abuuzahraa
Member
- Aug 13, 2009
- 24
- 9
Kaka wala usipate tabu TRA inauwezo (Caspacity) ya kuwashughulikia hao watu Tatizo ni kuwa Haipati ushirikiano wa Kutosha (Rushwa ni Siri). Kwa taarifa yako na Umma ni kuwa Mamlaka ya Mapato inacho kitengo kinaitwa "Internal Affairs" Kazi yake ni Kufanya uchunguzi (Investigation) kwa Tuhuma zote zinazohusiana na Maadili na Utendaji kazi wa Watumishi wake. Kitengo kina wachunguzi mahiri na kimeshafanya kazi zilizoathiri ufanisi na katika masuala ya Maadili ndani na nje ya mamlaka kinatambuliwa sana.NAMNA YA KUWASILIANA NA KITENGO:ili kukipa kitengo meno na Uhuru katika chunguzi zake kitengo kinapata maelekezo kutoka kwa Kamishna mkuu wa TRA na kitoa ripoti zake kwake. Kama unalo shitaka tuhuma tuma kwa barua kwa KAMISHNA MKUU MAMLAKA YA MAPATO TANZANIADar es salaam Tanzania Box 11491 +255222116453 +255222138866