Toward South Africa FIFA 2010 World Cup

Hawa upinnzani wao nao ni wa kizamani, ile fujo baada ya mechi yao ya kwanza ilikuwa mbaya sana, fujo mpaka Ufaransa, wapenzi wao wanaonekana wamedata kiaina.
 
Nani atatuwakilisha vyema bara la Africa katika world cup inayokuja, au ndo mambo yaleyale ya robo fainali sherehe?.Sikuhizi visingizio vya refa naona vinapungua kwaajili mpira upo live kwenye luninga zetu, sasa sijui watatupa kisingizio gani wakichemsha mwakani. Nadhani Ivory Coast wana tim nzuri, nawapa nafasi kubwa ya kuingia semi finals. South Africa..mmh!algeria ni under dog, Nigeria na Cameroon wanabidi wajitahidi kujiandaa zaidi.
Je Tanzania tunajifunza nini, apart kuangalia tu kila miaka nenda rudi wenzetu wakiwa wanashiriki mashindano makubwa?.
Kila siku tutaishia Challenge tuuuu hatuendi popote wala nini, hata African cup of nations jamani?majirani zetu wao wanashiriki kama Msumbiji....sisi twabaki kushangilia wenzetu.
 
Ni Algeria!!!!! The Pharaoha wanaback washangiliaji Algeria 1 Misri o

Ushindi mzuri bwana hadi mtoto wa Kiislamu anakupa fingers
_46754116_paris_afp.jpg
 
hata mimi soka la jiana nililipenda sana, kuna mahali kwenye hii thread nilisema kuwa allgeria anashinda

nimefurahi sana
 
Very good Algeria, ingawa mlikuwa 'underdog' lakini mmegangamara. Kudos kwenu!
 
Hapa timu ni nne tu! Ghana,Hiyo ya Drogba, Ya Obi na simba wasiofugwa kidogo..
 
Sauzi,Nigeria,Algeria hamna lolote timu za kuaminika ni Ghana na Ivory Coast tuombee wapangwe makundi mepesi
 
Sauzi,Nigeria,Algeria hamna lolote timu za kuaminika ni Ghana na Ivory Coast tuombee wapangwe makundi mepesi

Timu pekee dhaifu ambayo nina hakika itatolewa kwenye raundi ya kwanza ni Afrika Kusini. NIgeria ina uwezo mkubwa wa kubadilika na kutushangaza, Algeria inauwezo mkubwa na imebadilika sana kwenye miaka hii minne. Ivory Coast bado sio timu ya kutisha haijakamilika sana. Cameroon, Ghana zinaweza kufika nusu fainali, lakini anything can happen. Soka ina maajabu. Inategemea wamepangwa na nani, ukumbuke kuwa hakuna timu hata moja ya Afrika ambayo ni mbegu, mbegu karibu zote ni za Ulaya, na Brazil na Argetina. Timu pekee ya Afrika inayoweza kuwa mbegu ni Cameroon, lakini hata kuwa mbegu kunasaidia tu kwenye hatua ya kwanza.
 
Kila mtu atakuwa na uelewa wake kuhusu hili.Ninachokiamini timu bora ni ambayo itafanya maandalizi ya kutosha ya kuweza kuzitoa jasho timu kama Brazil,Hispania,Ujerumani, Uholanzi na Agentina.Wengi tulikuwa na imani na timu kama Nigeria na Cameroon pekee kwenye kombe la dunia 2006 ambazo zilikosa nafasi ya kushiriki hivyo kukosa imani na timu za Afrika lakini Ghana na Ivory cost walishangaza watu na hadi sasa nazo zipo kwenye timu zinazopewa nafasi ya kufanya vyema.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom