TRA na mfumo mpya wa kufanya valuation of Used Vehicles

Thats why naichukia ccm, wao ndio wanao pandikiza mifumo ya kipuuz, ili wamnyonye m2 wa chini wakat huko nyamongo, mereran, na wawekezaj wengine wakipewa msamaha wa kodi, tanzania sijui inaenda wap
 
Napenda kushukuru kwa aliyetuma hizi attachment, naomba kila mdau atulie na kujaribu kuzisoma, kuzielewa na kutumia naona kwangu mimi taxes zipo fair kikubwa hapa ni kujua source and authenticity ya hizo attacment kwani zinaweza kuwa nzuri hapa alafu ukiaenda TRA ukakutana na kitu kingine. iwapo hii info imetoka TRA basi naweza kusema haiko vibaya, hapa wanajaribu kuwabana wala rushwa kwa overestimate FOB prices kama ambavyo wamekuwa wakifanya siku za nyuma. Wadau naomba na mwingine ajaribu kama nilivyofanya ili kupata uhakika na tuendelee na mjadara huu kwani wanunuzi wa magari siku hizi ni wengi.
 
Kama hujaipata hii basi jiandae!!!!!!

Tarehe 1 July 2011 TRA wanaplan kuintroduce system yao mpya kwa ajili ya valuation ya used motorvehicles...

Mfumo mpya utakuwa kama ifuatavyo...Used vehicles zitakuwa valued on either ex-factory FOB au market value in local market...

Nianze na ex factory FOB..

Kwenye mfumo hu, TRA wataestablish database itakayo kuwa na bei za magari kipindi yameingizwa sokoni kwa mara ya kwanza...labda nitoe mfano mana kidogo ina mahesabu

Mfano: Mtu akiagiza gari aina ya Toyota Premio 2001 model..hapo ina maana hii gari imezidi miaka kumi tokea itengenezwe...kwa hilo bei pungufu itakayoruhusiwa ni asilimia 70% ya bei ilipoingia sokoni kwa mara ya kwanza..PREMIO bei yake ya awali sokoni ilikuwa USD 40,000 kwa huko Japan...

Kwa maana hiyo FOB ex factory itakuwa USD 40,000 toa 28,000 (70% of USD 40,000) = USD 12,000 na hiyo ndo itakuwa Customs Value ambayo itakuwa subjected kwenye Import Duty, Excise Duty, VAT na uchakavu (kama upo)....

Kwa namna hiyo kodi jumla itakuwa kama ifuatavyo

Import duty (ID)=0.25*12,000
Dumping Fees (DF) =0.2*(12,000+0.25*12,000)
Excise (E) =0.1*(12,000+0.25*12,000)
VAT= 0.18* (12,000+ID+DF+E)

Hii ni tofauti na bei za sasa ambazo weza kuagiza premio ya mwaka 2001 kwa CIF ya USD 3,000 to USD 3,500...na kodi ingekuwa kama ifuatavyo
ukiweka na uchakavu

Import Duty (ID)=0.25*,000
Dumping Fees (DF) =0.2*(3,000+0.25*3,000)
Excise (E) =0.1*(3,000+0.25*3,000)
VAT= 0.18* (3,000+ID+DF+E)


Market Valuation Method

Kwa market value method watachukua bei za sokoni Tanzania na kutoa profit margin ya asilimia 25 na kutoa gharama za kodi zilizolipiwa ili waweze kupata CIF kipindi gari linaingia nchini...Mfumo huu utatumika pale tu ambapo bei halisi wakati gari linaingia sokoni kwa mara ya kwanza itakuwa ni vigumu kujulikana...

My take:
Je hii ndiyo njia ya kupunguza foleni za magari Dar? na je vipi kule ambapo bado kuna shida ya usafiri itakuwaje?
 
Mkuu kweli inashangaza sana! Kwa vigezo hivyo wanataka kusema kwa mfano gari Cresta la mwaka 2000 lilotembea km 12,000 ni sawa na gari hilo hilo lilotembea km186,000! Au lilopatwa na ajali.


Huu ni ujinga, they should go back to the drawing board!
 
mtu aliyeleta huu mfumo anatumia akili kweli au anamatope humo kichani kwake. Hata sizani anajua mambo muhimu ya kuzingatia ukinunua gari lililotumika.
 
hiyo ndo wameona njia ya kuongeza mapato badala ya kubuni vyanzo vipya yahani wamekaa tu pale na nothing new to them na wanapokea mishahara mikubwa for nothing. Ilitakiwa wawe na kitengo cha research kwa ajili ya kuangalia opportunities za vyanzo vipya na sio kuzidi kuwapandishia gharama za maisha wananchi.
 
TRA kwa hili hapana: Hembu pambukeni kimawazo na kutengeneza mipango ya kisasa ya ukusanyaji kodi, ili kwamba hata yule mwenye Biashara ndogo, aweze kulipa hiyi kodi ndogo.

Hembu jifunzeni kwa Mzee Bharesa anayeuza maji ambayo hata mtu mwenye kipato kidogo kabisa anaweza kuyanunua na kunywa (Tsh. 100).

Hii kitu mnaita "Tax Mordenization Programme" ndiyo hayo madudu? Kitillya hii kwa kweli haina maana!
 
Navoona wanataka kudhibiti uingizaji wa magari nchini, kwa sasa imekuwa fujo sana
 
Tutapitisha gari Kenya au Uganda na kutumia usajili wao, kwani hata madini mengi yanapitia huko sababu ya ukiritimba wetu. Naipenda East Africa commuty
 
hiyo ndo wameona njia ya kuongeza mapato badala ya kubuni vyanzo vipya yahani wamekaa tu pale na nothing new to them na wanapokea mishahara mikubwa for nothing. Ilitakiwa wawe na kitengo cha research kwa ajili ya kuangalia opportunities za vyanzo vipya na sio kuzidi kuwapandishia gharama za maisha wananchi.

Hapo wamechemka, kwani Hamna atakaye agiza GARI tena na hayo MAPATO YATASHUKA, hii kitu ukiiangalia sana inafaidisha watu wenye UWEZO watu wengi walikuwa wanchukua mikopo maofisini kwao na kuagiza magari na ukichunguza wengi mishahara yao na uwezo wa kupata mkopo ni kati ya 10,000,000/= na 15,000,000/= sasa hapo hali itakuwaje? Maana kwa mkopo huu mtu ulikuwa unauwezo wa kununua saloon CAR yako na chenji ukanunua KIWANJA.
Kilicjhobaki Magari basi twendeni TUKAJENGE na kununua VIWANJA.
 
Navoona wanataka kudhibiti uingizaji wa magari nchini, kwa sasa imekuwa fujo sana

Wadhibiti hivyo wakiamini kwamba usafiri wa umma upo madhubuti lakini sivyo hali ilivyo sasa hivi,hii ni dalili ya kutengeneza matabaka ya walio nacho na wasio nacho ambapo ni hatari kubwa kwa usalama wa nchi yetu haswa wasiokuwa nacho wanapoendelea kuongezeka...

Na pia uingizaji sio fujo ni mindombinu mibovu ndio inayosababisha kuonekana gari nyingi barabarani..
 
Hili suala lilishaletwa hapa jamvini wiki jana kama skosei. Hawa mabwana wa TRA ni kama Magamba , vichwani wamejaza MAKAMASI. Wao wanadhani Tz ni Dar es Salaam tu, wanasahau kwamba kule vijijini hata hizo barabara tu ni shida achilia mbali magari. Sasa sijui wanapata wapi audacity na kiherehere cha kudhibiti uingizaji magari wakati mafuta watu wananunua wenyewe, mabarabara ya HOVYO na sio kwamba hapa Tz tuna kiwanda cha kutengeza magari ambacho tunakilinda. Hawa watu ni majuha sana.
 
Navoona wanataka kudhibiti uingizaji wa magari nchini, kwa sasa imekuwa fujo sana

Siyo fujo, population ya watanzania imekuwa kubwa pasipo miundombinu ya barabara, wavivu wa kufikiri wanadhani hiyo ndo solution. Kitakachotokea ni wananchi kuwa na hasira kwa serikali ukija uchaguzi watatupiliwa mbali!

Kitilya anatumiwa na wanasiasa wanaotumia matumbo kufikiri, kum-drive watakavyo. Usafiri wa punda na mikokoteni utarudi.
 
Wadhibiti hivyo wakiamini kwamba usafiri wa umma upo madhubuti lakini sivyo hali ilivyo sasa hivi,hii ni dalili ya kutengeneza matabaka ya walio nacho na wasio nacho ambapo ni hatari kubwa kwa usalama wa nchi yetu haswa wasiokuwa nacho wanapoendelea kuongezeka...

Na pia uingizaji sio fujo ni mindombinu mibovu ndio inayosababisha kuonekana gari nyingi barabarani..

Usafiri wa umma wenyewe hivi una exists?? mi naona tu kila mtu anaishi kibahati bahati very close to anarchy. Hivi kweli Tz tunaeza kusema tuna public transport? tuna takwimu zozote za magari, abiria, muda wa safari n.k?
 
duh! Tutanunua magari kweli????
Hata hao wanaobuni upuuzi kaa huu pengine wanadhani wao hawataguswa na haya maamuzi. Ni kweli huenda hivi sasa wanaendeshwa na magari ya serikali, au wanajua wapi watapenya wakiagiza magari yao huko, lakini with time itafika wakati watastaafu au wataachishwa kazi kipato kitayumba au connection zitakwisha hapo ndio watapojua uchungu wa mkuki wanaounoa hivi sasa.
 
Mkuu kweli inashangaza sana! Kwa vigezo hivyo wanataka kusema kwa mfano gari Cresta la mwaka 2000 lilotembea km 12,000 ni sawa na gari hilo hilo lilotembea km186,000! Au lilopatwa na ajali.
Huu ni ujinga, they should go back to the drawing board!
Kweli kabisa hapa wamechemka..!!
 
Back
Top Bottom