Tovuti ya BBC Swahili wamelala usingizi

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,396


Wameweka links tofauti na habari iliopo ndani.

BBC idhaa ya kiswahili inaonekana katika siku za hivi karibuni kuna dalili za uzembe.

Katika tovuti yake tegemeo kwa waswahili wengi hasa wale waishio nje ya Afrika, kuna habari mbili ambazo ukifungua hazikupi habari halisi.

Kwa mfano kuna kichwa cha habari ya kutaifishwa mali ya kiongozi wa zamani wa Zambia bwana Fredrick Chiluba, lakini ukifungua "link" iliopo unapewa habari kuhusu Nigeria.

Pia habari kuhusu maafa huko China lakini unapewa habari kuhusu mambo ya Burma.

Sasa je wale waliobahatika kupata kazi BBC wamelala au? Hii inaonesha watu waliopewa dhamana ya kusimamia mambo ya tovuti kutokuwa makini na kazi yao.

Angalia tovuti ya BBC kupitia "link" hio hapo chini.

http://www.bbc.co.uk/swahili/
 
Back
Top Bottom