurugenzi huyo alisema juzi, wakala huyo alikwenda katika ofisi za Kampuni ya Dowans akiwa na kufuli zake na kuzifunga katika lango kuu la kuingilia katika eneo la mitambo, bila kibali chake kusainiwa.


Alisema hata hivyo jana, wakala huyo alirudi katika eneo hilo na kufungua lango hilo, baada ya kubaini kuwa ametenda kosa.


“Wakati hayo yote yanatendeka juzi mimi au sisi hatukuwa na taarifa ya ugeni wa aina yoyote tuliona makufuli katika milango yetu, tukashangaa, kwa sababu hata kibali cha kusaini kufungiwa kwa milango hiyo hatujasaini,�alisema Munai.



Munai pia alielezea kushangazwa kwake na hatua ya TRA kuidai kodi Dowans, wakati ikiwa imeshafungiwa kwa muda mrefu.


“Tumefungiwa kufanya kazi kwa kipindi kirefu sasa, hivi tunauliza kampuni iliyofungiwa inawezaje kudaiwa kodi wakati haizalishi, hicho ni kitu cha kiungwana kweli,� alihoji Munai.


Alisema kwa sasa, Dowans na TRA zinaendelea na mazungumzo ya kuiwezesha kampuni kujua nini inachodaiwa na wapi inapaswa kulipa.


Alisema "mfanyabiashara na mkusanyaji kodi ni mtu na rafiki yake, wanafanya kazi pamoja na kwa kushirikiana, mfanyabiashara kudaiwa kodi si kitu cha ajabu na lazima alipe."


Kuhusu muda wa siku kumi ambazo Majembe Auction Mart imezotoa kwa Dowans kulipa deni vingine mitambo yake itapigwa mnada, mkurugenzi huyo alisema hizo ni porojo ambazo hazina msingi.



“Sisi hatumjui Majembe, hizo fedha anazodai kuwa tunadaiwa ni porojo zake tu, hafanyi kazi na sisi, kwa hiyo wanayosema ni maneno yao,� alisema.


Juzi kampuni hiyo iliweka kufuli katika lango la Dowans, ili kuishinikiza kuilipa TRA Sh 9 bilioni, jambo ambalo lilisababisha usumbufu kwa wafanyakazi.


Kwa mujibu wa habari hizo, deni hilo linalosemekana kuwa ni la muda mrefu, limetokana na Dowans kushindwa kutolipa kodi zake mbalimbali kwa TRA.


Alipotakiwa kuzungumzia suala hilo, Mkurugenzi Mkuu wa TRA, Harry Kittilya, alisema yeye si mhusika katika suala la ukusanyaji wa kodi na kuweka kufuli katika lango kuu la Dowans.


Alisema wahusika wakuu ni idara ya ukusanyaji wa kodi na kwamba ndiyo yenye mamlaka ya kujua kama kampuni hiyo ama imelipa au haijalipa deni.


Katika maelezo yake juzi, Ofisa Masoko wa Majembe Auction Mart, Dickson Kitime, alisema hatua hiyo imechukuliwa kufuatia kampuni hiyo kushindwa kulipa kodi kwa muda mrefu.

http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=15910
 
Tahadhali. angalie jamani wasije TRA wakawa kama chambo wakatumia majembe action mart kuuza then lowasssa au rostam kwa mgongo wa nyuma kwa kutumia watu wengine wakaununua then wakaanza kuuza umeme TANESCO. Afadhali serikali itaifishe mtambo huu. Lakini hawana ubavu kabisa.
 
Back
Top Bottom