Toyo iliyogongwa yaleta balaa na mwenye gari aina ya Prado kuikosa gari

Mimi nilishagongwa na Toyo, nikaamua kutokomea wengine wakanilaumu
Sasa matokeo si hayo kujifanya msamalia mwema.
Wale hawana hata chembe ya akili, ni ama wewe au gari yako.
 
Hatimaye mazishi ya marehemu aliyegongwa juzi yamefanyika leo kijijini kwao mkoani Mara na ikiacha majonzi mazito kwa wanafamilia. Marehemu aliagwa jana katika mochwari ya hosptali ya Mount Meru mkoa wa Arusha na safari ya kuelekea Mara ikaanza jana na wakafika salama salimin. Na MUNGU ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amen!
 
Kamanda wakati ajali hiyo inatokea mimi nilikua pale Lapiano baa napata moja moto moja baridi na nilishuhudia ajali hiyo ikitokea sio maeneo ya Silent Inn ni maeneo ya Azimio pembeni ya jengo la Lion Safaris! Kweli ni ajali ya kusikitisha na wale jamaa wa Toyo wanaumoja wa hatari sana baada ya yule kijana kufa walianza kwa kuiponda ile gari aina ya Toyota Prado mayai kwa mawe na bado wakawa hawajaridhika wakaipiga kibiriti na kuteketea kabisa!
Mimi ningewakuta ningefumua vichwa vyao kwa gun.... wapuuzi sana
 
Sasa kumekucha kwa jamaa wa Toyo kwani mwenye prado iliyochomwa ni ya Mwanajeshi JWTZ na hakika habari nilizopata toka kwa walengwa wameapa kwamba waliofanya hilo 2kio lazima awakamate wote. Na msako utaanza kesho j'3 rasmi. Ntawajuza zaidi. Ila inaashiria itakuwa soo kubwa kwa jamaa wa Toyo hapa A town.
Yaa lazima toyo wapigwe ndoa...huwezi chukua sheria mkononi.... nchi hii haijafika huko....ni jambo la kukemea.....tuna mahakama za utoaji haki.... hatuwezi kuishi kwa jungle laws
 
Kamanda wakati ajali hiyo inatokea mimi nilikua pale Lapiano baa napata moja moto moja baridi na nilishuhudia ajali hiyo ikitokea sio maeneo ya Silent Inn ni maeneo ya Azimio pembeni ya jengo la Lion Safaris! Kweli ni ajali ya kusikitisha na wale jamaa wa Toyo wanaumoja wa hatari sana baada ya yule kijana kufa walianza kwa kuiponda ile gari aina ya Toyota Prado mayai kwa mawe na bado wakawa hawajaridhika wakaipiga kibiriti na kuteketea kabisa!
Mwenye kosa nani?
 
Kuna tukio kama hilo limetokea maeneo ya mbezi beach makonde,karibu kabisa na hospitali ya IMTU takribani wiki mbili na ushee zimepita.

yenyewe iliusisha dereva wa toyota hiace kumgonga mwendesha pikipiki, kilichofuata waendesha pikipiki walinza kumfukuzia dereva wa hiace.

dereva baada ya kuona raia wnamfukuzia, akaona heri ya lawama kuliko kuchezea kichapo mzee akapaki gari pembeni na kusepa yeye na konda wake,nakuacha abiria waking'aa macho.

jamaa walivyofika pale baada ya kuona walengwa waliokusudiwa hawapo,walianza kuishambulia gari hatimae kuichoma moto. Hadi leo hii mabaki ya ile toyota hiace yapo pale kama nyumba ya makumbusho. Kwa walio wenyeji wa barabara ya new bagamoyo, baada ya kupita Engen petrol station na kabla hujafika IMTU kama unaelekea tegeta angalia upande wako wa kulia utaona hiyo kitu. Hawa jamaa noma.
Kilichowapata ulikisikia? Mpemba alienda kumshtakia Mungu.....kila aliehusika na kuchoma bio gari alikufa.
 
Back
Top Bottom