mkada
JF-Expert Member
- Nov 14, 2011
- 1,200
- 903
Wana JF,
Nataka kununua gari ya juu, isiyokula sana mafuta na ambayo matumizi yake ni ya mizunguzo ya biashara zangu mjini. Katika pitapita zangu kwenye mitandao nimeona gari ya Toyota Voltz. Hii gari nimeipenda kwa kweli. Nawaombeni msaada kwa waliowahi tumia hii gari au wanajua sifa, tabia na uwezo wake, ikijumuisha mapungufu yake kama yapo.
Thanx in advance.
WADAU WENGINE WANAHITAJI KUFAHAMU NINI?
Amani iwe kwenu wadau. Nimejichanga na nataka kununua gari aina ya Toyota Voltz kwa matumizi ya nyumbani. Itakuwa ikitumiwa zaidi na wife kwenda job na kurudi umbali wa takriban km 40 kwa siku (kwenda na kurudi)
Naomba ushauri juu ya uimara wa hiyo gari, upatikanaji wa spear parts na mambo mnayoona yanafaa kuyajua.
Natanguliza shukrani.
Wadau naombeni kunijuza juu ya ubora wa gari la aina yya TOYOTA VOLTZ imetokea kuipenda kwa ajili ya matumizi ya kawaida ofisini na binafsi. Ila nina wasiwasi juu ya either ubora na uimara wake. mie naishi mabonde kuinama zaidi ya 1,500km kutoka Dar.
Ushauri wenu utazingatiwa sana na mshukuriwe wote.
Wadau habari za hapa?
Ninataka kununua Voltz kwa sababu naipenda ilivyo hata mishe za mjini naona iko poa.
Je, hizi gari zina matatizo gani common na udhaifu wake ni upi?
Msaada
MICHANGO YA WADAU KUHUSU TOYOTA VOLTZ
NI GARI ZURI ILA KUNA WASIWASI WA SPEA KUPOTEA SOKONIHizi gari ukifuatilia historia yake si za toyota na zilitengenezwa na GMC Marekan ili ziuzwe Japan na wakaingia ubia na Toyota kuweka nembo yao tu ili waziuze kirahisi Japan. Ila hakuna mkono wala kifaa cha Toyota pale. Zilitengenezwa gari elfu kumi tu.
Unapoamua kuinunua have idea of that maana nina wasiwasi itafika muda spare zitakua hamna.
Ni gari nzuri kwa mwonekano na mafuta inatumia reasonable.
UZALISHAJI WAKE UMEKOMA, UKILIPATA LITAKUWA KUUKUU MNOKwa mtizamo ni gari zuri, cc zake haizidi 2000cc na engine nyingi zake ni vvt-i model 1 zz-fe maana ni kama za platz, vitz, Ist nk. nk
Down side ni kua magari haya yapo katika phase out huko Japan, hayakupendwa sana na soko lake lilidorora ni kuanzia mwaka 2000- mpk 2003 hivi au 2002 ndo ikawa mwisho wa kutengenezwa, hayazalishwi tena ndo maana lolote utakalo lipata litakua chakavu kwa sheria za Tz yaani more than 10 years since production.
Ninahis lina ubaya wake ila binafsi nililipenda nikajaribu kuangalia experience za watu katika mtanadao sikupata ubaya wake.
I hope this helps
HALINA UDHAIFUNi gari nzuri sana. Haina madhaifu. Ni gari ya Mmarekani imetengenezwa na NUMMI sema ikauzwa kwenye soko la Japan kati ya mwaka 2002 hadi 2004 kwa jina la Toyota Voltz. Awali ilikuwa inaitwa Pontiac huko North America ikiwa na baadhi ya features za Toyota Matrix.
Engine yake haina tofauti na engine ya Toyota Wish, Toyota Spacio ya 1.8 lt na ya Toyota Premio ya 1.8lt. Kuhusu uimara iko vizuri na spare parts zinapatikana coz watu kibao tu wanazimiliki.
NI GARI IMARA. UTUMIAJI WA MAFUTA NI MZURI. NI COMFORTABLEMkuu, Toyota Volz ni gari nzuri sana na imara pia ila uimara wake haufiki kwa Rav 4 old.
Utumiaji wake wa mafuta uko poa kwani ina cc1790 ambayo kawaida inakula 1lt/8-11km kutegemea na mwendo wa dereva.
Kwa upande Confitability iko poa sana ndani ina muundo kama Harrier.
Spear zilikuwa adimu kidogo ila kwa sasa naona zimeongezeka so usijali kuhusu hilo.
NB: Kama barabara unayopita haina shida kipindi cha masika chukua yenye 2 wheel bt kama ni njia zetu zile yenye 4 wheel itapendeza bt ulaji wa mafuta unaongezeka pia.
Ukiwa na swali uliza tu maana naijua vilivyo hii gari
UTUMIAJI WA MAFUTA UPO FAIRUtumiaji wake wa mafuta mi naona uko fair, nikama wastani wa km 11 na 12 kwa lita. Upatikanaji wa taa zake na bampa kwa dar sijui sababu Dar mimi ni wa ubungo posta uwanja wa Taifa nikimaanisha sio mwenyeji, kwa Arusha huku wanasema ni kwa sababu hizo gari hazijawa nyingi ndio maana bampa na taa zake ni ghari. Ila ni gari nzuri na mimi yangu ni 4WD, kwa hiyo ni imara kwenye zile njia zetu.