Top Ten footballers Tanzania ever produced

Naona katika majina yenu mmewasahau wakongwe Titus Bandawe na Bwana Mkubwa Yanga Omari na huku Nje kuna Shabiki Mkubwa Hamis Mduruma (RIP),Wakati huo Jumamosi mji mzima unahamia Mkwakwani...
yaani habari za mashabiki unanikumbusha yule wa RELI YA MORO- YA MUNGU......!
Wakati simba inafungwa na yanga JABIR SHIKAMKONO alinyoa nywele.....!
i like this.....!
 
Wengine wanaofaa kuingizwa kwenye Top 100 ni hawa
  • Selestin Sikinde Mbunga- Majimaji
  • Rashid Zito- Majimaji,KMKM
  • Innocent Haule - Small Simba
 
Kule Zanzibar bila kuwasahau Hassan Mrisho "Zitto" Mohammed Rajab, Abdul "Wakati" Jumaa nk
 
Nimeona muanzilishi wa hoja alianza vizuri lakini waliofuata walikuwa wanataja wachezaji wa zamani na sio waliokuwa bora. Hakuwezi kuwa na listi ya wachezaji BORA waliopata kutokea nchi hii bila kuwataja:

1. MOHAMED SALIM - COASTAL UNION
2. MOHAMED cHUMA - BANDARI MTWARA
3. ABDULRAHMAN JUMA 'LINKMAN' - YANGA
4. ALUU ALLY - MSETO/SIMBA
5. MOHAMED RISHARD ADOLF - YANGA/PAN AFRICA
6. YANGA FADHILI BWANGA - COASTAL UNION

7. sasa mnaweza kuendelea kutaja wengine...........
 
Hamna kitu. Walikuwa inconsitent. Kama walikuwa wazuri tumeshinda nini? Tulifika worldcup?

Ushabiki wa kwenye migahawa bana.
 
Mohamed Kachumbari na Ibrahim Mbuzi sijawaona kwenye list. Majina yao yalikuwa yananifurahisha mno.
 
Ally Mchumira, mzee wa mashuti
Katolila,
Beya Simba
Mao Mkami
Ally Yusuf Tigana
Kimti
 
Kwa kumbukumbu zangu kuanzia miaka ya 1970 mpaka wakati huu wachezaji waliokuwa na kipaji hasa cha soka na ambao wangeweza kucheza ligi yoyote ya Ulaya ni hawa:


Mohamed Ali Chuma
Aluu Ally 'Spoiler'
Mohamed Salim - Alikuwa Coastal Union
Jellah Mtagwa
Sunday Manara
Yanga Fadhili Bwanga
Willy Mwaijibe 'The Flying Winger'
Khalid Abeid
Nicodemus Njohole
Octavian Xavier Mrope
Hamis Thobias Gaga
Edibily Jonas Lunyamila
Athumani Idd Chuji
Haruna Moshi


Hawa ndio wachezaji ambao mimi mwenyewe nimewahi kuwashuhudia uwanjani, na niliwakubali/nimewakubali. These players had (have) all credentials for professional football abroad.
 
Kwa upande wa mashabiki pale MAJI MAJI STADIUM ALIKUWEPO MZEE BABU a.k.a Pitiku,huyu mzee alikuwa anleta burudani pale enzi hizo majimaji ikijimwaga alikuwa anacheza na alikuwa na midadi ole wako ukae nae karibu kwani strike akikosa goli naye hufyatua teke loh,nikimkumbuka mzee babua pia namkumbuka marehemu Mzee Gama aliyekuwa hakosi kuhudhuria mechi na wakati huo huo hamza kalala akingurumisha mziki wa kuhamasisha majimjai ishinde na pembeni utamkuta Willy gama mtoto wa marehemu Gama RIP akipiga kinanda,na uwanja ukizizima,jamani enzi hizo we achaa tu,saa hizi pale Majimaji ni gofu
 
Inocent Haule alikuwa Miembeni, na Rashid Lato sio Zito wa Navy kabla ya KMKM,


Zamani tulikuwa na wachezaji wanaojituma, walijulikana Afrika kote kama Dilunga, Mahadhi, Mambosasa,Manara na wengi wengineo, ile ilikuwa ni fahari tu kwa mchezaji
 
Tatizo la mpira wa Tanzania ni kwamba radio tanzania ndio ilikuwa inakuza majina ya wachezaji.Wengi wa mikoani ,tulitegemea masimulizi ya radio tu,huwezi kumwona mchezaji live!
Kwa hiyo tuliwaoverate wachezaji bila hata kuwaona na kulinganisha na wachezaji wengine bara la afrika au Ulaya.
Kuhusu Mohamed China kucheza Uingereza hii ni propaganda kubwa sana!Hata Mwameja alisemekana hivyo.Wahindi wafadhili waliyudanganya sana.

Wanaojua mpira ,ligi top class ni Spain,Italy.England,kidogo Germany na France.
Zingine ni uchwara tu,ila kama una toka nchi maskini ukicheza kama Denmark,Norway,Austria etc sio mbaya kupata pesa kidogo.

Kwa hiyo Kassim Manara kusheza Austria sio deal sana.Ndio maana tumeshindwa hata kucheza Africa Cup of Nations,ina maana wacheza wetu sio wazuri kama tunavyowasifia tangu miaka yote.

Mambosasa tutamjua tu wabongo,lakini ukiuliza Thomas Nkono ni afrika na dunia nzima wanaojua mpira!
 
1.Athumani Mambosasa-If in doubt ask any Egypt's Mehalla el- Kubra 1970's fan.

2. Sunday Manara-First ever Tanzanian footballer to play professional in Europe.

3.Abdallah Kibadeni-Simply King.

4. Gibson Sembuli-Hot shoot Hamish.

5. Maulidi Dilunga-African 11 Captain.

6. Omary Mahadhi-Tanzania One(Original)

7. Zamoyoni Mogella-Golden Boy

8. Gobos-Pioneer

9. Omary Gumbo-Zilipendwa

10. Omary Hussaini-Keegan

- Good idea na heshima mbele sana mkuu, lakini tunapotaka kuwahukumu mashujaa wetu wa shuguli yoyote ile, ni lazima tuheshimu kama ile shughuli inatambulika na dunia, sasa kama tunataka kutoa heshima kwa wacheza bora ever produced by this nation ni lazima kwanza tulenge kwenye sifa zao internationally pia sio nyumbani tu, kwa sababu walishaini hapa nyumbani na hata kutambuliwa nje ya mipaka yetu kama Mwalimu na uongozi wake.

- Sasa ukitumia hiyo standard, Maulidi Dilunga ndiye anakuwa the best ever, maana aliweza hata kuchaguliwa kwenye timu maalum ya Africa nzima na kutuwakilisha kwenye michezo ya mabara ya dunia kule Mexico, ambapo alicheza michezo karibu yote ya ile timu sio kwamba alienda kukaa bench.

- Alipokwenda huko alifuatana na Mahadhi Bin Jabir, ambaye naye pia alichaguliwa kuwemo kwenye ile timu, na alicheza pia katika moja ya mechi zake kule.

- Halafu sasa ndipo anapokuja Sunday Manara, na Kassim Manara, ambao waliweza kuwa waTanzania wa kwanza kucheza Europe kwenye professional ball, baadaye Nico Njohole pia. Pia kuna walioenda Uarabuni kama kina Haidari Abeid, mdogo wake Khalid Abeid, na pia Mohamed Bakari Tall, Jumanne Masuminti, Aluu Ali na Yusuf Kaungu.

- Sasa ndio unakuja kwa shujaa kama Peter Tino, aliyetupeleka Accra kwa mara ya kwanza kwenye finali za Africa kwa timu za taifa, unawakuta kina Zimbwe, Jumapondamali, Mohamed Chuma, Abdallah Kibadeni, Mohamed Salim, Leodgar Tenga, Athumani Mambosasa, Elias Michael, Mwinda Ramadhani, Martin Kikwa, George Kulagwa, Kitwana Manara, Leonard Chitete, Gibbson Sembuli, Jella Mtagwa, Hussein Goboss, Abdulrahman Juma, Shabaan Baraza, Mohamed Kajole, Ahmed Amasha na wengineo, hawa kwa nyakati mbali mbali walituwezesha Tanzania kunyakua ubingwa kombe la challenge na hata ubingwa wa Clubs kwa East and Central Africa.

- Kizazi kipya ni aibu tupu, maana mpaka leo hawajawahi kushinda anything internationally, kwa kifupi ni kwamba hawafai na wala huwezi walinganisha na wale wa kule juu, kwa maoni yangi ni kwamba no way! I mean not even close! Mpira wa manaa wa mwisho bongo ulikuwa ni kati ya Simba na As Vita ya Zaire, nja ule wa Yanga na Enugu Rangers ya Nigeria.

- Jana tu nilikuwa ninaangalia mechi ya FIFA's Clubs World Cup yaani hata timu ya TP Mazembe ya Zaire imo kwenye hiyo michezo inayoendelea sasa kule Dubai, yaani Zaire pamoja na vurugu zote wanazozipitia kisiasa bado wana timu nzuri ya kucheza huko kwenye World, sisi imebakia magomvi tu ya Yanga kandambili na Simba Taliban nonsense!

Respect


FMEs!
 
mimi top ten yangu!
1.Steven Nemesi
2.Keneth Mkapa
3.Willy mtendawema
4.Godwin aswile
5.Salumu kabunda "Ninja"
6. Issa Athumani
7.Sanifu lazaro "Tingisha"
8.Husein Masha
9.Edward chumila
10.Zamoyoni Mogela
11.Damiani kimti.
Wengine:Dua saidi,Twaha hamidu,Abubakari salumu "Sure boy"
KENETH MKAPA, for life...
 
-


- Halafu sasa ndipo anapokuja Sunday Manara, na Kassim Manara, ambao waliweza kuwa waTanzania wa kwanza kucheza Europe kwenye professional ball, baadaye Nico Njohole pia. Pia kuna walioenda Uarabuni kama kina Haidari Abeid, mdogo wake Khalid Abeid, na pia Mohamed Bakari Tall, Jumanne Masuminti, Aluu Ali na Yusuf Kaungu.

Na wengine walokwenda Uarabuni ni Mohammed Salim wa Coastal Union, na Yanga Fadhili Bwanga.

Aluu Ali mtoto wake sasa anacheza mpira UAE na captain wa timu na anachezea national team ya UAE pia.
Mohammed Salim mtoto wake aliwahi kucheza kidogo lakini sasa simsikii tena naona kama mpira kwisha.
Na yuko mtoto moja anacheza pia kwenye timu kubwa huku wanasema ni mtoto wa Yusuf Kaungu lakini not sure.
 
Tatizo la mpira wa Tanzania ni kwamba radio tanzania ndio ilikuwa inakuza majina ya wachezaji.Wengi wa mikoani ,tulitegemea masimulizi ya radio tu,huwezi kumwona mchezaji live!
Kwa hiyo tuliwaoverate wachezaji bila hata kuwaona na kulinganisha na wachezaji wengine bara la afrika au Ulaya.
Kuhusu Mohamed China kucheza Uingereza hii ni propaganda kubwa sana!Hata Mwameja alisemekana hivyo.Wahindi wafadhili waliyudanganya sana.

Wanaojua mpira ,ligi top class ni Spain,Italy.England,kidogo Germany na France.
Zingine ni uchwara tu,ila kama una toka nchi maskini ukicheza kama Denmark,Norway,Austria etc sio mbaya kupata pesa kidogo.

Kwa hiyo Kassim Manara kusheza Austria sio deal sana.Ndio maana tumeshindwa hata kucheza Africa Cup of Nations,ina maana wacheza wetu sio wazuri kama tunavyowasifia tangu miaka yote.

Mambosasa tutamjua tu wabongo,lakini ukiuliza Thomas Nkono ni afrika na dunia nzima wanaojua mpira!

Umenena vyema mkuu...
Mwenye utimamu wa akili atakuunga mkono.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom