Toto la nje ya ndoa ! Khaa!

Judgement

JF-Expert Member
Nov 13, 2011
10,327
4,779
Nimeshaona wazee wa kiume wakiwakataa, watoto walio wapata nje ya ndoa.
Aidha kuna wengine huwakubali, bt kw kificho ambapo inafanywa kua secret kati ya Mama aliemzaa mtoto huyo, Mtoto mwenyewe na Baba muhusika, ili mradi tu Mama aliepo madarakani aendelee kutokujua siri hiyo.
Mzee Ibrahim ni mmoja kati ya wahusika juu ya kadhia hii.
Akiwa ndani ya ndoa na mkewe Mama Pera, Mzee Ibra akawa amepata Mtoto wa kiume pembeni na mji aliokua anaishi.
Shughuli zake za minadani zilimkutanisha na Bi. Sara huko kijijini na kupata kijana aitwae Beka.
Mz Ibra hakutaka kabisa mkewe ajue , hata hivyo alijitahidi sana kua anapeleka kiasi cha matumizi.
Matumizi ambayo hayakua yakikidhi haja.
Kissa mkassa Beka alimlanda Mz Ibra kwa kila kitu, Sura, Umbo, Tambo, Pozi, wajihi wote jumla. Kiasi hata kuwazidi ya waliozaliwa ndoani ufanano na Baba yao.
Kidudu mtu mmoja akatokea na kwenda mueleza Mke wa Mz Ibra, kuhusu Beka.
Katika hali isiyozoeleka sana mkewe Mz Ibra alidodosa chini kwa chini na hatimae akafika kwa Mama wa Beka.
Alifika na kujitambulisha na kumwomba Mama Beka amruhusu aondoke na Beka (age 7) aendenae akalelewe na nduguze.
"Roho inaniuma kuona mtoto huyu upate nae shida kwa kumlea wewe peke yako kwa shida, wakati Babaake ni mwenye uwezo" aliongea Mkewe Mz Ibra maneno hayo.
Mama Beka hakua na pingamizi, alimridhia na akaondoka na Beka.
Mama Pera (mkewe mz Ibra) alifika na Beka nyumbani, hakika Mz. Ibra alifadhaika , kope zikimcheza kushoto kwenda kulia. Hata hivyo mkewe alimfariji kwa kumuondolea mfadhaiko.
Beka alilelewa pale kwa mapenzi yaliotakiwa mtoto apewe.
Hivi niandikavyo Beka ni mfanyabiashara akichukua bidhaa Thailand, China, Bangkok, kuleta Tanzania.
Mama mzazi wa Beka alikwishafariki zamani, Mama pekee anafaidi nguvu ya Beka ni Mama aliemlea.
Nduguze wote aliowakuta kwa Mz Ibra kawafungulia maduka.
Nyumba mpya kawajengea wazazi wake Mbezi beach, na kuwahamisha toka Kawe- ukwamani.
 
Hii ni stori nzuri inayohamasisha upendo kwa wale watoto tunaokosea kwa kuwaita 'watoto haramu' Huyu Bi Mkubwa wa mzee Ibra aliongozwa na hekima nyingi za upendo na matokeo yake ikawa ni hiyo faraja waliyoipata uzeeni.Nilipokuwa naisoma hii stori nilikuwa napumua kwa shida nikifikiri mama ibra alikuwa na nia ya kwenda kumdhuru Beka kama wanawake wengi wafanyavyo.Enyi wanawake, chukueni somo kwenye hii stori.Huenda nyota yako haipo kwenye watoto wako uliowazaa ila ipo kwenye watoto wa nje wa mumeo! Kaichukue nyota yako! Halafu sambamba na hii sgtori ni wale wababa wanaowakataa watoto wao wachanga na kuwaachia mama zao kuwalea. Mtoto aliyekataliwa anachanua ukubwani na kupata nafanikio makubwa. Baba anabaki kulia na kusaga meno.
 
Hamna mtoto wa haramu. Kuna tendo la kujamiana nje ya ndoa ndiyo haram.

Unanikumbusha msanii mmoja wa mziki wa kizazi kipya ambaye story yake kidoooogo yafanana ni hiyo. Au umebadilisha majina tu?
 
kwa mlotoka kwenye tamaduni za mke mmoja.
Polygamy, mtoto ni mtoto na ni faida kwa ukoo mzima na hakuna kuficha. Wote mama na mtoto wanaletwa home.
 
Hivi inakuwaje wanawake wanashindwa kulea watoto wa nje! Huyo mama ni mfano wa kuigwa.
 
hongera mama ibra, hakuna mtoto haramu haramu ni hao waliofanya uzinzi

ila mie wala hujaniletea mtoto ambaye ni zao la wewe kunisaliti!!!!! Ila kama nimekukuta na watoto nitawalea kwa mapenzi yoooooooooteee, kwa maana hiyo huyo mwanamke ana moyo mkuu,
 
kweli background inahusu sana

mmeo akizaa mtoto nje
ukamkataza kumleta hapo kwake
unadhani atakaa na amani wakati mmoja wa watoto wake hayuko naye?

Hivi upendo wa wanamme kwa watoto wao ni tofauti na wanawake?

Je wewe mwanamke ukizaa mtt wa nje afu ushaolewa na mmeo akakusamehe ila akamwondoa mtoto utajisikiaje?

Na je akikubali mtoto huyo aendelee kuishi hapo utasikiaje??

Kwanza kumnyima mme kumleta mtoto wake wa nje ni kumpa excuse ya kwenda kwa mama yake

anyway, social life haina fomula.
 
Yeah Kongosho...

Sawa social life haina formula... Ila tumwangalie mtoto,tumuache mama yake,au baba yake... Yeye wala hana kosa,masikini...
 
nadhani hata makuzi yanachangia
mtu ambaye hajawahi kuishi na step sisters/brothers
inamuwia vigumu zaidi kupokea step kids


kuna dada mmoja aliwahi sema
hawezi kukubali kuzoeana hata na step sister
na anaye mmoja
alivyomfuata akamwambia ishia huko huko
tunashea baba lakini si ndugu

na wote ni watu wazima na wanafanya kazi tena nzuri tu.
Mi nilimshangaa

Ni roho mbaya,unafiki,choyo,kisirani,na yote yanayofanana na hayo......
 
nadhani hata makuzi yanachangia
mtu ambaye hajawahi kuishi na step sisters/brothers
inamuwia vigumu zaidi kupokea step kids


kuna dada mmoja aliwahi sema
hawezi kukubali kuzoeana hata na step sister
na anaye mmoja
alivyomfuata akamwambia ishia huko huko
tunashea baba lakini si ndugu

na wote ni watu wazima na wanafanya kazi tena nzuri tu.
Mi nilimshangaa

Ila,inategemea mama alivyomraise mwanae,au wanae...
Kwanini.... Kama anakujulisha,au unajua tu kuna ndugu yako/zako wa baba mmoja...
Bado katika maongezi,au sura yake kwa mtoto anaonyesha kabisa hataki uwe na taarifa za hao ndugu wengine...

Hiyo inajenga chuki,na mara nyingi mama ana influence kubwa kwa mwanae...
 
kweli background inahusu sana

mmeo akizaa mtoto nje
ukamkataza kumleta hapo kwake
unadhani atakaa na amani wakati mmoja wa watoto wake hayuko naye?

Hivi upendo wa wanamme kwa watoto wao ni tofauti na wanawake?

Je wewe mwanamke ukizaa mtt wa nje afu ushaolewa na mmeo akakusamehe ila akamwondoa mtoto utajisikiaje?

Na je akikubali mtoto huyo aendelee kuishi hapo utasikiaje??

Kwanza kumnyima mme kumleta mtoto wake wa nje ni kumpa excuse ya kwenda kwa mama yake

anyway, social life haina fomula.

Swala la kulea mtoto aliyezaliwa baada ya ndoa ni la binafsi na nyeti sana. . .kwasababu linakua limevunja makubaliano. Ila uliyemkuta na bado ukamkubali mzazi wake hiyo shurti mtu apokee jukumu la kulea maana hajashtukizwa wala hajaletewa kwa lazima.
 
Au la mtoto aliyezaliwa kabla ya ndoa,ila taarifa haikutollewa,kisha mtoto akamitokeza,wakati Mr hayupo...
Scenario hiyo...
 
yaani
utadhani umemtukania mama mzazi
ananuuuuna hadi basi

Siku hiyo patakuwa hapaliki...wala hapalaliki...

Mama m/nyumba: Hilo jambazi hapo nje ulizaa na malaya gani? Nijibuuu...!! Au , Mama m/nyumba: huyo changudoa hapo nje ulizaa na malaya gani?
 
"Man chauvinism @work".
Tunaliangalia hili kwa upande mmoja, mumu kazaa nje ya ndoa, mke wake hana wajibu wowote na mtot huyo (labda huruma na mapenzi binafsi). Wajibu hapo ni wa huyo baba kicheche.

Mnawashauri wanawake wawakubali watoto wa nje ya ndoa wa waume zao, lakini tumewahi kujiuliza ni wanaume wangapi wangekubali mke azae nje ya ndoa halafu mume amkubali mtoto huyo?
 
Kumbe mtoto wa nje anafungua maduka na kusafirisha bidhaa kutoka tailand na china!! ngoja na mimi nitafute wangu watano ili wafungue maduka mengi.
MAPROSOO.
 
Back
Top Bottom