Kwanini benki hakuna vyoo/maliwato kwa ajili ya wateja?

kakamukubwa

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
203
27
1587114913802.png
BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU
Nimefatilia Muda mrefu sana na kubaini kuwa ni karibu Bank zote hazina vyoo vya wateja.
Kwanini?
---
Heshima yenu wakuu.
Moja ya sehemu zenye msongamano mkubwa wa watu ni benki lakini cha kushangaza ni kukosekana kwa huduma muhimu ya choo kwa wateja. Na kama vyoo vipo basi vimejificha sana na ni maalum kwa wafanyakazi wa benki. Hawa jamaa walione hili ni kero kwa wateja hasa siku ambazo kuna foleni humo.

c.c: Patrickn
---
Waziri mwenye mamlaka,asikie kilio chetu.
Vyoo ni muhimu sana bank,unakuta umepewa mkwanja mrefu tu na Bi mkubwa anakwambia nipelekee bank nifate mzigo, sasa ukibanwa na tumbo lzm utafute public toilet kitu kinachohatarisha usalama wa pesa
---
Taasisi nyingi za kifedha zinashindana kwa huduma na kujinadi kwenye upande wa huduma kwa wateja (customer care), ila taasisi hizo ukifika kupata huduma ikatokea ubanwe haja kubwa au ndogo huwezi pata msaada wowote, ukiulizia kwa mlinzi utaambulia kutolewa nje au kuambiwa katafute huko nje, ukiulizia kwa muhudumu wala hawezi kukusikiliza,

Ikatokea umebanwa kiu ya maji, kuna wa mama huwa wanaenda na watoto ghafla mtoto analilia maji ndani ya taasisi nyingi za kifedha huwezi kuta maji au water dispenser iko pembeni kwa ajili ya wateja, sana sana mama huyo ambae ni mteja atatolewa nje na mlinzi na kuambiwa kamuhudumie mtoto nje,

Baadhi ya taasisi mpaka uwe unapata Executive service au premium ndio utapewa huduma hizo sasa huo ni ubaguzi, Premium au Executive customers ni wangapi na normal customers ni wangapi.

Maswali haya ukiuliza baadhi ya watu watakwambia wanahofia Usalama kumpeleka mteja washroom anaweza kuwa na agenda yake binafsi, Je kupanga foleni nakuwasubiri for 3,5,10minutes hawezi kuwa na agenda ya kuwa na subira na kuwavumilia mpaka apate huduma haina maana..?

La mwisho jaribuni kumilikisha customer service yenu kwa staff na sio Walinzi, Walinzi kazi yao ni Ulinzi, Lugha wanazotumia kwa wateja zinakuwa ngumu mpaka mtu unaona uhame tawi au taasisi kabisa...

tuwekeeni vyoo jamani...
---
Habari wakuu? Katika matumizi yangu ya benki mbalimbali, nimegundua kwamba mabenki hayana vyoo vya wateja na ukizingatia kwamba baadhi ya benki zina foleni znazoweza kumfanya mteja asubiri hata zaidi ya lisaa limoja.

Je, ni sababu za kiusalama au kimazingira? Kuna siku nilimshuhudia dada aliyebanwa na haja benki akikamatwa na polisi kisa ameenda chooni.

Karibuni kwa hoja.

===
BAADHI YA MAJIBU YALIYOTOLEWA NA WADAU

Benk nyingi zimepanga kwenye majengo ambayo sio yao, na kwa jinsi majengo hayo yalivyojengwa kuna vyoo tayari vipo kwa ajili ya watumiaji wote wa jengo au ghorofa husika, kwa hiyo ukiulizia watakuonyesha tu. Sio rahisi kuwepo ndani ya bank maana chumba chenyewe cha bank hudesigniwa baada ya jengo kuwa lishakamilika.
---
Moja kat ya BOT inspection before bank haijapewa go ahead kuanza operation ni public toilet kwa ajir ya wateja.

Ni kwel baadhi ya majengo zimejificha ila ukiwauliza walinz wanakuonyesha, kuhusu folen NMB CRDB nsha hama cku nyiiingiii bank ka Exim mpango mzima staff vijana wako sharp n smart brand yao nzur sana kwa kwel hamien huku q management system wanazo pia!
-----
Niliwahi kusikia kuwa ni masuala ya kiusalama zaidi.
Kukiwa na choo wateja wezi / majambazi wanaweza kutumia eneo hilo (choo) kwa kubadirishia sura (kuvaa vinyago) na au kuweka siraha zao sawa humo msalani.
(hapa najiongeza).
---
MeinKempf,
bare this in mind, in most cases there are nearby public washrooms,though not necessarly within bank premises.When dealing with ''people`s money'',security is the utmost priority,.HOW WILL YOU PROVE beyond reasonable doubt,The "FISTULA'' thing,and not a conspiracy for the bandits?.

Remember its a not a healthy institution.Freebooters with unlawful intentions would just formulate excuses to be granted access to key areas and SUCCESSFULLY carry out their pre-drafted missions..
---
Nadhani ni suala la kiusalama zaidi.

Hata majengo ya kisasa kabisa ambayo yanajengwa na miudombinu rafiki hadi kwa walemavu lakini sehemu za bank hawaweki vyoo sehemu inayoonekana na wateja kirahisi (sidhani kama wanasahau)

BTW: Bank siyo sehemu ya ku-deposit uharo!

Hapo ni pesa tu kunya kwenu!
---
Jibu ni rahisi sana ...

Bank zote zipo kwenye majengo na hakuna jengo lisilo na choo, tatizo ni kwamba vyoo vilivyopo sio kwa ajili ya public bali staffs. The same kwa biashara nyingine zote, vyoo vya umma vinapatikana nje na huduma ni ya kulipia, ukikamatika sana sana sana si vibaya ukaanzia huko ndio uingie kupata huduma otherwise, kama ni dharura sana then jaribu kuwasiliana na Meneja huduma kwa wateja, naamini atakusaidia.

Haiwezekani kuweka choo kwenye kila ''frame'' ya duka ama biashara, mwisho wapo watakaotaka pia wawekewe hotel kisha na vitanda then wengine watataka vyote hivyo viwemo pia kwenye saloon, retails shop, wakala, daladala, taxi mpaka na bodaboda

(Ni mtazamo binafsi)
 
Nimefatilia Muda mrefu sana na kubaini kuwa ni karibu Bank zote hazina vyø vya wateja.
Kwanini?

Ndo mazoea ya Watanzania. kama shule zinakosa vyoo iwe benki? hakuna miongozo mizuri ya kusimamia utoaji huduma wa kirafiki kwa mteja.
 
Hili swali nimetumiwa kwenye sms kwa jina la "jahazi" Anyways, ushawahi kuulizau umefuatilia kimykimya?
 
Vyoo vipo unadhani wafanyakazi wanapata huduma zao wapi? Ukibanwa na kuuliza unapata huduma si lazima waandike vyoo vya wateja.
 
Nimefatilia Muda mrefu sana na kubaini kuwa ni karibu Bank zote hazina vyø vya wateja.
Kwanini?
Ulishawahi kujiuliza ni kwa nini sisi wateja tunaziamini sana bank zote na kuweka hela (pengine hata mamilioni ya hela) zetu kwao ila wao hawatuamini hata chembe kiasi kwamba hata kalamu(pen) wanazifunga kamba. Hii imekaaje?

Tukazitoe hela zetu wao hawatuamini hata kidogo!
 
Ila kunapaswa kuwepo vyoo kwa ajili ya wateja kwani bank zingine unakaa sana kupata huduma. Hivyo ni busara kuwa na vyoo vya wateja, hiyo sababu ya ulinzi mimi bado sijaiona kuwa imekaa vizuri kwani wanapoingia hapo ndani ya bank kufanya huduma hawawezi kuhatarisha huo usalama?
 
Ni kwaajili ya security!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Tiririka Mkuu, funguka tujuze, sababu za kiusalama kivipi?!!!, si lazima vyoo viwe ndani ya bank, nadhan hata vikiwa nje, let say jirani na sehemu wanyokaa walinzi wa nje! Pia nimuhimu kuandika huduma ya choo ili watu wajue inapatikana upande upi, nijuavyo mimi hii ni huduma muhimu sana!

Halafu si kweli kuwa wateja hawakai muda mrefu, nakumbuka nilispend 4 hrs NMB Temeke sudan just kudraw hela, nilikuwa nahitaji kiwango zaidi ya kile cha kutoa kwa ATM! Binafsi naona haja ya kuwa na sheria ya kulazimisha bank ziwe na vyoo kwa ajili ya wateja!!
 
Benk nyingi zimepanga kwenye majengo ambayo sio yao, na kwa jinsi majengo hayo yalivyojengwa kuna vyoo tayari vipo kwa ajili ya watumiaji wote wa jengo au ghorofa husika, kwa hiyo ukiulizia watakuonyesha tu.

Sio rahisi kuwepo ndani ya bank maana chumba chenyewe cha bank hudesigniwa baada ya jengo kuwa lishakamilika.
 
Ulishawahi kujiuliza ni kwa nini sisi wateja tunaziamini sana bank zote na kuweka hela (pengine hata mamilioni ya hela) zetu kwao ila wao hawatuamini hata chembe kiasi kwamba hata kalamu(pen) wanazifunga kamba. Hii imekaaje?
Tukazitoe hela zetu wao hawatuamini hata kidogo!
Ha ha haaaa dah!! Ni hivi kwa habari ya kalamu, inafungiwa kamba kwasababu wateja wengi mara kadhaa hutembea bila kalamu, basi ile kalamu isipofungiwa kamba wengine tunaweza kujisahau na kuibeba akija mteja mwingine, atatumia nini? ile ni "public" pen mdau...
 
Je, hili ni tatizo kwa bank za Tanzania pekee? What about our neighbouring contr and abroad?
 
Heshima yenu wakuu,

Moja ya sehemu zenye msongamano mkubwa wa watu ni benki lakini cha kushangaza ni kukosekana kwa huduma muhimu ya choo kwa wateja.

Na kama vyoo vipo basi vimejificha sana na ni maalum kwa wafanyakazi wa benki. Hawa jamaa walione hili ni kero kwa wateja hasa siku ambazo kuna foleni humo.

c.c: Patrickn
 
Last edited by a moderator:
Niliulizaga hili nikajibiwa nikiwa naenda bank natakiwa niwe nimemaliza haja zangu zote!

Unaweza kuchafukwa na tumbo muda wowote au ukabanwa na mkojo muda wowote, benki zenyewe wateja wanakaa katika foleni masaa kibao.
 
Waziri mwenye mamlaka, asikie kilio chetu. Vyoo ni muhimu sana bank,unakuta umepewa mkwanja mrefu tu na Bi mkubwa anakwambia nipelekee bank nifate mzigo, sasa ukibanwa na tumbo lazima utafute public toilet kitu kinachohatarisha usalama wa pesa.
 
Back
Top Bottom