Sanctus Mtsimbe
R I P
- Jul 14, 2008
- 1,820
- 1,031
Gari ambayo ilileta misaada ya namna mbalimbali ofisi za Red Cross
Katibu Mkuu wa TPN Mzalendo Method Bakuza, akikabidhi misaada ambayo imekusanywa na TPN na Wadau wake (Jamiiforums.com na Michuzi.blogspot.com) kwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Msalaba Mwekundu Bw. Peter Mlebusi
Mzalendo Sanctus Mtsimbe ambaye ni Rais wa TPN na Meneja Mauzo na Masoko wa SimbaNET (T) Limited akisikiliza maelezo kutoka kwa naibu katibu Mkuu wa Red Cross Bw. Peter Mlebusi
Katika Misaada hiyo SimbaNET Limited ilichangia kiasi cha TZS 1,500,000 ambazo zilitumika kununua misaada hiyo. Misaada hiyo kwa upande wa SimbaNET ilikabidhiwa na Sanctus Mtsimbe, Meneja Mauzo na Masoko wa SimbaNET.
Rais wa TPN Mzalendo Sanctus Mtsimbe, akimsomea orodha ya Misaada itakayokabidhiwa ambayo imekusanywa na TPN na Wadau wake (Jamiiforums.com na Michuzi.blogspot.com) Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Msalaba Mwekundu Bw. Peter Mlebusi
Katibu Mkuu wa TPN Mzalendo Method Bakuza, leo alikabidhi misaada ambayo imekusanywa na TPN na Wadau wake (Jamiiforums.com na Michuzi.blogspot.com) kwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Msalaba Mwekundu Bw. Peter Mlebusi. Misaada iliyotolewa ni pamoja na: Ndoo 40, Magodoro 40, Sabuni Cartoon 5, Vyandarua 40, Mablanketi 200 vyote vikiwa na thamani ya TZS 1,619,000 Pia kulikuwa na misaada ya vitu mbalimbali kama nguo nyingi sana, viatu, vyombo vya nyumbani vyote vikiwa mizigo kama 10 vikiwa na thamani ya TZS 4,600,000 ambavyo vilichangiwa na wadau mbalimbali.
Katika Misaada hiyo SimbaNET Limited ilichangia kiasi cha TZS 1,500,000 ambazo zilitumika kununua misaada hiyo. Misaada hiyo kwa upande wa SimbaNET ilikabidhiwa na Sanctus Mtsimbe, Meneja Mauzo na Masoko wa SimbaNET. Kampuni ya simu za Mkononi ya Tigo ilichangia kiasi cha mablanketi 200 yenye thamani ya TZS 1,600,000.
Kampeni ya Kuhamasisha uchangiaji imeshamalizika huku TPN na Wadau wake wakiwa wamechangia misaada yenye thamani ya karibia TZS 20 Million. Jumla ya watu 2000 Walichangia kwa SMS na kiasi cha Shilingi TZS 2,037,332 zimekusanywa.
Misaada yote ambayo imekabidhiwa ni kwa ajili ya wahanga wa mafuriko katika maeneo mbalimbali yaliyoathirika na mvua kubwa.
TPN inazindua Mfuko wake wa Uwezeshaji katika Mkutano Mkuu wa Mwaka utakaofanyika siku ya Jumapili Tarehe 14-03-2010 katika ukumbi wa Blue Pearl Hotel Ubungo Plaza.