Tra mbeya lawamani

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,710
2,226
[h=2]Maaskofu waitupia lawama TRA kwa kodi kubwa[/h] Na Thobias Mwanakatwe

27th November 2011









Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro

Maaskofu, Wachungaji na wanataaluma mkoani hapa wameishitaki kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mbeya kwa kuwakimbiza wafanyabiashara kuwekeza katika mkoa huo kutokana na kuwatoza kodi kubwa na kusababisha wakimbilie mikoa mingine.
Walisema hayo juzi wakati wa kongamano la kujenga mkakati wa maendeleo ya mkoa wa Mbeya waliloliandaa na kuwashirikisha viongozi wa dini na wananchi ambalo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Kandoro alikuwa kama mgeni rasmi.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Dayosisi ya Konde, Dk.Israel Mwakyolile, akisoma maazimio ya maaskofu na wachungaji katika kongamano hilo, alisema TRA mkoa wa Mbeya amekuwa kikwazo kikubwa kwa wafanyabiashara.
Dk. Mwakyolile alisema watu wanajitahidi sana kufanya biashara katika mkoa wa Mbeya lakini wanakatishwa tamaa na TRA ambayo inawatoza kodi kubwa hali ambayo inawafanya wafanyabiashara kukimbilia katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Dar es Salaam ambako kodi inakuwa ya kawaida ukilinganisha na Mbeya ambako ipo juu.
Dk. Mwakyolile alisema TRA Mbeya lazima watambue kuwa biashara ni chanzo kikuu cha ajira kwa vijana hivyo wafanyabiashara wakubwa wanapoanza kuukimbia mkoa vijana nao watakosa ajira na matokeo yake watajiingiza katika makundi yasiyofaa na kusababisha mkoa kutokuwa na amani.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Kandoro akijibu hoja hiyo aliwaahidi maaskofu hao kwamba atakaa na Maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Mbeya kujadiliana suala hilo.
Kwa muda mrefu TRA Mbeya imekuwa ikilalamikiwa na wafanyabiashara wa mkoa huu ambao walishatoa tishio la kuacha kupitisha mkoani hapa bidhaa zao yakiwemo magari wanayoyanunua toka nje kutokana na Mamlaka ya Mapato Mkoani Mbeya (TRA) kuwatoza kodi kubwa ambayo wakati mwingine inazidi thamani ya bei waliyonunulia vitu hivyo toka nje.
Walisema maofisa wa TRA waliopo kitengo cha forodha wamekuwa wakiwatozwa kodi kubwa kila wanapoingiza bidhaa hususani magari kutoka nchi za Malawi, Zambia na Afrika Kusini hali ambayo inawafanya wapate hasara katika biashara zao.
Mmoja wa wafanyabiashara hao Protence Mpora alitoa mfano kuwa mwezi Januari mwaka huu aliingiza magari mawili yaliyotumika kutoka Malawi lakini kiwango cha kodi alichoambiwa atoe ni kikubwa sana ukilinganisha na bei aliyonunulia.
Mpora alisema tangu Januari amekuwa akifuatilia kuomba apunguziwe kodi hiyo lakini maafisa wa TRA wameshilia msimamo wa kutaka kiwango cha kodi walichomkadilia akitoe na kumtishia kuwa asipolipa watayataifisha magari hayo.
Meneja wa kanda wa TIC, Daudi Riganda akizungumza wakati wa semina ilitoandaliwa na TIC kuwatambulisha wafanyabiashara utendaji kazi wa kituo hicho ambayo ilifanyika mjini Vwawa wilayani Mbozi alisema tangu afike mkoani Mbeya amekuwa akipokea malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara juu ya utendaji wa baadhi ya maafisa wa TRA ambao wamekuwa wakiwaona wafanyabiashara kama adui zao.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
Kinahitajika kikao cha pamoja kati ya wafanyabiashara na TRA vinginevyo uchumi wa Mbeya utaendelea kudorora. Na inashangaza kuona kwamba kilio hiki ni cha siku nyingi na hakuna hatua madhubuti zilizokwisha chukuliwa.

Ni vyema pia hao TRA wakawa na wazo kuwa bila wafanyabiashara watakuwa hawana la kufanya hivyo wafanyabiashara ni wateja na sio maadui zao.
 
Back
Top Bottom