TRA yajipanga kudai mabilioni CHADEMA

Hivi hawa hawajui Dr wa ukweli ni rais wa moyoni wa watz?? Na hapo kama wanaguswa marais waanze na yule wa magamba. Je analipa kodi katika mshahara wake, na hayo marupurupu mengine ni kiasi gani? na je anayalipia kodi au zinakusanywa ili ale na riz 1? Bado vitu vyote anapewa bura hata akisafiri popote kila kitu anagharimiwa !!! Mkiendelea tunaandamana kutaka mshahara na marupu rupu yote hayo yawekwe wazi. Halafu tuambiwe ccm status yao ya kodi iko vipi.
 
Ccm nao watoe, panga lisikate sehemu moja tu panga hili hili litumike kukata kote kote tuone
 
Tupo hapa kinondoni mbona hatuwaoni? Kwani TRA hawana ofisi? Je TRA hawaijui ofisi ya CDM? Waambieni waje sie tupo tunawasubiri. Wao walikuwa wapi miaka yote hiyo? kama ndivyo wanavyofanyakazi basi nchi hii inamatatizo makubwa.
 
kama hawajalipa kodi kwa miaka yote 19 maana yake tra kuna makosa makubwa kiasi kwamba inabidi mamlaka yote ivunjwe iundwe upya.na hii tabia ya kutekenya ndipo uanze kazi nsons imeshamiri sana kwenye utawala wsa kikwete.
1.posho mbili za wabunge.
2.kesi ya jeri muro.
3.kodi za chadema.
HITIMISHO.
TUNAIOMBA MAMLAKA YA MAPATO ITUCHAPISHIE TAARIFA YA ULIPAJI KODI YA CCM TOKA MFUMO WA VYAMA VINGI VIANZISHWE KWENYE GAZETI LA UHURU,MZALENDO,TBC NA HABARI LEO.
 
kama kweli wamekwepa ushuru basi walipe, na hilo lisiishie chadema tu, bali hata vyama vingine including ccm na tutaanzia ada za maegesho ya magari, biashara zingine nk
 
Nafikiri hapa kuna tatizo kubwa, kama huu ndio utendaji wa TRA! basi ndio maana mashule hayana madawati, hospital hakuna dawa, vitanda, mishara duni kwa watumishi, kila kitu hovyo! hapa mwenye tatizo sio Chadema wenye tatizo ni TRA wewe miaka yote umekaa kimya then umeumbuliwa ndio unakurupuka oo na nyie hamlipi kodi!,

Sasa mimi naomba yafuatayo?

tunaowataalam wa kodi nje ya TRA ambao ni wazalendo wa kweli wa nchi hii, waunde tume wafanye ukaguzi wa matumizi na mapato ya Vyama vyote tangu mfumo wa vyama vingi urejeshwe nchini na watupe report, nafikiri watu watazimia wakiona ile ya chama cha magamba.

Kama kampuni za madini ambazo zinaiba madini yetu zimesamehewa kodi! sasa inakuwa ajabu kwa chama kinachotetea maslahi ya mtanzania!? sio nia yangu kuhalalisha Chadema kutolipa kodi ila TRA wawajibike kwa kutowafuatilia kwa muda wote huo kama hawana msamaha wa kodi kama ccm.(najaribu kufikiri Barrick ya canada kwa manufaa ya canada hawalipi kodi, Chadema ya TZ kwa manufaa ya MTZ washupaliwa na Kodi)

Halafu asiyelipa kodi ni Chadema au Dr Phd Slaa!?, mimi naona kuna watu wanamtafuta Dr kumchafua kwa udi na uvumba, sisi wananchi tunasema Dr hachafuliki, ameshajenga heshima yake, na hayo mnayosema ni mambo madogo sana na ni yakawaida kwa binadamu yoyote, sisi tunachoangalia ni mchango wake kimawazo kwa taifa hili.

Dr Slaa, sisi watanzania, tunakuamini na tutaendelea kukuamini pamoja na hila zote hizi za chama cha magamba na mimi naomba wafanyie uchunguzi mkubwa TRA halafu waelimishe wanachi jinsi hawa jamaa wavyochangia nchi hii kuwa maskini.
 
Umetumwa na NAPE haya nenda ofisi za CCM ukachukue posho naona umemaliza kazi ulichotumwa na NAPE
 
Hii ndio Tanzania, zaidi ya uijuavyo, yaani haishi vituko. Mosi, gazeti la Uhuru ndio limekuwa Afisa Habari wa TRA? Pili, TRA walikuwa wapi mpaka Chadema ikakwepa kodi kwa miaka 19? Tatu, rekodi ya ulipaji kodi ya CCM iko wapi? Nne, TRA wameshindwa kukusanya kodi kwenye sekta nyeti ya madini, mafuta na biashara leo wanataka tuamini kuwa Chadema ndio wakwepaji wakubwa wa kodi? Tano, kwa Tanzania kodi hulipwa kutokana vipato vya uwekezaji, ajira na biashara. Kimantiki chadema haiwezi kukwepa kodi kwa sababu haifanyi biashara, haina uwekezaji na haijaariwa. Tunaposema wamekwepa kodi tuna maana gani? Ushuru wa forodha, kodi ya mapato, ushuru wa stemp, kodi ya ongezeko la thamani, kodi ya majengo, Skill and Development Levy, withholding tax? Kuhusu kodi ya mapato ya waajiriwa PAYE, mwajiriwa ndiye anayelipa kodi ambapo mwajiri ana jukumu la kukata kodi hiyo kwa mujibu wa sheria kutoka ktk mshahara na mapato mengine ya mwajiriwa na kuwasilisha TRA. Taarifa zilizopo zinaonyesha mpaka mwaka jana mwishoni chadema ilikuwa ikipata ruzuku ya sh mil. 20 hivi na baada ya uchaguzi kiasi kimeongezeka mpaka zaidi ya mil 200. Taratibu za kisheria zipo za kupambana na ukwepaji wa kodi (anti-avoidance/evasion) inashangaza kwanini hazitumiwi. TRA fanyeni ukaguzi mtoe kadirio la kodi wanayodaiwa chadema walipe kwa mujibu wa sheria. Tuache kulialia. Hitimisho, ukanjanja na ushabiki wa kisiasa unadharirisha taaluma ya habari. Kuandika chadema wamekwepa kodi bila kusema aina ya kodi na kiasi cha kodi husika ni ishara kuwa waandishi wetu wana fikiri kwa kutumia matumbo yao. Tanzania ya leo sio ya jana wala juzi, wallaah iko siku bubu atasema halafu watawala watakosa pa kushika. Mungu ibariki Tanzania.
 
Walikuwa wapi toka CDM ianzishwe. Maofisa wao wanapotajwa kuwa ni mafisadi wanalipa kisasi. Wanatumia uti wa mgongo kufikiria badala ya ubongo! Mwaka huu wataipata kwani wahisani hawatatoa pesa zao mpaka wajisafishe na kuacha kutumiwa kisiasa. Wanajisahau kuwa wananchi wanajua wanachofanya hivyo HAWADANGANYIKI TENA.

Wanatakiwa wafikiri namna ya kuongeza walipa kodi na kuondoa misamaha ya kodi sio kulipa visasi.TRA sio mali ya watu wachache ni ya Tanzania.

Labda TRA imeanzishwa mwaka huu!!
 
Sheria ya Kodi inaagiza posho yoyote inayozidi kima cha chini cha mshahara kukatwa kodi. “Taarifa zao zinaonyesha kodi hawalipi na viongozi wao wanasema hawalipani mishahara bali ni posho, lakini kisheria posho inayozidi sh. milioni moja inakatwa kodi,’’ Mbona hapo wamechanganya mambo?Mara inayozidi kima cha chini, mara inayozidi milioni moja,sasa tuelewe lipi? Hiyo inaonyesha ni jinsi gani hiyo stori ni ya kutunga cause kima cha chini cha mshahara ni sh.135,000/- na si milioni moja.UHURU NI TOILET PAPER, TUPA KULEEE.
 
Chanzo hakijawahi kuwa credible. Kwa hiyo taarifa hiyo siyo credible. Mfano majibu ya Chadema yangekuwa na uzito kama aliyeyatoa ananukuliwa sawia kwa jina na wadhifa. Inaniaminisha aliyetoa majibu hayo kwa niaba ya Chadema ni kitengo cha propaganda cha CCM.

Ili kuwe na uwiano wangetupa mfano mzuri wa ulipaji kodi wa chama kingine; hapa naamini CCM ni walipaji wazuri wa kodi za serikali basi wangetupa "uzuri" wa ulipaji kodi wao tulinganishe na wa CDM.
 
KWANI NANI ALIWAKATAZA WASIDAI HAAAA, WAKADAI NI HAKI YAOo
 
Walikuwa wapi toka CDM ianzishwe. Maofisa wao wanapotajwa kuwa ni mafisadi wanalipa kisasi. Wanatumia uti wa mgongo kufikiria badala ya ubongo! Mwaka huu wataipata kwani wahisani hawatatoa pesa zao mpaka wajisafishe na kuacha kutumiwa kisiasa. Wanajisahau kuwa wananchi wanajua wanachofanya hivyo HAWADANGANYIKI TENA.

Wanatakiwa wafikiri namna ya kuongeza walipa kodi na kuondoa misamaha ya kodi sio kulipa visasi.TRA sio mali ya watu wachache ni ya Tanzania.

Ki fupi wanatakiwa wafukuzwa kazi wote. Yaani muda waote walikuwa wapi na wakaamka sasa hivi. Tena wakati ambapo CDM inaeonekana ina nguvu zaidi nchini. Hii moja kwa moja ita tafsiriwa kama wana taka kuwakomoa. Nadhani wangetakiwa wawe- smart zaidi.

Kikwebo.
 
TRA pambaneni na cdm walipe kodi tena haraka ila tahadhari tunataka taarifa ya ulipaji kodi kwa vyama vyote na cha mfano kiwe chama chetu cha ccm, Luoga upo, ccm wawe kioo ili tuheshimiwe tusijifiche kwenye kichaka cha karanga wakati tunalipa kodi bila mashaka.

Wachambulie ni jinsi gani tulilipia magari yote yaliyoagizwa kwaajili ya uchaguzi, mabango, kanga, kofia, t-shirts nk, mwisho wawekee idadi ya waajiriwa wetu (ccm) nchi nzima na kiasi cha kodi kilicholipwa ili wajue tunachangia maendeleo ya Taifa letu kwa vitendo na si maneno matupu.

Mkifanya hivyo itasababisha chati ipande na kiasi cha kodi kinachokusanywa kitaongezeka, kwani ni hakika hicho wanachokwepa ni kikubwa kuliko wafanyabiashara.
 
mimi naunga mkono,TRA kudai wadaiwa ila yafuatayo yazingatiwe
  1. kama wana mandate ya kukagua mahesabu ya vyama vya siasa,basi huo uwe mwanzo wa kukagua vyama vyote hususan vikubwa (CUF, NCCR-Mageuzi, TLP, UDP na CCM)
  2. sioni kama ni busara kuongelea jambo hili kwenye media hususan at preliminary/investigation stage maana kwa wakati huu obvious wanaonekana kutumika kisiasa. Makampuni mangapi wanayadai kimyakimya,why CDM
  3. Je, kodi iliyokwepa na CDM ni signifivant hivyo?
 
Gazeti la magamba wambieni TRA au washaulini hao mnawatumia kuchafua cdm wakafuate kodi kwenye madini ambayo hayana faida za kusababisha vifo kwa watanzania na kuaribu mazingira.
 
Back
Top Bottom