Tovuti kwa ajili ya Vijana

SN_VijanaFM

Member
Mar 25, 2010
58
0
Napenda kuwakaribisha kwenye tovuti ya Vijana FM.

Huu ni uwanja wa watu kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali yanaotukabili vijana; hasa kwenye elimu, sayansi, teknolojia, sanaa, muziki, siasa na mambo mengine kwenye jamii yetu kwa ujumla.

Pia, michango yenu inakaribishwa -- iwe ni makala zitakazozaa mijadala, kusaidiana kwenye kutafuta vyuo n.k.

Tembelea uone kinachoendelea. Mnakaribishwa.

PS: Kwa wale waliokuwa wanaendelea kutembelea vijanafm.blogspot.com, hatuko tena pale. Tumeamua kuonganisha tovuti na blog ili kuongeza ufanisi kwenye mambo ya uhariri wakati tunaangalia uwezekano wa Vijana FM kuwa tovuti inayojiendesha yenyewe.
 
X-Paster, unamaanisha kuwa na Anonymous commenting? Kama hilo ni tatizo unaweza ukaandika "Anon" tu kwenye sehemu ya jina na ukaendelea kama kawaida... Na sio lazima mpaka wahusika waje ku-approve comments.

Au unaongelea user-friendliness nyingine?
 
Nina maanisha kuwa, mtumiaji akitembelea tovuti yenu, hawezi kujuwa wapi pa kwenda mpaka hawe mjuzi wa mambo ya mtandao.
Mfano angalia hii tovuti ya JF, ukitembelea tu kila kitu kinajieleza... Hii ndio tunaita friend user, yaani rahisi kwa mtu kutumia.
 
Nimekusoma vizuri... Ujumbe umefika na tutaangalia nini cha kufanya.

Lakini kwa sasa hivi kuweni wavumilivu na ukitumia sekunde kadhaa tu kuperuzi utajua wapi kuna blogs, contact info, lengo la tovuti, n.k. kwa kutumia icons zilizopo juu..
 
Nimekusoma vizuri... Ujumbe umefika na tutaangalia nini cha kufanya.

Lakini kwa sasa hivi kuweni wavumilivu na ukitumia sekunde kadhaa tu kuperuzi utajua wapi kuna blogs, contact info, lengo la tovuti, n.k. kwa kutumia icons zilizopo juu..
Nimekuelewa mkuu!
 
Back
Top Bottom