Tour fupi ya shamba langu la greenhouse

Mkuu hakika umenipa hamasa...sasa naanza rasmi maana ninaekari 20 tabora na zipo ndani ya manispaa tena barabara ya lami..nimeshajenga nyumba ya mlinzi imeisha na nimeweka solar tayari nilikua nimeanza na vibanda vya ufugaji na mizinga michache ya nyuki..sasa ntaweka mizinga 300 na kuna siku niliwapigia Balton wakanipa bei zao nikaona kama ni ghali kumbe inalipa sana maana walinambia wananipa greenhouse,madawa,simtank na mfumo mzima wa umwagiliaji ndani na nje ya greenhouse. Byebye umaskini

Bro Open Field Kit ni kiasi gani na inachukua ukubwa gani kwa balton
 
Duuh umenifungua akili ila niko mbali na wewe. Niko arusha alafu shamba langu liko karibu na maji kabisa. Nataka kulima nyanya mda si mrefu nasaka hiyo hybrid.
 
1464279520413.jpg
 
Bw. Ngamba umeuliza swali zuri sana, ni swali ambalo watu wengi wamekuwa wanapenda sana kufahamu. Kwa bahati ambayo sio poa wakulima wengi na wale ambao wana mpango wa kulima imekuwa vigumu kwao kupata info sahihi ntalijibu katika vipengele viwili

Mbegu hizi special kama Heirsloom, Corazon, Anna F1, Julia, Carson, Memoneta na n.k zina shelf life kubwa tu na zimeboreshwa kutoka katika nchi za ulaya zenye baridi na zilikuwa maalumu kwa ajili ya kupandea kwenye greenhouse. Sasa waafrika tunafoji na kuamua kuzitumia huku afrika ndio maana wakulima wengi wanalalamika zinawatesa zinashindwa kuvumilia hali ya joto ndio maana zinalimwa Arusha na Nairobi angalau penye kaubaridi

The kick ni kuwa hazikubali nje ya greenhouse yaani kulima kilimo cha wazi. Hii inanyima fursa kwa watu wasio na uwezo wa kifedha wa kujenga gh kushindwa kufanya kilimo cha kisasa na kufanya wakulima wa kawaida kubaki na zile mbegu za kawaida mfano Tengeru na Tanya

Mbegu ambayo mi nawashauri watu waitumia ndio ambayo mie naitumia. Hii imeboreshwa kutoka nchi ya ulaya ambayo iko karibu na bahari ya med. ambalo ni eneo lenye kiwango angalau cha joto. Baada ya hapo ililetwa afrika kusini kuboreshwa Zaidi. Pia ikajaribiwa ktk nchi za afrika ktk gh na kilimo cha wazi. Mbegu hii unaweza ilima ndani ya gh na kilimo cha wazi km ilivyo kwenye hiyo video yangu hapo juu na inavumilia ukame na jotohivyo ni nzuri kwa mikoa yote ya tz
mbona hata hujaitaja sasa hii aina ya mbegu?
 
Mwala juzi nilipata simu kutoka kwa jamaa anaitwa Jackson akitaka nimfundishe haya maujuzi ya kilimo. Nikamwambia aje shamba ajifunze. HaKuja. Sasa leo ananipigia tena akitaka aanze kulima. Akasema ni uoga tu wa kujaribu vitu vipya ndio umekuwa ukimrudisha nyuma.

Nimeamua kuandika haya kwa kuwa nimegundua kuwa watz ss ni waoga wa kujaribu vitu vipya km kilimo n k. Hivyo kuna umuhimu wa watu wrote kujaribu kuondoa uoga na kuamua kulima kisasa. Tusiruhusu kuwa watumwa wa uoga. Tembelea shamba darasa ujifunze
 
Mkuu biashara 2000 ukienda pale balton wanaweza kukuzia vifaa vya greenhouse kama zile UV plastic, drop irrigation... bila ya kutaka wao wa kujengee? yaaan ukitaka kununua vifaa tu wanaruhusu bila wao kuja kukujengea?
 
Mkuu biashara 2000 ukienda pale balton wanaweza kukuzia vifaa vya greenhouse kama zile UV plastic, drop irrigation... bila ya kutaka wao wa kujengee? yaaan ukitaka kununua vifaa tu wanaruhusu bila wao kuja kukujengea?
Yes wanaweza ila wale wa arusha 0719222722
 
Mkuu biashara 2000 zile. mbegu za anna f1 zinakubali nchini kwetu hapa? au ni mbegu gani ya hybrid inayokubali Tanzania kwenye greenhouse?
 
Mkuu kabla sijakupigia simu ili uniweke sawa baadhi ya mambo, naomba kuuliza huko dar mbegu aina ya eden f1 inauzwaje?
Huku arusha gm 50 ni sh 405000/=
 
Habari za asubuhi.

Kwa wale waliotaka angalau kuona kwa ufupi shamba langu la greenhouse ambalo nimelima nyanya ndani ya greenhouse na nje pia yaani bila greenhouse ila kwa kutumia formula maalumu ya kitaalamu ya kutumia gharama kidogo ila mavuno mengi na makubwa wanaweza ku click hiyo video hapo chini na kuangalia.



0758 308193


Mkuu habari

Tafadhali hiki kilimo cha green house kinawezekana kufanyika maeneo ya Dar es salaam, Kibaha au Bagamoyo?
 
Green house inakubal popote tanzania hii sema tutambue watanzania wengi tunatumia walking tunnels sio green house maana green house ni ile inayoweza ku control all weather elements kama mvua,jua,hali ya hewa etc,sasa hizi walking tunnels popote unafanyia kazi sema vipimo vitakua tofauti usitegemee vipimo vya Arusha kufanya vyema dar es salaam
Pili tusiruke hatua ,tafadhar kabla hujajenga green house/walking tunnel pima udongo na maji ujue kweli yanafaa wewe uweke green house /walking tunnels,maana kama eneo lina magadi unalima mazao yanayovumilia kama beetroot bila hata ya kuweka hiyo gh/walking tunnel.
Mazao ya green house ni hoho(za rangi na zile ndefu zenye mchanganyikl wa hoho na kali,nyanya ndefu (indeterminate),tango ,maua hapo itakulipa sio green house/walking tunnel unalimia mboga za majani
 
Back
Top Bottom