TRA hii ni haki?

Watunduru

Senior Member
Dec 29, 2011
170
39
Naomba kuelimishwa,mamlaka ya mapato ktk kukadiria kodi wajasiriamali kwa mwaka huu wa 2012-2013,hapa ktk wilaya ya tunduru,wanahitaji bank statement ya mwaka uliopita na kwamba makadirio yate yatatokana na pesa iliyoingia na kutoka bank kwa kipindi chote cha mwaka uliopita bila kujali kwamba kuna pesa ambazo hupitia ktk akaunti kwa sababu moja ama nyingine lakini haziwahusu wenye akaunti.sasa kutumia bank statement kama kigezo cha makadirio ni haki,sheria,au kuwakomoa wajasiriamali?
Nawasilisha.
 
wezi na mifumo yao mibovu...wamo humu humu jf wanaona aibuu
yaani ukiwa mlipa kodi unakuwa adui yao wanakutafutia vijisababu,ila ukiwa mkwepaji wanakufurahia ili wakuvute
 
TRA hawana tofauti na Trafic wanaoshika tochi barabarani kucontrol speed!
 
Kama unatunza kesabu zako za biashara vizuri na hauna ubabaishaji hauna sababu ya kuonesha account yako ya biashara au ya binafsi kwani itaonesha hizo pesa zilivyoingia na hata kama ni za watu wamepitishia kwako itaonesha tu. Au unafanya money laundering? kwanini uruhusu watu wengine watumie akaunti yako? na kwanini uogope kuionesha? hapa kuna walakin hapa.
 
Kama unatunza kesabu zako za biashara vizuri na hauna ubabaishaji hauna sababu ya kuonesha account yako ya biashara au ya binafsi kwani itaonesha hizo pesa zilivyoingia na hata kama ni za watu wamepitishia kwako itaonesha tu. Au unafanya money laundering? kwanini uruhusu watu wengine watumie akaunti yako? na kwanini uogope kuionesha? hapa kuna walakin hapa.

mkubwa,wao wameshaweka sharti la bank statement bila kujali kama umetunza vema hesabu ama la,cha ajabu afisa wa tra anaonyesha wivu na chuki ya wazi kwa mfanya biashara kiasi kwamba ni kama kukomoa flani,na pia swali la mtu kupitishia pesa ktk akaunti ya mtu ni la kawaida sana hasa kwa watu walio nje ya tunduru na ambao wanatumia benki tofauti na nmb.ikumbukwe kwamba tunduru kuna benki moja tu-nmb,japo kilio kikubwa cha wananchi ni kuwa na benki mbadala kutokana na maumivu wanayopata toka nmb.inafikia hata kupata mkopo ni lazima uwahonge maafisa mikopo.kwa kweli hali ni ya kuhuzunisha mno.
 
mimi nadhani katika kutizama bank statement huonyesha kila transaction ilifanyikaje na tarehe! Ni vyema lakini tra wakaliangalia hili kwani iwapo kuna bank moja tu huko, ama kwa hakika mtateseka sana! Na hiyo jam ikoje huko?
 
Tatizo liko wapi

Kama watatumia hiyo account kufanya makadirio basi fungua account nyingine ya biashara ili Pesa za biashara ziwe za biashara na uwe mwaminifu kwa Taifa letu..


Tatizo hatufuati utaratibu tumebaki kulalamika tu Mwaka mzima malalamiko tu.

Kila utaratibu mbaya wewe unashauri nini sasa au ulitaka humu jamvini tukusaidie nini?

Sasa Tuwe tunaulizana solutions na mawazo yako kabla ya wengine humu kuchangia Kama kukukosoa tukukosoe Kama kukushauri tukushauri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom