TRA wanavunja rekodi ya mapato: Serikali haina pesa hapo vipi?

Vijijini Lawama

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
298
73
Wadau naomba kujua ni vipi serikali inakosa pesa za kuendeshea shughuli zake za kiofisi na kufanya miradi ya maendeleo kama alivosema Pinda wakati TRA inavunja rekodi yake ya ukusanyaji wa mapato? Je Vile viwanja vya ndege, mito ya maziwa na mabomba ya maziwa na asali, ujenzi wa reli, ununuzi wa ndege za kisasa, bajaji za wagonjwa kila kijiji, barabara za angani, meli za kisasa katika maziwa yetu na laptops kwa kila mwanafunzi, vitanda kwa wajawazito kwa kila nyumba yenye mwanamke n.k tutafanyaje?

Nisaidien mimi nabwabwaja sina pa kusihka tena
 
simple question simple answer kuna 'mchwa' unakula hayo mapato basi.
 
Wala hainiingii akilini, kuikubali lazima uwe na matatizo ya kifikra. Kwamba pesa iko tena wanavunja rekodi ila wale ambao kodi hukusanywa na kupekwa kwao HAWANA PESA? We are lacking strategists in this country!!!!!!
 
Nchi ya walalamikaji nilimsikia mkubwa wa TRA akisema wangekusanya zaidi kama isingekuwa vimemo wanavyolazimishwa watoe misamaha ya kodi unajuwa wamesame kwa kiasi gani kwa ripoti ya CAG ( 18%)
Sasa ndugu yangu embu tafiti uone nani wamesamehewa makampuni yote ambayo vigogo na watoto wao wana ubia na makampuni hayo ,kazi ipo kweli kweli
 
simple qn and the simple answ is:Baada ya kuona vyanzo vya kodi vimepungua kutokana na kupungua kwa uzalishaji,TRA wanajiwekea achievable targets kwa kujipunguzia malengo (projections).Na hicho kidogo anakula JK na misafara yake.
 
Swali lako linastahili jibu alilowahi kutoa Jk alipoulizwa kwa nini Tanzania ni masikini ingawa ina rasilimali nyingi sana.
"SIJUI"
 
malengo/target kiduchu, halafu wanalinganisha viwango bila kuangalia ushukaji wa thamani ya tsh
 
Nchi ya walalamikaji nilimsikia mkubwa wa TRA akisema wangekusanya zaidi kama isingekuwa vimemo wanavyolazimishwa watoe misamaha ya kodi unajuwa wamesame kwa kiasi gani kwa ripoti ya CAG ( 18%)
Sasa ndugu yangu embu tafiti uone nani wamesamehewa makampuni yote ambayo vigogo na watoto wao wana ubia na makampuni hayo ,kazi ipo kweli kweli

Jana kamishina wa KRA (KENYA) alikuwa anaagwa na raisi baada ya muda wa utumishi kwisha,yeye alisema chini yake walitafuta vyanzo vipya vya kodi ni kuifanya bajeti ya serekali yao kuwa inajitegemea sisi hivyo vyanzo vichache bado tunavisamehe kwa vimemo. Tunayo safari ndefu mbele yetu!
 
Ni mambo yako waz jamani,Arumeru kwa harakaharaka walitapanya kias gani cha pesa??je zilitoka wapi??? Suala la kutuambia serikali haina pesa ni kiini macho tu!!!! pesa zipo na kwa manufaaa ya wachache!!! Leo hii ukiamrishwa uchaguzi wowote wa mbunge,utaona kwa jinsi vigogo na makada wa magamba watakavyotapakaa mtaani na pesa za kurubuni wananchi!!! je hizo zinatoka wapi??? ole wao,siku inakuja,watalia na kusaga meno!!!
 
Nchi ya walalamikaji nilimsikia mkubwa wa TRA akisema wangekusanya zaidi kama isingekuwa vimemo wanavyolazimishwa watoe misamaha ya kodi unajuwa wamesame kwa kiasi gani kwa ripoti ya CAG ( 18%)
Sasa ndugu yangu embu tafiti uone nani wamesamehewa makampuni yote ambayo vigogo na watoto wao wana ubia na makampuni hayo ,kazi ipo kweli kweli

kweli mkuu hilo unalosema lina ukweli na hawa jamaa wanatuchezea akili bt iko siku haya yote yatafahamika.
 
Jana kamishina wa KRA (KENYA) alikuwa anaagwa na raisi baada ya muda wa utumishi kwisha,yeye alisema chini yake walitafuta vyanzo vipya vya kodi ni kuifanya bajeti ya serekali yao kuwa inajitegemea sisi hivyo vyanzo vichache bado tunavisamehe kwa vimemo. Tunayo safari ndefu mbele yetu!

Wakenya ni wabunifu sana, na hawana lelema katika mambo ya kazi-wanafanya kazi as if there is no to-morrow!
 
Mkulo ni bingwa wa KANYABOYA, hapo alikuwa anapoza wale waliolalamikia TRA kuwa haifanyi kazi nzuri, fuatilia kama hiyo record collection ipo kweli?! Kumbuka hata EPA tuliambiwa kuna fedha ilirudishwa but hadi leo hakuna anayejua ziko wapi.
 
Back
Top Bottom