TRA, BoT wanalipwa mishahara minene kuliko maprofesa’

Sumasuma

JF-Expert Member
Jun 23, 2011
342
110
Nora Damian
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Profesa Abdallah Safari, amesema sera mbaya za Serikali katika mishahara zimesababisha mgomo wa madaktari.

Amesema sera hizo zimesababisha mkanganyiko mkubwa katika mishahara na kuibua manung’uniko katika baadhi ya sekta na hatimaye migomo.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika katika viwanja vya Keko Magorofani juzi, Profesa Safari alisema sera hizo zimesababisha kuwe na viwango tofauti vya mishahara kwa baadhi ya watumishi wa umma.
Alitoa mfano wa watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambao alisema wanalipwa mishahara mikubwa tofauti na watumishi wengine wa sekta za umma.

“Mimi ni Profesa wa chuo kikuu lakini mshahara wangu haufiki hata Sh2 milioni lakini huko BoT na TRA kuna watu wa kada za chini kabisa wanalipwa mamilioni ya pesa,”alisema Profesa Safari.

Profesa Safari ambaye alikuwa akizungumza kwenye kampeni maalumu ya chama hicho ijukanayo kama ‘Ondoa CCM Dar’ alisema mgomo wa madaktari unaoendelea sasa ni matokeo ya sera mbovu za mishahara zilizowekwa na Serikali.

Katibu wa Chadema katika Kanda ya Dar es Salaam, Henry Kileo, alisema Serikali ndiyo inayopaswa kulaumiwa kuhusu mgomo wa madaktari na kwamba wananchi wasio na hatia ndiyo wanaoumia.

“Hao viongozi na familia zao wakiumwa wanakimbilia nje ya nchi lakini walalahoi hawana pa kwenda na ndiyo wanaoumia,”alisema Kileo.

Alisema mfumo mbaya wa utawala uliowekwa na CCM, umesababisha maisha yawe magumu na taifa kukosa mwelekeo.
“Tutapambana kudai haki zetu za msingi na tukishindwa kuwaondoa kwa kura tutatumia nguvu ya umma,”alisema Kileo.

Kuhusu kampeni hiyo, Kileo alisema ina lengo la kukiimarisha chama na kujiandaa kwa chaguzi mbalimbali..
source,gazeti,mwananchi,07/02/2012
 
"Mimi ni Profesa wa chuo kikuu lakini mshahara wangu haufiki hata Sh2 milioni lakini huko BoT na TRA kuna watu wa kada za chini kabisa wanalipwa mamilioni ya pesa,"alisema Profesa Safari.

Anafundisha chuo gani huyu profesa? Manake nijuavyo mishahara ya walimu wa UDSM miaka ya hivi karibuni imeboreshwa kwa kiasi kikubwa sana.
 
Wasomi wa chuo kikuu katika level ya PhD wanalipwa shillingi ngapi?

Senior Professor analipwa shillingi ngapi?

Kuboreshwa ni kutoka shillingi ngapi hadi ngapi?

Serikali ya CCM wakiongeza Shs 1000/= kwa mwaka juu ya 500,000 hwaachi kuita mshahara umeboreshwa.
 
Huyu prof bado anamentality za kizamani. Inabidi afanye tena research yake kuhusu mishahara. Kwa miaka hii mishara mikubwa TZ hii haipo tena B0T na TRA!!
 
Huyu prof bado anamentality za kizamani. Inabidi afanye tena research yake kuhusu mishahara. Kwa miaka hii mishara mikubwa TZ hii haipo tena B0T na TRA!!

Rejao, 'follow your heart but go with your brain' eenh! Anachozungumzia Pro.ni tofauti ya mishahara baina watumishi wa umma wenye sifa zinazofanana au vice-versa. Inakuaje afisa wa (lets say) Ewura mwenye BA awe na mshahara mkubwa kuliko afsa mwenye MA aliyeko kule wizara ya fedha na wote wako Dar? Tumie akili zenu jaman nyie kina FF japo 1/100!
 
Anafundisha chuo gani huyu profesa? Manake nijuavyo mishahara ya walimu wa UDSM miaka ya hivi karibuni imeboreshwa kwa kiasi kikubwa sana.

Hii lugha isiyoambatana na figures umeitoa wapi.
 
Anafundisha chuo gani huyu profesa? Manake nijuavyo mishahara ya walimu wa UDSM miaka ya hivi karibuni imeboreshwa kwa kiasi kikubwa sana.

Imeboreshwa na kuwa sh. ngapi? pamoja na hayo unayoyaita maboresho mshahara wa "Full Professor " katika vyuo vikuu vyote vya umma nchi ni "fixed" kati ya Tsh. 3million-3.5mil. Hakuna profesa anayepata mshahara 4 miln.
 
Huyu prof bado anamentality za kizamani. Inabidi afanye tena research yake kuhusu mishahara. Kwa miaka hii mishara mikubwa TZ hii haipo tena B0T na TRA!!

Wala hajakosea. Kwenye taasisi za serikali mishahara mikubwa ipo TRA na BOT. Kama wewe unajua taasisi nyingine iweke hapa
 
Huyu prof bado anamentality za kizamani. Inabidi afanye tena research yake kuhusu mishahara. Kwa miaka hii mishara mikubwa TZ hii haipo tena B0T na TRA!!

kweli kabisa amesahau ewura,tcra na sumatra
 
Nora Damian
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Profesa Abdallah Safari, amesema sera mbaya za Serikali katika mishahara zimesababisha mgomo wa madaktari.

“Mimi ni Profesa wa chuo kikuu lakini mshahara wangu haufiki hata Sh2 milioni lakini huko BoT na TRA kuna watu wa kada za chini kabisa wanalipwa mamilioni ya pesa,”alisema Profesa Safari.

Kwa wanaomjua Profesa Safari na outputs zake kama kweli wanamlipa hizo hela there is no value for money ilibidi alipwe chini ya hizo.
 
Anafundisha chuo gani huyu profesa? Manake nijuavyo mishahara ya walimu wa UDSM miaka ya hivi karibuni imeboreshwa kwa kiasi kikubwa sana.

imeboreshwa kwa kiasi gani? inakuwa ni basic 3m, ukichukua makato lazima zibaki 2m. wanataaluma wamepuuzwa, ndo maana wanaingia siasa
 
Hii ndio bongo viongozi wanaposema wananchi fungeni mikanda wao huwa wanalegeza.
 
Nimekuwa tu nasikia mishahara minono lakini hakuna aliyewahi kuja na vielelezo vya kutosha kila mmoja wetu anadaka maneno ya mwenzake na kufanya mjadala
 
Na huko tra,bot n.k. ndiko wanakowapeleka watoto,wajomba,mashemeji na vimada wao.
 
Back
Top Bottom