TRA yajipanga kudai mabilioni CHADEMA

Kwa hiyo ulivyoongea na hicho "chanzo" chako cha habari ndani ya TRA wamesema wanaifikisha lini CDM mbele ya sheria? Waambie wanasubiriwa kwa hamu, CHADEMA ni waumini wa WAJIBU na HAKI, Naamini JOPO la wanasheria CDM watasimama kidete kuhakikisha haki zote zinatendeka kwa USAWA ulio SAWA; MUMENO UKIKATA MBELE, SHARTI NA NYUMA UKATE! JE, MTAWEZAKULIPA KODI MNAZODAIWA NYIE MAGAMBA?:becky::becky::becky::becky::becky::becky::becky:
 
Kweli nyani haoni kundule, ninyi mnawasema waandishi wa gazeti bila kusema hoja yenyewe. Great thinkers? Blaa blaa blaa!
 
Mafilili.
i) Kodi haidaiwi kwenye magazeti, TRA walitakiwa kuleta Hati ya Madai Chadema, na baada ya Hati hiyo wanaenda Mahakamani. Ndiyo hasara ya ushabiki, lakini sishangai Gazetti lenyewe Uhuru Mali ya Chama cha Mafisadi na kuwadi wa Mafisadi.
2) TRA walifika CHADEMA. Waliahidi watarudi Chadema kutoa Taarifa yao. Hadi leo hawajaonekana. Huu ndio ushahidi wa chombo kinachotakiwa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria lakini kinatumika kisiasa, na kulinda ufisadi ndani yake kwa propaganda zisizo na msingi.
3) Hoja ya msingi ni:-
a) Waziri Mkuu anatakiwa kulieleza Taifa hili kwanini Bwana Luoga hajachukuliwa hatua za kisheria na kinidhamu hadi leo wakati nilimwandikia toka mwaka 2008. Hiki ni kiashiria jinsi Serikali inavyolinda ufisadi, ubadhirifu, na uwizi wa Mali ya umma. Waziri Mkuu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali TRA wote wanajua jinsi Taifa lilivyoingizwa hasara ya Millioni 550 kwa kushikilia magari ya Tango Transport kwa siku 90 (kwa makosa ambayo hata yangelikuwepo-na bado hayakuwepo ndio maana alilipwa shs 53 Millioni na hati,maye interest ya 550 Millioni). Pili Masdai ya Tango Transport ya kushikilia Kadi ya magari Semi Trailer na Magari yenye Trailer na mengine madogo kwa zaidi ya miaka 10 kinyume na sheria. Uzembe wa mtumishi wa Serikali haiuwezi kuachiwa kufilisi wazalendo na wao wakaendelea tu kula kuku kwa mrija. Luoga anategemewa kustaafu katikati yamwezi huu (Juni 2011). Hatutakubaliana Luoga alipwe mafao yake na joto la jiwe linamsubiri punde.
b) TRA inapaswa kueleza na kuweka hadharani kama wanavyofanya kwenye vyombo vya uhuru na magazeti ya Serikali hela hiyo iliyolipwa na inayotakiwa kulipwa kwa Tango Transport ni kiasi gani, "hata ingelikuwa kweli na kodi wanayodhani Dr Slaa hakulipa( ikumbukwe, Dr Slaa amelipa kodi kipindi chote cha Ubunge, labda waseme hakulipa na iwapo ni hibvyo lazima waliambie Taifa zaidi shs 360,000 nilizokuwa ninakatwa kwa mwezi zilikuwa zinaenda wapi?) ikilinganishwa na mabilioni aliyolipwa na anayotakiwa kulipwa Tango Transport (na wengine ambao bado ninakusanya taarifa zao)
4: Nimekwisha kutamka iwapo TRA wanadhani chadema haijalipa kodo toka 1992 hadi leo basi walete hati ya madai tuone wanadai nini na ni kiasi gani au waende Mahakamani kudai iwapo wanadhani kuleta Chadema hati hizo ni ngumu. Sheria inawaruhusu kwenda mahakamani, tukutanie kule.
5: Nimekwisha kusema, iowapo wataleta hati ya madai Chadema, kwanza watangaze kwenye vyombo vya habari ili watanzania wote wajue,:-
a) Mishahara/posho zote za viongozi wote wa vyama vya siasa ikianzia na CCM (ambao wanalipa posho hadi wilayani) tujue wamelipa kiasi gani tangu 1992 kwa majina ya viongozi wote. Hii ni pamoja na Wenyekiti na Makamu wenyeviti wote.
b) Mishahara na posho zote za Wabunge, Makatibu wakuu wa Wizara, Viongozi wakuu wote wa TRA, Makamishna mbalimbali na watendaji wakuu wote wa Taasisi zinazojitegemea. Kwa Taarifa niliyo nayo kuna ufisadi mkubwa katika eneo hili, na kwa Taarifa ya WanaJF wabunge, akiwemo DR Slaa posho zaidi ya 5 million kwa mwezi) zilikuwa haziingii kwenye payroll na mbunge alikuwa anakutana nayo tu benki. Dr Slaa niko on record kuwa huo ni uwizi, ni ufisadi na nimeisema hadharani na ndani ya Bunge na Bado ninaiosema hadharani. Nimeeleza siku zote so long as mfumo haujarekebishwa nitaendelea kupokea na mimi, tofauti ni kuwa upinzani tunatumiaje fedha hizo. Upinzani hatuzitumii kujengea maghorofa (kama kuna mwenye ushahidi auweke hapa jamvini na kwenye vyombo vya habari kwa Dr Slaa wengine sitaki kuwasemea). Mapambano haya ndio yatarejesha heshima ya nchi na fedha nyingi zilizotumika vibaya kwa kukopa kodi siyo ya Dr Slaa na Chadema. Nchi imeoza na radsilimali za Taifa zimeteketea na zinaendelea kuteketea. Iwapo haya yote yatafanyika, na Chadema itaridhika, iko tayari kulipa viwango vyote ambavyo Chadema haijalipa na inapaswa kulipa kwa mujibu wa sheria. Hili ni jambo la kisheria na halihitaji ushabiki kama ambavyo TRA, magazeti ya Serikali na wapambe wao wanavyotaka kuonyesha. Dr Slaa na Chadema kwa hili hatuna kigugumizi chochote. Tunashukuru kwa TRA na Magazeti ya Serikali na uhuru kutusaidia kuwasha moto, mapambano ndio sasa yameanza. Ninawataka sasa TRA waharakishe kuiletea Chadema Taarifa yetu ili tuanze kazi rasmi. Naomba radhi kwa kutoa kwa kirefu lakini nadhani inahitajika kuondoa ushabiki na upotoshaji usio na maana.

CHAMA cha CHADEMA, ambacho kinadaiwa kukwepa kulipa kodi halali za serikali, kimeshindwa kutoa taarifa za mapato kwa kile kilichodaiwa kumbukumbu zimepotea.Badala yake, CHADEMA imetoa taarifa ya hesabu za mikoa mitatu ya Kilimanjaro, Arusha na Dar es Salaam, za kuanzia mwaka 2007 hadi 2010, huku ikidaiwa kutolipa kodi tangu kuanzishwa kwake.Kutokana na hilo, CHADEMA iko katika hatari ya kudaiwa mamilioni ya shilingi na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ambayo imeanza kufanya uchunguzi wa madai hayo. Habari za kuaminika ndani ya TRA zimesema taarifa ya hesabu za chama hicho kwa mikoa hiyo zina utata na zinaonyesha ukwepaji kodi. Katika utetezi wake kwa maofisa wa TRA, CHADEMA imedai haiwezi kukatwa kodi kwa kuwa inawalipa watendaji wake posho na si mishahara. Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, maofisa wa TRA katika uchunguzi wamebaini fedha wanazolipwa watendaji wa chama hicho ni nyingi kuliko kima cha chini cha mshahara. Sheria ya Kodi inaagiza posho yoyote inayozidi kima cha chini cha mshahara kukatwa kodi. “Taarifa zao zinaonyesha kodi hawalipi na viongozi wao wanasema hawalipani mishahara bali ni posho, lakini kisheria posho inayozidi sh. milioni moja inakatwa kodi,’’ kilisema chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya TRA. Uchunguzi wa kina uliofanywa na gazeti hili umebaini CHADEMA iliwasilisha taarifa ya fedha ambayo ina dosari. Watendaji ambao hawalipiwi kodi ni pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, anayelipwa mshahara wa zaidi ya sh. milioni 7.4, fedha ambazo ni nyingi kuliko mshahara wa mbunge.
Dk. Slaa alishawahi kuhadaa Watanzania kwa kupaza sauti akidai mshahara wa mbunge ni mkubwa hivyo upunguzwe. Kuibuliwa ufisadi huo ndani ya CHADEMA kulimfanya Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa chama hicho, Anthony Komu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Mabere Marando kukanusha kupitia vyombo vya habari wakidai ni uongo. Komu alidai Dk. Slaa analipwa mshahara wa sh. 1,725,000 na lita 1,000 za mafuta kila mwezi, wakati waraka ambao Uhuru inao unaonyesha mamilioni ya fedha yanayochotwa na mtendaji huyo. Viwango hivyo ni mwendelezo wa mapendekezo ya posho ya Dk. Slaa kama Azimio la Kamati Kuu iliyokutana Januari 29 na 30, mwaka huu, mjini Dar es Salaam na kuonyesha kuna tofauti kubwa na maelezo waliyotoa Komu na Marando. Kwa mujibu wa waraka huo ambao hauonyeshi kiwango kinachokatwa kodi, posho ya Dk. Slaa imegawanywa katika sehemu sita ambazo ni posho ya mwezi, fedha za mafuta, majukumu, viburudisho, nyumba na utendaji kazi. Wakati Komu katika ufafanuzi wake alisema Dk. Slaa analipwa mshahara (basic) wa sh. 1,725,000 waraka unaonyesha analipwa sh. 2,300,000. Mbunge analipwa sh. 2,305,000 kabla ya kukatwa kodi. Kwa upande wa posho, Dk. Slaa analipwa fedha za mafuta sh. 1,387,500 kwa wastani wa lita 750 kwa
mwezi, huku fedha za majukumu zikiwa sh. 575,000, mawasiliano sh. 460,000 na nyumba sh. milioni moja. Posho nyingine ni kwa ajili ya viburudisho sh. 462,500 na utendaji kazi sh. 989,000. Mshahara huo umefanywa maalumu kwa Dk. Slaa pekee na iwapo chama hicho kitapata katibu mkuu mwingine hawezi kulipwa hivyo. Dk. Slaa anadaiwa kupata posho ya nyumba mara mbili, kwani ilipendekezwa alipwe sh. milioni 40 ili kukamilisha ujenzi wa nyumba yake eneo la Mbweni, nje kidogo ya mji wa Dar es Salaam, ambako anaishi kwa sasa. Hata hivyo, licha ya kulipwa fedha hizo Dk. Slaa ameendelea kupewa posho ya nyumba ya sh. milioni moja kila mwezi.

Source: Gazeti la Uhuru, Juni 8,2011

KAZI KWELI KWELI CDM
 
Magamba mtafuta kila njia kutoka mdomoni mwa mamba kweli mmeishiwa hoja mtatumia kila hila kuichafua cdm mtashindwa "changes coming tomorrow never avoid if deniy ask mubbarack".
 
Vijana wa Nape wapo kazini, Vilaza wakubwa. wanaachia madini bure kwa wazungu wanakuja kujadili posho za wakombozi wa nchi hii, hawana akili
 
Tunataka taarifa ya ccmmakamba alikuwa analipa kodi kiasi gani?, hizo mbinu za kudhoofisha upinzani hazitashinda, na badala yake mnazidi kujichimbia sehemu mtakako zikwa
 
Mafilili.
i) Kodi haidaiwi kwenye magazeti, TRA walitakiwa kuleta Hati ya Madai Chadema, na baada ya Hati hiyo wanaenda Mahakamani. Ndiyo hasara ya ushabiki, lakini sishangai Gazetti lenyewe Uhuru Mali ya Chama cha Mafisadi na kuwadi wa Mafisadi.
2) TRA walifika CHADEMA. Waliahidi watarudi Chadema kutoa Taarifa yao. Hadi leo hawajaonekana. Huu ndio ushahidi wa chombo kinachotakiwa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria lakini kinatumika kisiasa, na kulinda ufisadi ndani yake kwa propaganda zisizo na msingi.
3) Hoja ya msingi ni:-
a) Waziri Mkuu anatakiwa kulieleza Taifa hili kwanini Bwana Luoga hajachukuliwa hatua za kisheria na kinidhamu hadi leo wakati nilimwandikia toka mwaka 2008. Hiki ni kiashiria jinsi Serikali inavyolinda ufisadi, ubadhirifu, na uwizi wa Mali ya umma. Waziri Mkuu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali TRA wote wanajua jinsi Taifa lilivyoingizwa hasara ya Millioni 550 kwa kushikilia magari ya Tango Transport kwa siku 90 (kwa makosa ambayo hata yangelikuwepo-na bado hayakuwepo ndio maana alilipwa shs 53 Millioni na hati,maye interest ya 550 Millioni). Pili Masdai ya Tango Transport ya kushikilia Kadi ya magari Semi Trailer na Magari yenye Trailer na mengine madogo kwa zaidi ya miaka 10 kinyume na sheria. Uzembe wa mtumishi wa Serikali haiuwezi kuachiwa kufilisi wazalendo na wao wakaendelea tu kula kuku kwa mrija. Luoga anategemewa kustaafu katikati yamwezi huu (Juni 2011). Hatutakubaliana Luoga alipwe mafao yake na joto la jiwe linamsubiri punde.
b) TRA inapaswa kueleza na kuweka hadharani kama wanavyofanya kwenye vyombo vya uhuru na magazeti ya Serikali hela hiyo iliyolipwa na inayotakiwa kulipwa kwa Tango Transport ni kiasi gani, "hata ingelikuwa kweli na kodi wanayodhani Dr Slaa hakulipa( ikumbukwe, Dr Slaa amelipa kodi kipindi chote cha Ubunge, labda waseme hakulipa na iwapo ni hibvyo lazima waliambie Taifa zaidi shs 360,000 nilizokuwa ninakatwa kwa mwezi zilikuwa zinaenda wapi?) ikilinganishwa na mabilioni aliyolipwa na anayotakiwa kulipwa Tango Transport (na wengine ambao bado ninakusanya taarifa zao)
4: Nimekwisha kutamka iwapo TRA wanadhani chadema haijalipa kodo toka 1992 hadi leo basi walete hati ya madai tuone wanadai nini na ni kiasi gani au waende Mahakamani kudai iwapo wanadhani kuleta Chadema hati hizo ni ngumu. Sheria inawaruhusu kwenda mahakamani, tukutanie kule.
5: Nimekwisha kusema, iowapo wataleta hati ya madai Chadema, kwanza watangaze kwenye vyombo vya habari ili watanzania wote wajue,:-
a) Mishahara/posho zote za viongozi wote wa vyama vya siasa ikianzia na CCM (ambao wanalipa posho hadi wilayani) tujue wamelipa kiasi gani tangu 1992 kwa majina ya viongozi wote. Hii ni pamoja na Wenyekiti na Makamu wenyeviti wote.
b) Mishahara na posho zote za Wabunge, Makatibu wakuu wa Wizara, Viongozi wakuu wote wa TRA, Makamishna mbalimbali na watendaji wakuu wote wa Taasisi zinazojitegemea. Kwa Taarifa niliyo nayo kuna ufisadi mkubwa katika eneo hili, na kwa Taarifa ya WanaJF wabunge, akiwemo DR Slaa posho zaidi ya 5 million kwa mwezi) zilikuwa haziingii kwenye payroll na mbunge alikuwa anakutana nayo tu benki. Dr Slaa niko on record kuwa huo ni uwizi, ni ufisadi na nimeisema hadharani na ndani ya Bunge na Bado ninaiosema hadharani. Nimeeleza siku zote so long as mfumo haujarekebishwa nitaendelea kupokea na mimi, tofauti ni kuwa upinzani tunatumiaje fedha hizo. Upinzani hatuzitumii kujengea maghorofa (kama kuna mwenye ushahidi auweke hapa jamvini na kwenye vyombo vya habari kwa Dr Slaa wengine sitaki kuwasemea). Mapambano haya ndio yatarejesha heshima ya nchi na fedha nyingi zilizotumika vibaya kwa kukopa kodi siyo ya Dr Slaa na Chadema. Nchi imeoza na radsilimali za Taifa zimeteketea na zinaendelea kuteketea. Iwapo haya yote yatafanyika, na Chadema itaridhika, iko tayari kulipa viwango vyote ambavyo Chadema haijalipa na inapaswa kulipa kwa mujibu wa sheria. Hili ni jambo la kisheria na halihitaji ushabiki kama ambavyo TRA, magazeti ya Serikali na wapambe wao wanavyotaka kuonyesha. Dr Slaa na Chadema kwa hili hatuna kigugumizi chochote. Tunashukuru kwa TRA na Magazeti ya Serikali na uhuru kutusaidia kuwasha moto, mapambano ndio sasa yameanza. Ninawataka sasa TRA waharakishe kuiletea Chadema Taarifa yetu ili tuanze kazi rasmi. Naomba radhi kwa kutoa kwa kirefu lakini nadhani inahitajika kuondoa ushabiki na upotoshaji usio na maana.
Mkuu umeeleweka,ila kunabaadhi ya mjuha watakuja muda si mrefu na kuanza kazi yao ff.............
 
Ikiwa hivi tu bado hawajakomaa wanakwepa kodi, jee wakikomaa itakuwaje? Ikiwa mambo yenyewe ndio haya, nawaomba TRA wafatilie na biashara binafsi za hawa makada na wadau wa cdm, kwani tabia mbaya huanzia nyumbani ati, haina haja ya kuwa scientist kulijuwa hilo.
 
Hivi yale mapambo ya kampeni za ccm yaliombewa msamaha!
 
Ikiwa hivi tu bado hawajakomaa wanakwepa kodi, jee wakikomaa itakuwaje? Ikiwa mambo yenyewe ndio haya, nawaomba TRA wafatilie na biashara binafsi za hawa makada na wadau wa cdm, kwani tabia mbaya huanzia nyumbani ati, haina haja ya kuwa scientist kulijuwa hilo.

Bibi wa pumba umeingia, karibu. tabia mbaya huanzia nyumbani mbona we umeanza humu JF kwa kumegwa na mods? itabidi TRA wakuchunguze na wewe kama unalipa kodi kwenye biashara yako na mods.
 
Join Date : 28th April 2011
Posts : 176
Thanks 5 Thanked 22 Times in 14 Posts

Rep Power : 21
Napita tu!
 
Wewe mawazo yako mgando, hauwezi kuamini habari sharti itolewe na TZ Daima pekee!

Join Date : 28th April 2011
Posts : 176
Thanks 5 Thanked 22 Times in 14 Posts

Rep Power : 21

Napita tu!!!!
 
Hii exercise ni nzuri sana kufanyika!ifanyike kwa vyama vyote vya siasa!na sio CDM peke yake!tunaweza kujikuta tunapata pesa za kutosha kujenga fly over walau moja pale ubungo!manake CCM kwa miradi walio yano itakua ni ma bilion kodi yake.
 
Back
Top Bottom